Kama unataka kufanikiwa na kuwa tajiri, acha tabia hizi...

Somo zuri mkuu. Kusema na kusikia ni rahisi sana, shida ni utekelezaji wa hayo uliyoyasema. Bila kukandamiza nafsi huwezi kutekeleza hayo, ni lazima ukubali kubadiliko kutoka ndani moyo wako mwenyewe. Vinginevyo ni ngumu mkuu. Tusisahau kutoa Sadaka kwa Mwenyezi MUNGU MUUMBA, ina baraka kubwa sana kwenye mapato yetu
 
Asante sana kwa Elimu nzuri ya kimaisha mimi binafsi nimeipenda sana hii.
 
pia ongezea no. 8, kuchagua mke mwema, maana anaweza kuwa kikwazo kikubwa sana katika kuwa tajiri,
 
Hahaaa aache tabia yakusahau condom KWA michepuko

Ukisahauu hatauwe NA zote hapojuu hunamaana
 
Washauri wengi wa biashara au mafanikio hawajafanikiwa au hawafanyi biashara
 
Kama unamuamini Mungu utakuwa unaamini pia kuwa utajiri hauji kwa nguvu za mwanadamu pekee.
 
nimepata point....

Kuna jamaa yangu, kila nikikutana naye, ananiambia kuna ndoto inanisumbua muda sana, ipo hivi hivi, halafu inajirudia mara kwa mara tu....!

Ndoto inamsumbua mshikaji mpaka kutafuta kazi kashindwa..au akifanya jambo analiachia ktkt, huku akisema ndoto, ndoto, ndoto...!
 
Kuna mada nyingine huwa zinaishia kunitoa machozi tu, zina ukweli asilimia mia moja na moja.....
 
Acha kukopa, acha kujilinganisha na watu, acha ngono, usitumie sukari wala chumvi wala mafuta.

Usitoe pesa kwa mtu yeyote labda awe na shida ya kufa. Tumia nishati nafuu kutokana na mazingira uliyopo. Usinunue vifurushi vya t.v, usinunue CD au kukodi, epuka magomvi.

Asubuhi kunywa maji tuu, mchana kula 1,000/=(kama ni lazima kula).
Usinunue kitu usichokitumia., uza vitu usivyotumia mfano viatu,nguo,vyombo,n.k.

Omba mungu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…