Kama unataka kufanikiwa na kuwa tajiri, acha tabia hizi...

Kama unataka kufanikiwa na kuwa tajiri, acha tabia hizi...

Somo zuri sana ubarikiwe sana. Kwa mtindo huu tutatoka.
 
Aisei, tabia zote ulizoziorodhesha ninazo (weaknesses). Sitakuwa tajiri kamwe.
Ndugu acha kujilaani,mtoa somo lengo lake ni kuhakikisha kila mmoja
anajipima na kubadilika inapobidi,Kama wewe huna mpango wa kufanikiwa
basi familia yako inayahitaji hayo mafanikio.
 
tunashukuruu kwa uzii lakini kuna kitu umesahau apoo!!
 
Kwa mapapaa inakuaje! Mbona wanatumia ovyo pesa zao na bado wanaendelea kuitwa mapapaa
 
Mimi kuna vitu viwili sikubaliani na mtoa mada, ni vizuri tukaviweka sawa Moja point namba sita Acha kuwa na Madeni mengi; kwanza nataka ujue kuna madeni mazuri na mabaya ukitaka kuwa tajiri jitahidi sana kuwa na madeni esp mazuri.

Tofauti ya matajiri na masikini iko hapo! sikuzote umewahi kujiuliza ni kwa nini ina kuwekea riba?? ni kwamba masikini wao huweka pesa benki kwani hawana kazi nazo wakati matajiri huzichukuwa na kwenda kuzifanyia kazi kisha wana rudisha nyingi za kutosha kulipia riba yako na profit ya benki.

Pili ukitaka kuwa tajiri usiogope kuongelea ndoto zako kwani ndizo zitakazo kuamsha asubuhi kila siku kujituma kisha kuzitimiza na cha mwisho usiogope kutumia pesa eti kubajeti tuna shauriwa kuongeza mifereji mingine ya kipato badala ya kujibana matumizi huta kua kiuchumi hivyo ongeza mikondo ya fedha ili ukue Thanks
 
Naamini aliyeniamini atafanyia kazi nami nayafanyiakazi.
 
bonge la somo, uzi kama huu kwa watu wenye malengo chanya lakini uthubutu unawashinda inawafaa sana kwani the good entepreneure is the one who bear risk, usiogope kujaribu hata kama wanakukatisha tamaa kwamba hautaweza.
 
Yaani hii mada imenilenga mimi direct....ee mola nisaidie..nimeshaahirisha project nyingi sana kwa woga
 
unaweza kutimiza zote hizo lakini kama huna tabia ya kusaidia wengine na kutoa sadaka mafanikio yako hayana maana! kuna faida gani ukifanikiwa wewe mwenyewe? matajiri wengi wenye majina pia ni watoaji wakubwa wa misaada na sadaka.
 
Asante mkuu kwa somo zuri.

Nina kitu cha kuongezea hapo, ni rahisi sana kusema acha uvivu, acha kutumia pesa ovyo, anza kuweka akiba n.k

Ila ni ngumu kuacha uvivu au kutumia pesa ovyo kwa kuambiwa tu na mtu. Kuna haja sasa ya kuanzisha somo la ni jinsi gani mtu unaweza kuacha hizo tabia. Mbinu gani zitumike kuacha hizo tabia.

Kanuni kuu ya kuacha tabia fulani ni kuireplace hiyo tabia na tabia nyingine, let's say unataka kuacha tabia ya ulevi ni lazima uwe na tabia mbadala ya kucover nafasi ya ulevi.

Mfano ukiwa na hamu ya pombe, badala ya kunywa pombe ukifika bar anza tabia ya kuagiza juice kubwa zile na ukiweza kufanya hivyo mara kadhaa kwa mwezi ni mwanzo mzuri katika kubadili tabia usiyoitaka.

NB: Kubadili tabia sio jambo dogo hata kidogo.

Tatizo la wengi wanawazia ulevi kuwa ni pombe tu ..... kumbuka ipo pia bangi, heloin, gundi n.k
Ulevi ni ile tabia ya kupendelea jambo kupita kiasi .... wapo wengine ni walevi wa mademu / wanawake
 
Asanate baba paroko!, mm namba 5 inanihusu sana naomba Mungu anisaidie sana. Mapato sisimizi matumizi Tembo, dah!. Naomba unishauri kwa hapo tu, kuna baadhi ya miezi nikianza kupiga hesabu za matumizi yangu huwa nakuta natumia hadi 1M na nipo peke yangu (Bachelor) naishia kuhuzunika, natafuta mchawi wa maisha yangu tu!!. Hebu nishauri kwa PM
Kila tumizi lako liandike kwenye diary yako.
Hakikisha kila unapotaka kulala unahesabu hela ulopata na kutoa uliyotumia hili kujua upotevu wa pesa yako.
Kamwe huwezi kutunza pesa hadi siku utakapojua wapi inapotelea.
 
Back
Top Bottom