Ni bora kubaki single kuliko kulea bao la mwanaume/wanaume wenzako
Siku ukiwa unaoa nenda kamwambie mama au dada zako unaoa single maza watasikitika na kukushangaa sana
Hata kama mama yako alikulea akiwa single maza hakuna siku atakuuunga mkono uoe single maza mwenzake anaweza akalia sana
Ndio ujue wanawake wanajuana
Mungu naye akiwa mbinguni anakushangaa na kukuona mjinga, amemuagiza mwanaume aanzishe familia yake wewe unaenda kujiunga kwenye familia ya mwanaume mwenzako!
Imagine siku umemuoa single maza halafu unawatembelea wazazi wako ukiwa na watoto wa mwanaume mwenzako. Then unawaambia watoto wa mwanaume mwenzako msalimie bibi na babu yenu. Lazima baba yako na mama yako wakuone mpumbavu na mjinga, a useless son.
Ni mwanaume mpumbavu tu ndiye anayeoa single maza.
Learn or perish
Kuna member hapo juu kasema vizuri sana. Kila mtu ashike analoona litamfaa. Oa yeyote. bikra, single mumy, ajuza au hata kuacha, acha tu.
Familia moja kijana alitangaza kuoa single mumy. Mama mzazi nusuru azimie kwa kilio kupinga kijana wake kuoa single mother. Kijana akisimamia msimamo wake na alioa.
Baadhi ya ndugu walimtenga kijana kiaina. Wazazi wa kijana hawakuwa na upendo kwa mke wa kijana wao. Waliishi nae basi tu ashaolewa na mtoto wao.
Kijana wa pili alitangza kuoa binti ambaye alianzisha yeye binti akiwa sekondari. Sifa zikawa sifa kwa kijana kuleta chombo kipya. Akapendwa kijana na mkewe. Wakafanywa kuwa watoto wenye hekima na ndoa ya mfano.
Siku hazikuganda. Kaka na mkewe waliokuwa hawaishi pale kijijini walijaliwa kupata mtoto. Lakini hakuthaminiwa sana. Lakini hakujali, walimlea mtoto wao pamoja na yule wa kufikia kwa upendo wote. Maisha yao yakawa ya amani ndani na nje. Heshima na upendo kati yao vikawa nyota angavu..
Kwa upande wa mdogo, baada ya muda kukawa mushkeli kidogo. Baada ya kupata mtoto wa kwanza vizuri, mke alianzisha mchezo mchafu. Mara alibeba mimba nje ya ndoa. Akaona ataumbuka. Akaamua kuitoa mimba. Mambo yalipokuwa magumu, alipelekwa hospitali. Kama kawaida ya manesi, walimbana aseme ukweli. Akasema katoa mimba na sababu ni kuwa haikuwa ya mumewe. Ile ndoa kwa sasa kauli ya mwisho bila kujali ubora, msemaji ni mke. Kijana kawa poyoyo kiasi kwamba mke alale asilale nyumbani, mume haruhusiwi kuhoji.
Naunga mkono jamaa aliyesema kila mmoja afanye analoona linafaa. Ukipata chema asante Mungu, ukipata koroma bahati mbaya.
Jioni njema member wote.