Kama unataka kupunguza umasikini fuga kuku chotara na kama unataka kufanya biashara fuga Kisasa

Kama unataka kupunguza umasikini fuga kuku chotara na kama unataka kufanya biashara fuga Kisasa

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Kwanza ieleweke kwamba kuku chotara ni kwa ajili ya kupunguza umasikini na si kwa ajili ya Biashara.

Ukisoma hata andiko la ku introduce Kuroiler kule Uganda ilikuwa ni kwa ajili ya kupambana na umasikini kule Uganda.

KWA NINI SIO MBEGU ZA BIASHARA?
1. kwanza ni performance yao kwenye utagaji kuwa ni ndogo kiasi kwamba haowezi kidhi demand.

2. Ukuaji wao pia.

3. Ni breeds ambazo hazitaki kuzaliana na hapo ndo kosa kubwa sana linapo fanyika.

COMMERCIA BREEDS.

1. Layers

2. Broiler.

Hawa ndo kuku wa biashara achana na story sijui za.kubeba tenga la kuku kutoka vijijini kuja sokoni.

Layers ni kuku wa mayai na mayai yao ndo the most consumed mjini. Na production yao iko juu pia.
Mayai ya layers yanatumika sehemu zifuatazo.

1. Bekary au watengeneza keki.

2. Chips

3. Viwandani.

4. Mahotelini.

Usitarajie eti kiwanda cha keki kiahize mayai ya kienyeji kutengenezea keki never.

BROILER- Hawa ndo kuku wenye soko kubwa na wanao liwa kwa wingi sana.


Kama unataka kupunguza umasikini fuga Kuku chotara ila kama unataka kufanya biashara fuga kuku wa mayai au wa nyama wa kisasa.
 
Asante Kwa mawazo haya, hapo katika fungu la Kwanza,

Kwanini hawa kuroiler kwenye kutaga inakuwa shida?
Ni chotara na pia sio watagaji wazuri. na pia unakuta wamezaliana.

Chotara hataki kuzaliana kamwe.

Chotara fuga Kizazi cha kwanza kama hakuna basi Fuga hata Broiler au Layers
 
Ni chotara na pia sio watagaji wazuri. na pia unakuta wamezaliana.

Chotara hataki kuzaliana kamwe.

Chotara fuga Kizazi cha kwanza kama hakuna basi Fuga hata Broiler au Layers
Asante Kwa darasa,

Kwanini wasiwe wa biashara?
 
hao kuku unaodai ni wakibiashara mara nyingi humpa faida mfanya biashara na sio mfugaji ukitulia ukapiga hesabu ya matumizi ya pesa utayotumia kuwa tunza toka wakiwa vifaranga hadi kupeleka sokoni kuuza 4500 au uuze mayai utajikuta hela yote ya mayai inaishia kwenye kuwatunza kuku bado muda na care ya nguvu utayotumia kuwatunza maana bila uangalizi huambulii kitu.
Biashara ni Sayansi. Elewa kwamba wale ndo kuku wa biashara. Maysi ya Chotara au kienyeji yanaliwa wapi?

Kuna viwanda vinayatumia?
 
Asante Kwa darasa,

Kwanini wasiwe wa biashara?
Wana kosa vitu vingi sana kuanzia Production ya mayai hadi ukuaji na kadhalika.

Wewe fanya uchunguzi mbona rahisi sana?

Zunguka maeneo ya mjini tembelea viwanda vinayo tumia mayai pia tembelea vibanda vya Chips, ukitoka hapoa nenda Hoteli kubwa pia nenda Sokoni.Pia tembelea Sherehe kubwa kubwa zote kama Harusi au semina sijui angalia aina ya kuku wanao liwa pale na kwa nini

Kuku kienyeji na mayai ni kwa home Consuptions.

Tena kwa kiwango kidogo sana.
 
Ni chotara na pia sio watagaji wazuri. na pia unakuta wamezaliana.

Chotara hataki kuzaliana kamwe.

Chotara fuga Kizazi cha kwanza kama hakuna basi Fuga hata Broiler au Layers
Mkuu naomba ufafanuzi kidogo hapo kwenye kizazi cha kwanza, wa kizazi cha kwanza wanatoka wap na wakizazi cha pili wanatoka wap! Nin faida ya kizazi cha kwanza?
Pili, ukimumuwekea kuku wa kienyeji mayai ya chotara hawaatamii?
 
Kuku chotara wanafaa wote kwa biashara inategemeana tu unataka kuwafanya kuwa wa nyama au wa mayai km ni wa mayai ndani ya wiki 18 tu km unamlisha vizuri ataanza kukupa mayai kwa faida, na mayai yake utayagroup kwa mayai ya kienyeji,n km tunavyofanya mayai ya kuku wa kienyeji bei yake tofauti na layers wa kawaida kwa apo unaweza ukafuga kwa faida kubwa sana, pili awo kuku pia unaweza ukawafuga km kuku wa nyama na ndani ya izo week ukaanza kuwauza kwa bei ya kuku wa kienyeji na faida ukapata, kwa ufupi unaweza kumaliza umaskini na kupata kipato kikubwa sana.
 
Kwa uzalishaji wa bidhaa yoyote kibiashara iwe kilimo ama ufugaji ni vema kuzingatia vipengele hivi:-
1. Product (bidhaa)
2. Price (bei)
3.Promotion(matangazo)
4. Place (mahali)
5. People (watu unaowalenga).
Ukizingatia hayo iwe kroiler, broiler ama layer mambo yataenda
 
Back
Top Bottom