Huu uzi naufatilia kitambo na nimezidi kugundua kuwa wabongo wengi tunafeli kwenye ujasiriamali pamoja na sababu nyingine kwamba tunafanya mambo kwa kufuata uelekeo wake badala ya malengo na msingi wake.
Hii ndiyo sababu utasikia kauli kama "kuku wa kienyeji hawalipi" au "mayai ya kienyeji ni biashara kichaa".
Mimi sikutaka kabisa kusikia negativities za aina hiyo hivyo kwa mwaka mzima 2019 nilikuwa nikifuga kuku mchanganyiko, chotara na kienyeji. Lengo la mradi wangu ni pamoja na mambo mengine kutatua changamoto ya upatikanaji wa mayai na kuku wa kienyeji.
Masoko yake ni makubwa sana na yanakua kila siku. Mimi huwauzia mayai ya kienyeji wateja wa nyumbani/households ( watumishi, wafanyabiashara, nk) na wateja wa jumla (maduka/kiosk). Changamoto yangu kubwa kwa sasa ni uzalishaji mdogo. Immediate demand ni zaidi ya trei 10 na uwezo wangu ni pungufu ya trei 3/siku.
Lengo langu ni kuona kuwa 2020 inaisha nikiwa nazalisha trei 10/siku na trei 100/siku mwishoni mwa 2021.
Kwa sasa nimeishiwa kuku wa kienyeji kwa ajili ya nyama kwani sukuwa na uwezo wa kuzalisha wengi awamu ya kwanza. Hivyo nimeanza upya kuzalisha kundi jipya ambapo sasa mradi utakuwa non stop.
Changamoto yangu kubwa kwa sasa ni ukubwa wa soko. Yaani wateja wanataka kuku na mimi sina. Siku hizi nyama choma hawataki tena kuku chotara au wa kisasa bali wanataka kienyeji pure.
Kuna tofauti kubwa baina ya MJASIRIAMALI na MFUGAJI TU WA KAWAIDA. Mjasiriamali huyakita malengo yake kwenye kutatua changamoto flani (kuleta ahueni na kuleta manufaa) ilhali mfugaji wa kawaida (mfanyabiashara) hujenga shughuli yake kwenye msingi wa faida (kupiga pesa haraka haraka).
Ukiwa na module nzuri itakayotatua tatizo flani automatically utapata faida tena endelevu.
Kwa mfano. Watu wa nyama choma na sherehe wanapohitaji kuku hupata changamoto kama vile ubora duni wa hao kuku wa vijijini, mara nyingine hawapatikani "on demand", wakiwa wazuri bei huwa siyo rafiki, nk. Sasa ukiwa na mradi wako mzuri utaosolve hizo changamoto lazima ufanikiwe.
Mambo kadhaa ya kuzingatia unapofuga kuku wa kienyeji;
Kwa biashara ya mayai hakikisha unachagua breed inayotaga mayai mengi. Mfano mimi nilianza na breed nyingi lakini mwishowe nikachagua wale "kuku weusi wa Malawi" yaani Black Australorps. Pis kuna breed kama "salu" (manyoya yao husimama kuelekea juu) au wale wenye manyoya kama sufu.
Kwa kuku wa nyama chagua breed zenye maumbo makubwa kama vishingo, salu, kuchi, nk.
Pia hakikisha unatumia module itakayokupunguzia gharama lakini kukupa ubora wa kuku yaani nusu huria. Ukiwa na eneo kubwa waweza tumia huria pekee (rejea post/maada za
Kubota kwenye ile sticky thread ya ufugaji wa kuku wa kienyeji).
Binafsi naiona future kubwa sana kwenye huu ufugaji wa kuku wa kienyeji.
Sent using
Jamii Forums mobile app