Chasha, natambua wewe ni mfugaji mzuri wa kuku chotara kupitia taarifa zako hapa jukwaani. Naelewa unazungumza kwa uzoefu.
Katika hili, nitakuwa tofauti na wewe kidogo. Biashara huendana na mazingira yanayokuzunguka. Kuna mazingira ambayo broiler hawawajui hata kidogo, hususani miji midogo, ambapo maeneo kama haya, yanayotegemea kuku wa kienyeji tu, kuku chotara Ukiwafuga kibiashara watakulipa sana.
Mbali na mazingira, mikakati ya biashara hutofautiana mtu mmoja hadi mwingine. Tatizo ninaloliona hapa umezungumza kwa ujumla sana, pengine kwa kudhani biashara ya ikileta matokeo mabaya kwako basi itakuwa kwa watu wote. Hapana. Na hii inakuja kwa kujiamini kupita kiasi.
Nadhani ingetosha tu kutia uzoefu wako kuwa kwa upande wako, biashara ya kuku chotara imeenda ndivyo sivyo na sio kutamani uzoefu wako uwe princple kwa wote.