Kama unataka kuwa na akili kubwa ya maisha na biashara kuliko wasomi, nenda Kariakoo kauze hata maji kwa miaka mitatu badala ya kwenda chuo

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Zaidi ya 90% ya vijana wanaokwenda chuo siku hizi wanakwenda kupoteza muda wao na kutengeneza mazingira ya kuwa frustrated siku zijazo.

Siku hizi hata ukimaliza chuo na ufaulu mkubwa unatakiwa uwe na bahati kubwa sana ili uweze kupata ajira.

Badala ya kupoteza muda mwingi na fedha nyingi kwenda chuo ni bora ukaenda Kariakoo ukaanza kufanya biashara yoyote ile unayoweza kufanya na kwa mtaji wowote ule ulionao.

Fanya hata biashara ya kutembeza maji ya kunywa tu na endelea kujijenga katika biashara yako bila kukata tamaa utaniambia baada ya mwaka, miwili au mitatu rafiki zako waliokwenda chuo watakuomba uwarushie mia.

Usipoteze muda na fedha zako kwenda kujitayarishia frustration na kuchelewa kimaisha ukitafuta elimu isiyo na manufaa maishani.

Yatosha tu siku hizi kuwa na fedha za kukidhi mahitaji yako kwani ni fedheha kubwa kuwa na elimu pasipo kuwa na fedha.

Kumbuka kuwa hata hao wanaokwenda chuo mwishowe wanatarajia wataajiriwa na kupata fedha. Kwanini usianze kujiajiri mwenyewe sasa kuliko kusubiri hadi upoteze muda na fedha zako kwanza?

Ukitaka nenda kasome baada ya kuwa na uchumi wa uhakika utafurahia maisha yako zaidi.
 
Elimu ni mbaya kama unayo.. lakini ni bora ukawa na elimu ukakosa fursa ya ajira kuliko kupata fursa ya ajira huna hiyo elimu Maumivu yake ni makali mno..bahati mbaya ss huwezi kurudi kuitafuta tena...unaweza miliki ukwasi still ukaihitaj elimu maana utaketi na watu wakubwa kichwa ikiwa empty uwezo wa kureson kisomi kama wakubwa utakuwa huna na watakutambua tu kuwa jamaa shule hakuna..tusiibeze elimu kiasi hicho as if ni kitu hakina maana kwa kuwa tu hujaajiriwa tungalie kwanza faida ya elimu kwa kutoa ujinga mengine nature ya mazingira itakushape mtaani kulingana na struggle za mtu binafsi..kwa mtazamo huo unawakatisha tamaa wenye nia ya kupambania ndoto zao kielimu kwa kuhisi mambo ni magumu kiasi hicho..hakuna aijuaye kesho
 
Elimu ya muhimu ni elimu msingi tu , unajua kusoma na kuandika unajua mahesabu na angalau lugha ya kimataifa kiengereza , hzo zengne mbwembwe tu za kusoma mpka chuo afu ajira bahati nasibu na ushatumia fedha nyng kusoma
 
Binafsi sijutii elimu niliyoipata na wala sitawakatisha tamaa wanangu ..ntawatia moyo nitawaeleza ukweli soko la ajira lilivyo wasome wakijua hilo..mengine anapanga Mungu
 
Elimu ni muhimu tu,hakuna namna yoyote ile ya kuikwepa.hata maandiko matakatifu yanatuambia,MSHIKE SANA ELIMU USIMUACHE AENDE ZAKE.
 
Elimu ni mbaya kama unayo.. lakini ni bora ukawa na elimu ukakosa fursa ya ajira kuliko kupata fursa ya ajira huna hiyo elimu Maumivu yake ni makali mno..bahati mbaya ss huwezi kurudi kuitafuta tena...unaweza miliki ukwasi still ukaihitaj elimu maana utaketi na watu wakubwa kichwa ikiwa empty uwezo wa kureson kisomi kama wakubwa utakuwa huna na watakutambua tu kuwa jamaa shule hakuna..tusiibeze elimu kiasi hicho as if ni kitu hakina maana kwa kuwa tu hujaajiriwa tungalie kwanza faida ya elimu kwa kutoa ujinga mengine nature ya mazingira itakushape mtaani kulingana na struggle za mtu binafsi..kwa mtazamo huo unawakatisha tamaa wenye nia ya kupambania ndoto zao kielimu kwa kuhisi mambo ni magumu kiasi hicho..hakuna aijuaye kesho

Kishimba unamzungumziaje ?

Hawezi kukaa na watu wakubwa na hawezi ku reason ?
 
Back
Top Bottom