Kama unataka paa lako liwe imara tumia mbao za mlingoti

Mbao C ndio mkaratusi...

Huwa zina mafuta fulani ambayo huchefua wadudu kuweza kuitafuna...mafuta ya huu mti pia hutumika kwenye kutengeneza dawa za mafua kama vicks



Na picha ya chini hapa ndio mti wa mkaratusi/mlingoti...

Kama ni hii basi huitwa pia Eucalyptus.
 
Huo mliingoti utautambuaje na una uzwa wapi wa hapa Dar es Salaam?
Chanika zinapatikana. Licha ya ubora wa Hali ya juu ya mbao hizi, mafundi wengi hawatakuambia uzitume. Nilipokuwa Nataka kuezeka ndipo nilipozitambua hizi mbao. Mafundi wengi niliozungumza nao hawakuzipendekeza Kwa maslahi Yao. Ila fundi mmoja ndiyo anapenda kuzituma hizo mbao. Alipokuja tu kufanya tathmini, hata kabla ya kumwambia kuhusu mbao hizo ni Yeye aliyependekeza zitumiwe hizo Kwa ajili ya ubora. Ana usemi anapenda kuseka, ukituma mlingoti uliokomaa, bati zitaisha, utazitoa na kuweka nyingine na zitaisha tena huku mbao zako Aiko vilevle.
 
Haswa haswa upate ule mlingoti unaoitwa gamzi daaa ni chuma balaaa
 
Mafundi hawapendi kuzitumia sababu ya kuwa zinatumia muda mwingi kunyoosha
 
share namba zake tucheze nae
 
Bei ya kupaua lazima iwe kubwa na uzipate mbichi, hizo mbao mafundi wanazikwepa kutokana na hii misumari ya kibongo inapinda sana
 
Bei ya kupaua lazima iwe kubwa na uzipate mbichi, hizo mbao mafundi wanazikwepa kutokana na hii misumari ya kibongo inapinda sana
Hilo ndio tatizo kuu la mlingoto ukikauka , pia ni mbao nzito sana nyumba iwe imejengwa imara huko chini la sivyo itayumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…