Watu wajifunze, hasa hawa chawa na wazee wapumbavu wasiotaka kujua dunia inakwendaje.
Kwa dunia ya leo ni ujinga kuyakataa mabadiriko, kuna muda ni lazima watu wakubaliane na uhalisia, kama mtanzania ni muda sasa wa kujifunza mambo mapya na fursa mpya za kiuchumi hasa ktk hiki kipindi kigumu ili ujikinge na lawama hapo baadae za kusema NINGEJUA, fanya sasa.
Kuna siku si siku uchumi wa hii nchi utayumba vibaya, kuna Institutes zitadrop financially, kuna watu kazi watakosa, then BOOM mfumuko wa bei, hapo ndipo mtaona kila kitu kinapanda bei, kuanzia nauli(mafuta), bidhaa na huduma zote, soko la bidhaa za nje kupata mtikisiko sababu ya kukosekana kwa pesa za kigeni/pesa ya nchi kushuka thamani, kuongezeka kwa kodi na gharama za maisha kupanda wakati huo kiwango cha mapato ni kile kile kikizidi kuanguka.
Ni wakati sasa vijana kwa wazee jifunzeni fursa mpya za dunia ya kidigitali, tafuta maarifa ya Foreign currency exchanging, Cryptocurrency opportunity, bila kusahau fursa za mauzo na uwekezaji wa hisa za makampuni yanayoeleweka,
La mwisho maono ya kujua tupo katika ulimwengu unaotaka nini na nini kisichotakiwa, tuache ubishi na kupuuza mambo, kama serikali hii itaendelea kushupaza shingo, basi tutegemee anguko la uchumi kwa % kubwa, na baadhi ya wanasiasa lawama hizi watazibeba na hazitaishia kwao tu bali zitazitafuna mpaka familia zao.
Twendeni tu, wabishi watatubu hivi punde.