Kama ungekuwa na mtaji wa Tsh 200,000,000/=, ungeanzisha biashara gani Dubai?

Kama ungekuwa na mtaji wa Tsh 200,000,000/=, ungeanzisha biashara gani Dubai?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,645
Reaction score
10,867
Kuna mtu atasaidika na mchango wako wa mawazo.

Inawezekana milioni mia mbili ni kidogo sana kwa uwekezaji nje ya nchi, lakini pengine bado zinaweza zikafanya kitu.

Nilishawahi kumsikia binti mmoja akisema anamiliki saluni jijini Dubai. Simkumbuki jina, lakini anaishi Dar Es Salaam!

Ingelikuwa una milioni mia mbili, na ukaamua kwenda kuanzisha biashara Dubai, ungewaza kufanya biashara gani?

ANGALIZO: Lazima ofisi za biashara ziwe Dubai.
 
Nunua bidhaa za nafaka ,matunda na viungo kutoka Tanzania na upeleke kwenye masoko ya dubai
 
Nunua bidhaa za nafaka ,matunda na viungo kutoka Tanzania na upeleke kwenye masoko ya dubai
Bora biashara za aina hii unaweza ukafanikisha.
Lakini kwenda na hela Dubai uchukue fremu uweke bidhaa tofauti na hizi za asili ya nyumbani huwezi kutoboa hata uwe na bilioni 5.
Biashara za Dubai ziko very strategic and competitive ukienda kufanya kwa mtindo wa kibongo umefungua fremu halafu unangojea wateja waje tayari umeshafeli.
Hapa mtu anaweza akaniuliza umejuaje kuwa jamaa atafeli au unajuaje kuwa jamaa atafanya kwa mtindo wa kibongo?
Jibu lake ni jepesi tu kama ifuatavyo;
Kitendo cha mtoa mada kuuliza kwamba mtaji wa milioni 200 inatosha kuanzisha biashara Dubai?tayari inaonyesha wazi hana utaalamu wa biashara,kitaalamu kwenye biashara yoyote cha kwanza unatakiwa uwe na idea ya biashara,cha pili strategies za kuifanya hiyo biashara,cha tatu connections za wateja ishu ya mtaji ndio inafuata baadae.
Kwa mentality hiyo hautaweza kupambana na wahindi ambao kwa asilimia kubwa ndio wameshikilia soko Dubai na wanafanya biashara kwa mbinu za kisasa za marketing kama unajua kitu kinachoitwa Digital marketing/Artificial Intelligence marketing Dubai ndio ipo applicable kwa asilimia 100.
Kitu kingine ambacho kinafanya soko la Dubai kuwa gumu mauzo ya Dubai yanategemea Taifa ambalo umetoka kwa lugha nyepesi yaani watu wanaungishana kwa mataifa yaliyotoka kwa mfano kama wewe umetokea Tanzania au Sudan kwa asilimia kubwa wateja wako watakaokuungisha ni watu waliotokea Tanzania au Sudan ikizidi sana utapata wa ziada kutoka Kenya au Burundi kwa sababu cultures zetu zinafanana that means hakuna possibility za mtu wa kutoka India/Pakistan au Afghanistan kuja kununua bidhaa kwako so kwa miaka ya mwanzo utakuwa unalipia leseni bila mauzo ya kutosha gharama ya leseni kwa mwaka kwa makadirio inacheza katikati ya milioni 10 hadi milioni 35 za kibongo kutegemea aina ya biashara na location ulipofungulia biashara plus kodi ya pango ya fremu ambayo inaanzia milioni 2 hadi milioni 6 za kibongo kwa mwezi na kuendelea kutegemea ukubwa wa fremu na location ilipo fremu.
Sasa wakati huo unaanza kuwatafuta Watanzania wenzako wakuungishe ambao wako asilimia chache tu na hata hao asilimia chache ni watu wa kujificha sana sio rahisi kukutana nao then fikiria machungu wa hizo gharama za kodi na leseni unazolipia unaweza ukalia na kusaga meno.
Kwa sasa niko na hayo machache tu muda hautoshi kuelezea zaidi ila mambo ni mengi sana.
 
Safi sana, napenda sana mtu mwenye fikra na uthubutu kama huo.

Changamoto kubwa za biashara za dubai kwa sisi ni kuwa mazingira ya dubai ni muhimu sana kupata watu wajamii yako kukuunga kwenye biashara yako, Tatizo kubwa ni kuwa watanzania hatupo wengi dubai, hilo linatufunga kupata fursa nyingi sana mana fursa nyingi kule huzaliwa kupitia uwepo wa watu wa jamii yako. kuna wanigeria wana survive dubai kwa kuuza mama ntilie au kupanga mafungu ya vigimbi tu mitaani kinyemela kinachowasaidia ni uwepo wa wanigeria wingi kwenye ule mji kwahio huwa wanaungiana, kuna wadada wa kisomali na wakisudani wanauza samabusa na maandazi tu na maisha yanakwenda kwa sababu ya mazingira hayo hayo.

Biashara ambazo unaweza kutemebea nazo kwa hicho kiwango chako.

Grocery / mini market. - Hii haina bwana, ukipata location tu unapiga, na uzuri wa Dubai location sio isue kubwa mji wenyewe tayari location.

Restaurant. - usifungue direct African restaurant, tafuta wapishi wahindi/ pakistani upike vyakula vyao, huku vyakula vya kiafrica ukianza kuvichomekea kidogo kidogo.

kuhusu Saloon za kike na kiume ni high risk, mana lazima ue na guarantee ya kupata wa east africa wa kukuungia, ila ya kike ni nyepesi zaidi unaweza kupata mashot waki west Africa kiharaka zaidi. ila kwa wanaume sio wepesi kabisa.

Clearing agent haifai kabisa competition ni kubwa sana

Option nyengine ni Gym, hii ni nzuri kidogo mana ni rahisi kuwapata wa west africa na wa Ethiopia. mana sio wengi katika wao wanamiliki biashara hii kwahiyo wengi wao hujiingiza kwenye magym ya wahindi, wa far east na waarabu. kwa hapa unaweza kuwapata.

Ukiweza kupata mchongo wa kupeleka vitu kule ni bora zaidi.

Na kwanini lazima Dubai? Kwanini usianzie Sharjah? kupo alot cheaper utapata kuufahamu mji vizuri ili upande kwenda stape by stape.
 
Safi sana, napenda sana mtu mwenye fikra na uthubutu kama huo.

Changamoto kubwa za biashara za dubai kwa sisi ni kuwa mazingira ya dubai ni muhimu sana kupata watu wajamii yako kukuunga kwenye biashara yako, Tatizo kubwa ni kuwa watanzania hatupo wengi dubai, hilo linatufunga kupata fursa nyingi sana mana fursa nyingi kule huzaliwa kupitia uwepo wa watu wa jamii yako. kuna wanageria wana survive dubai kwa kuuza mama ntilie au kupanga mafungu ya vigimbi tu mitaani kinyemela kinachowasaidia ni uwepo wa wanigeria wingi kwenye ule mji kwahio huwa wanaungiana, kuna wadada wa kisomali na wakisudani wanauza samabusa na maandazi tu na maisha yanakwenda kwa sababu ya mazingira hayo hayo.

Biashara ambazo unaweza kutemebea nazo kwa hicho kiwango chako.

Grocery / mini market. - Hii haina bwana, ukipata location tu unapiga, na uzuri wa Dubai location sio isue kubwa mji wenyewe tayari location.

Restaurant. - usifungue direct African restaurant, tafuta wapishi wahindi/ pakistani upike vyakula vyao, huku vyakula vya kiafrica ukianza kuvichomekea kidogo kidogo.

kuhusu Saloon za kike na kiume ni high risk, mana lazima ue na guarantee ya kupata wa east africa wa kukuungia, ila ya kike ni nyepesi zaidi unaweza kupata mashot waki west Africa kiharaka zaidi. ila kwa wanaume sio wepesi kabisa.

Clearing agent haifai kabisa competition ni kubwa sana

Option nyengine ni Gym, hii ni nzuri kidogo mana ni rahisi kuwapata wa west africa na wa Ethiopia. mana sio wengi katika wao wanamiliki biashara hii kwahiyo wengi wao hujiingiza kwenye magym ya wahindi, wa far east na waarabu. kwa hapa unaweza kuwapata.

Ukiweza kupata mchongo wa kupeleka vitu kule ni bora zaidi.

Na kwanini lazima Dubai? Kwanini usianzie Sharjah? kupo alot cheaper utapata kuufahamu mji vizuri ili upande kwenda stape by stape.
Una hoja fulani ambazo ni nzuri
 
Mimi binafsi kama nakamata hiyo hela ningejiripua na Grocery / mini market. Ishu ya uhakika ambayo haina stress, ni kutrack location. nilishawahi kutaka kujaribu Sharjah ila mawe yakawa changamoto. Ila kwa hiyo 200 ningejiripua tu nikaishi kwenye mji wa uhakika nipate kuenjoy life. Huku Bongo kwa kweli shida tupu.
 
Back
Top Bottom