Safi sana, napenda sana mtu mwenye fikra na uthubutu kama huo.
Changamoto kubwa za biashara za dubai kwa sisi ni kuwa mazingira ya dubai ni muhimu sana kupata watu wajamii yako kukuunga kwenye biashara yako, Tatizo kubwa ni kuwa watanzania hatupo wengi dubai, hilo linatufunga kupata fursa nyingi sana mana fursa nyingi kule huzaliwa kupitia uwepo wa watu wa jamii yako. kuna wanageria wana survive dubai kwa kuuza mama ntilie au kupanga mafungu ya vigimbi tu mitaani kinyemela kinachowasaidia ni uwepo wa wanigeria wingi kwenye ule mji kwahio huwa wanaungiana, kuna wadada wa kisomali na wakisudani wanauza samabusa na maandazi tu na maisha yanakwenda kwa sababu ya mazingira hayo hayo.
Biashara ambazo unaweza kutemebea nazo kwa hicho kiwango chako.
Grocery / mini market. - Hii haina bwana, ukipata location tu unapiga, na uzuri wa Dubai location sio isue kubwa mji wenyewe tayari location.
Restaurant. - usifungue direct African restaurant, tafuta wapishi wahindi/ pakistani upike vyakula vyao, huku vyakula vya kiafrica ukianza kuvichomekea kidogo kidogo.
kuhusu Saloon za kike na kiume ni high risk, mana lazima ue na guarantee ya kupata wa east africa wa kukuungia, ila ya kike ni nyepesi zaidi unaweza kupata mashot waki west Africa kiharaka zaidi. ila kwa wanaume sio wepesi kabisa.
Clearing agent haifai kabisa competition ni kubwa sana
Option nyengine ni Gym, hii ni nzuri kidogo mana ni rahisi kuwapata wa west africa na wa Ethiopia. mana sio wengi katika wao wanamiliki biashara hii kwahiyo wengi wao hujiingiza kwenye magym ya wahindi, wa far east na waarabu. kwa hapa unaweza kuwapata.
Ukiweza kupata mchongo wa kupeleka vitu kule ni bora zaidi.
Na kwanini lazima Dubai? Kwanini usianzie Sharjah? kupo alot cheaper utapata kuufahamu mji vizuri ili upande kwenda stape by stape.