Pre GE2025 Kama Upinzani unataka mafaniko ya kweli 2025, Iachane na Urais, Ujikite Serikali za Mitaa, Ubunge na Udiwani, Urais labda 2030!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
P umeandika sana ila juankama kukiwa na KATIBA mpya huru na tume ya uchaguzi huru mbona kila kitu kitaeaka mbelekwa mbela!
 
CCM sio chama cha siasa bali ni kundi la mafisadi wanaowatumia maskini wa kitanzania kuendelea kujinufaisha wao na familia zao. Bahati mbaya hata watu mnaojiita wasomi kama wewe huwezi kuona mbele zaidi ya tumbo lako
 

Ifike mahali hata aibu iendane na umri na reputation uliyotengeneza kwa miaka mingi.

Unamsifia huyo JPM ambaye kwa mwenye akili anajua October 28 ,2020 alirudije madarakani.

Yaani hii CCM ndio unasema iko madarakani kwa sababu ya utashi wa majority.

Kuna kile kimsemo cha Joseph Stalin

It's not the people who vote that count, it's the people who count the votes.


Unapenda kukitumia na ndio CCM na nchi za ushenzi wa kijamaa zinaendelea kukumbatia vyama chakavu vyenye sera chakavu .
 

Update​

"Kama Upinzani unataka mafaniko ya kweli iachane na 2025 lengo liwe 2030"​

Dear Mode, kwanza niwapongeze mode kwa kazi nzuri. Pili bila kuingilia uhuru wako wa kubadili heading yoyote for brevity, lakini huna mamlaka ya kubadili maana, yaani changing meaning!.. Hii heading yako is not what I meant!. Sijasema iachane, nimesema only kwenye presidential I focus on 2030, kwa urais wa 2025 it's too little too late.

Kwa vile Jf ni user generated forum, na pia ni social media, na sio mainstream media, hivyo user tuachwe na uhuru wetu wa kutumia lugha yoyote ikiwemo ruhusa ya kuchanganya lugha!, as long as sio offensive words
Paskali
 
CCM sio chama cha siasa bali ni kundi la mafisadi wanaowatumia maskini wa kitanzania kuendelea kujinufaisha wao na familia zao. Bahati mbaya hata watu mnaojiita wasomi kama wewe huwezi kuona mbele zaidi ya tumbo lako
Mkuu Gulwa , hakuna kitu kizuri kama kuukubali ukweli jinsi ile ulivyo!, uwepo wa kitu ni ile existence in reality, kitu ambacho kipo na kina exist in reality kusema hakipo ni denial.
Mimi sijawahi kujiita msomi!.
P
 
Ushauri wa mlamba asali huyu sio wa kuufuata.
 
Overconfidence....
 
Kuna kosa nimeisha linote, hii ya kudhani 2025 goli liko wazi kwa sababu unadhani kipa ni demu, hivyo ukipiga mashuti makali, badala ya kubana, ataacha na atapanua na nyie kuingiza kiulaini!. 2025 you will be surprised!. Kipa wa 2025 sio demu!.
P
Umetoa Siri au umeamua kuisaidia Cdm ?
 
Ccm ilishazeeka usitarajie irudi ujanani, tutaenda nayo hivyohivyo mwisho itadodoka, usidhani simba huwa anazeeka na nguvu zake, Tz ilivyo haina tofauti na Urusi, china, Korea nk siasa zake ni ngumu sana ila tunasema Mungu yupo ipo siku zitakaa sawa, na wananchi wasichoke kudai chao, Kutwambia tusubiri mpaka 2030 hiyo ni dharau isiyo na mfano.Unadhani ni kwanini wameruhusu mikutano ya Adhara??
 
Naunga mkono hoja.ukiwa na nia lolote linaweza kutokea 2025 ni mbali sana .Mayalla ni muumini wa nature na kawaida ya nature hutokea muda wowote tu.kwahiyo in between hapa kuelekea 2025 chochote kinaweza kutokea nani alijua Magufuli asingemaliza kipindi chake.hata hivyo sio vibaya kuzingatia ushauri wake maana ushauri wa bure haukataliwi.
 
Endelea kulala usingizi mkuu ...tutakuamsha kipindi Cha kampeni 2025 ...
 
Bro! Acha ujinga,acha demokrasia itamalaki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…