Wanabodi,
Mikutano ya siasa imeruhusiwa, Samia atabadili sheria za uchaguzi, ataruhusu hadi wagombea binafsi, atarekebisha Tume ya Uchaguzi kwa kuunda Tume Huru na Shirikishi, ataleta katiba mpya, lakini bado ni CCM ndio itaendelea kushinda na kutawala Tanzania, kwa kipindi kirefu kijacho and probably milele!, kwasababu Tanzania hatuna any serious and credible opposition to checks out CCM!.
Watu wanamatumaini sana na Chadema, lakini amini usiamini, Chadema kwa hivi ilivyo sasa, chini ya Mbowe, bado ni hakuna kitu pale!, labda ibadilike, kule juu iingie mijitu bold kama Lissu, Heche na Lema
Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?
Nimesema hatuna any serious and credible opposition kwasababu upinzani uliopo nchi ni upinzani myopic, una short sightedness, hauoni mbali!, hauna long distance vision ya unataka kufika wapi, hawana good vision ya kuona mbali kuwa wanataka nini kesho, wanakwenda wapi, watumie njia gani na watafikaje, hivyo kukosa a clear vision of its target, na kukosa clear focus hivyo kushindwa ku focus and eventually end up missing the target.
Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ... yaani wapinzani Tanzania ni wanatangatanga tuu!.