Pre GE2025 Kama Upinzani unataka mafaniko ya kweli 2025, Iachane na Urais, Ujikite Serikali za Mitaa, Ubunge na Udiwani, Urais labda 2030!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Naunga mkono hoja na hili mimi pia nilishauri Kama Upinzani unataka mafaniko ya kweli iachane na 2025 lengo liwe 2030
P
 
Sisiem ni weupe katika vichwa vyao, waoga, wazandiki na wezi waliokubuhu. Sasa hivi ndio wanatumia vibaraka wao wale wale kwamba upinzani uachane na urais 2025 na wajielekeze 2030. Ikikaribia 2030 watakuja na uchoro huu huu wa stori zile zile kwamba upinzani waachane na 2030 waelekeze nguvu 2035.
Uchaguzi wa 2025 ndio golden chance kwa upinzani.
Ccm kwa sasa hawana mtu wa kuuzika kwenye urais, kwa mama ni sawa na goli lililobaki bila kipa na wakijaribu kulazimisha wizi ule mwisho wa uvumili wa wananchi kuibiwa utakuwa ndio ukomo.
Nchi haitatawalika msije shangaa Rwanda na Burundi kuja kuwa wasimamizi wa mazungumzo ya kurejesha amani iliyopotea ghafla kwa taifa la Tanzania
 
Mkuu P., nadhani suala la upinzani kuchukua dola ni lini naliona liko mikononi mwa wananchi. Wapinzani wameshafanya kazi yao kwa nafasi yao kwa uwezo wao ni jukumu la Umma kuamua wanachotaka na lini. Hata ikichukua miaka 100 kwa Umma ambao hauna muamko na upinzani, hata aje nani....tutabaki na chama tawala!
 
Haki ya Watanzania haiwezi kuliwa bure miaka 100 kuna siku moja huko huko ccm watu wataanza kuparuana kwa sababu nchi sasa hivi imeanza kutoka kwenye misingi ya sheria inaenda kwa Matakwa ya Watawala.Na sasa undugu umeshaanza kuingia kwenye system pole pole na hapa ndiyo ugonjwa ulipo.Watanzania tuwe wavumilivu siku hao watawala wakidhulumiana tutajua mbivu na mbichi.Pamoja na hila mbalimbali zinazofanywa na viongozi mbalimbali wa ccm kuanzia Mwendazake na waliomfuatia,ukweli utaendelea kuwa ukweli na uongo utabaki kuwa uongo.
Hakuna marefu yasiyo na ncha.Endapo tutaendelea kuishi duniani lazima siku moja tuyashuhudie kwa macho mapinduzi yatakayokuja kutokea kwa hao hao wanaccm.Mungu halali wala hasinzii kamwe.
 
Nasikitika kusoma huu upuuzi wa mtu aliyeonja shule japo kwa shahada moja. Eti opposition waache uchaguzi, wajaribu 2030. What a rubbish advice.

Any registered political party lazima;

1: Ishiriki uchaguzi. Lengo ni kujipima kisiasa dhidi ya vyama vingine. Uungwaji mkono, kuuza sera, itikadi na kukubalika uhalali wa kisiasa (political ligitimacy

2: Uhai wa chama ni chaguzi na kusaka mamlaka ya dola.

3: Kuonyesha hasira za kisiasa watawala hasa chama tawala kuwa kuna mbadala wa mawazo dhidi yao kupitia sanduku la kura no matter umepata kura ngap

4: Kutingisha mfumo wa uongozi. Unapopata kula chache au nyingi unampunguzia margin ya majority votes mshindi na kukupa heshima ya credible opposition results

5: kwa mfumo wa ruzuku, unaposhiriki na score votes unajiakikishia financial support ya ku run chama na uhai wa chama usika na kutengeneza network countrywide.

6: Ni ujinga uliyopitiliza kumuachia chama fulani uchaguz na wew kujibagua labda kama hauna uwezo wa kifedha na kilojikia kufanya hivyo

7: kwa Marekani haitatokea hata cku moja REPUBLICANS wakawaachia DEMOCRATS kwa sabab dhaifu ulizozitoa hata kama kwa mazingira ya nyumbani. Siasa haina mbadala wa kuachiana hiyo mpira wala mke.
 
CHADEMA hawawezi kusubiri 2030 kwa sababu 4:
  • Hoja walizokomaa nazo za DP World zikijikita kwenye ubaguzi wanadhani zitawabeba. Hizo hoja hazitakuwepo 2030.
  • Jinsia ya mgombea wa Urais wa CCM, CHADEMAwanafikiri ni advantage kwao.
  • Mabadiliko ya sheria za uchaguzi, inawapa nguvu na matumaini.
  • Kuruhusiwa kwa maandamano na mikutano ya hadhara, wanadhani ni bao la wazi kwao.
Kwa maoni yangu: Vyama vyote vya upinzani vijikite na kugombea wabunge mpaka 2040. Mwaka 2040 ndio wawe makini kwenye nafasi ya urais.
 
Pascal Mayalla ,2024 bado unaamini hili ? "Samia atabadili sheria za uchaguzi, ataruhusu hadi wagombea binafsi, atarekebisha Tume ya Uchaguzi kwa kuunda Tume Huru na Shirikishi, ataleta katiba mpya"
 
Eliona Kimaro ndiyo nani?
 
Hata huko ni bure tu kwani ccm mbona kote tu wanaiba hata wangesema anatafutwa kiranja wa darasa moja ya shule ya msingi bado ccm wataiba tu.

Tanzania hamna uchaguzi ni kupoteza tu fedha na muda wa watu kwenda kupigwa jua kwenye mafoleni eti mnapiga kura wakati chama fulani kina matokeo ya nchi nzima hata kabla ya huo wanaouita uchaguzi kufanyika. Bure kabisa.
 
Pascal Mayalla ,2024 bado unaamini hili ? "Samia atabadili sheria za uchaguzi, ataruhusu hadi wagombea binafsi, atarekebisha Tume ya Uchaguzi kwa kuunda Tume Huru na Shirikishi, ataleta katiba mpya"
Mkuu kalou , hili bandiko ndio naliona leo!, bado naamini, mwanzo alianza vizuri, sasa anawasikiliza Wahafidhina, ila mwisho atamaliza vizuri na katiba mpya na wagombea binafsi.

P
 
Nakubaliana na wewe boss
 
Hakuna aijuaye kesho
Ni kweli kabisa hakuna ajuaye kesho yake, ila Rais Samia ni mtumishi wetu, sisi ndio tume muajiri kupitia kura zetu na ndio tunao mlipa mshahara wake kupitia kodi zetu, tunawajibu wa kumpangia tunataka nini, akishindwa kutekeleza... tunamfuta kazi!.
P
 
habari JF , kwa sababu kuu tatu;-

1. Ni ngumu sana kuitoa madarakani CCM kwa katiba na Tume hii ya uchaguzi , 2025 ni karibu sana kupata tume au katiba Mpya
Mkuu Nehemia Kilave naunga mkono hoja,nami pia niliwahi kushauri Kuelekea 2025 - Kama Upinzani unataka mafaniko ya kweli 2025, Iachane na Urais, Ujikite Serikali za Mitaa, Ubunge na Udiwani, Urais labda 2030!
3. Tundu Lissu ambae ndiye kwa sasa anaonekana anafaa zaidi bado kuna vitu inabidi ajifunze kabla hajaingia madarakani hivyo 2030 kama ni yeye atakuwa ashaiva.
Naunga mkono hoja ya upinzani kujiandaa na urais 2030 Uchaguzi mkuu wa mwaka 2030, ndio mwanzo wa mwisho wa CCM! Wajinga karibu wote watakuwa wamemalizika!
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…