Scorpio Me
JF-Expert Member
- Aug 2, 2016
- 6,119
- 7,934
Pole sweetheart...u'll get over it...time heals kumbuka...pray and get busy...after sometime u'll be totally okay...Basi karibuni nimeachika. Acheni kabisa. Nilidata karibu two weeks. Kuachwa kunauma hasa kama ulipenda kweli. Yule kaka wa Kicongo aliniweza sana wallah. Alinifanya mpaka niache sehemu niliyokua naipenda aliponipeleka ili tu nisimuone.
Nimepona kidogo, sijui nikikutana nae tena nitajisikiaje.
Pole sweetheart...u'll get over it...time heals kumbuka...pray and get busy...after sometime u'll be totally okay...
Usimwamini binadamu yoyote chini ya jua, umwambie ukweli au uongo, be careful with ur heartNilicho jifunza toka kwa kiumbe mwanamke....kwanza haridhiki,pili hajui anacho kitaka,tatu kigeugeu....lakini anatakiwa kudanganywa zaidi kuliko kumwambia ukweli.
Sent using Jamii Forums mobile app
Pole Sana wa congo hawaaminiki kabisa, na marafiki wacongo nikienda saloon huwa naweka boundaries kaliBasi karibuni nimeachika. Acheni kabisa. Nilidata karibu two weeks. Kuachwa kunauma hasa kama ulipenda kweli. Yule kaka wa Kicongo aliniweza sana wallah. Alinifanya mpaka niache sehemu niliyokua naipenda aliponipeleka ili tu nisimuone.
Nimepona kidogo, sijui nikikutana nae tena nitajisikiaje.
Pole Sana wa congo hawaaminiki kabisa, na marafiki wacongo nikienda saloon huwa naweka boundaries kali
Shida ya wacongo wanajua kubembeleza na udhaifu wetu wanawake kubembelezwa na kudekeza, Sasa ukinogewa tu wafwa. Usipende kumkabidhi moyo mtu mapema kabla hujajua misimamo yake ili usije umia. Mimi napenda kulinda moyo wangu aisee kupenda no nakuweka kiunoni ukizingua nakutingisha tupa kuleAsante mpenzi. Sasa mie niliingia kichwa kichwa. Ila mpaka sasa naona nimepata nafuu. Week 3 za mwanzo zilikua ngumu sana.
Shida ya wacongo wanajua kubembeleza na udhaifu wetu wanawake kubembelezwa na kudekeza, Sasa ukinogewa tu wafwa. Usipende kumkabidhi moyo mtu mapema kabla hujajua misimamo yake ili usije umia. Mimi napenda kulinda moyo wangu aisee kupenda no nakuweka kiunoni ukizingua nakutingisha tupa kule
Pole Sana huyo alikuwa tu mpitaji aisee, na watu wa hivo ukigusa tu attachment unayo I feel sio ya nchi hii.Wanabembeleza, wanajali. Yani alinifanya nisahau kila kitu. Alinionyesha mapenzi sijayapata karibu miaka miwili. Alijua kuwin moyo wangu na mimi ni wale watu nikipenda nimependa na sichukui round.
Sasa mwenzie nishakwama kosa la kijinga sana nikanuna akaniacha.
😃😃😃 Wewe cariha pimbi kweliShida ya wacongo wanajua kubembeleza na udhaifu wetu wanawake kubembelezwa na kudekeza, Sasa ukinogewa tu wafwa. Usipende kumkabidhi moyo mtu mapema kabla hujajua misimamo yake ili usije umia. Mimi napenda kulinda moyo wangu aisee kupenda no nakuweka kiunoni ukizingua nakutingisha tupa kule
😂😂Kuna mwanamke aliwahi kuniandikia message ya hivyo aisee! Ile nimemaliza kuisoma tu, nikavuta pumzi ndefu nikatulia.
Nikampigia simu, nikamuuliza hii message ni ya kwangu au imekosewa kutumwa? Akajibu ni ya kwako. Nikakata na simu bila kuongeza neno. Sikupenda kubembeleza maamuzi yake wala kudadisi.
Baada ya siku nne, nilishangaa kuona sms nyingi za kuomba msamaha, sikujibu hata moja. Alipiga simu kibao na sikupokea kabisa. Nilimfowadia ile sms ya kuachana nikaongeza na sms moja tu " Nimeshapata mwingine ".
Alipokuja kuonana nami, nilimwambia 'usivunje mapenzi na mtu wako kwa ahadi za bwana mpya'. Wengine hatuumii kwa kuachwa bali tunasikitika tena kidogo tu.
Japokuwa tulikuwa tunakulana ila penzi halikunoga tena. Maana sikumuamini tena hata 20%
Sent using Jamii Forums mobile app
Naaamdaah nimesoma comments zenu, wanangu mnaachwa kikatili sna... Ila msikate tamaa Wanangu point ya msingi Wee TAFUTA HELA, narudia TAFUTA HELA Wanawake wapoo
Sent using Jamii Forums mobile app
Relax broJF ya sasa inakera kama nini, unascrol page moja tu comments zingine hazionekani. Kama mnataka kuifunga si muifunge tu tujue imeisha
Vp mzigo ulikula?Nakumbuka mi nliachwa July 2019 kwa Phone call. Kwa kweli nilimpenda sana yule binti na kwa muda mfupi nlokua naye alinichuna lakini mi nlichukulia poa kwa sababu nlimpenda saaaaaana
Baada ya kumpiga sound, Nilimsafirisha toka Dar kuja Arusha, bata mbili tatu na baadae nkamrudisha Dar huko huko kuna hela kanikopa ila hata nguvu ya kumdai sina [emoji18]
Akaanza kutopokea simu zangu, hajibu text, ndo ikawa nimepewa silent treatment iyooo na baadae breakup phone call
Aiseeeee nilivyokua na mipango naye nkaona kama ndoto zangu zooote zimezimika ghafla, nikaugua Insomnia, depression na anxiety juuu!
Mpaka sasa hivi bado naendelea ku-recover ila daaaaaa kuna wanawake wanajua kutu-take for granted
One day Yes!!!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo imeishaImetoka hii.View attachment 1469248
Tupe kisa cha hii issue mzee kakufanya nnImetoka hii.View attachment 1469248
... akanifata na kunishikisha laki moja...Mimi Kuna manzi mmoja aliniacha kimasihara Sana. Yaani siku iyo alinipigia simu nikamwelekeza nilipokuwa nagonga mtungi. Akaja na jamaa ambaye kwangu alikuwa NI mkubwa kidogo.
Basi wakajoin. Jamaa akawa anasimamia bill zote pale. Mwisho wa siku manzi akaniambia - ujue kawoli hii ndio itakuwa mwisho wa Mimi na wewe kunywa pamoja Kama hivi. Huyu hapa NI Mr T ndio mpenzi wangu mpya nimeona Bora nikutambulishe ili tuachane kwa amani.
Nikaumuuliza tu yule manzi kama Kuna tatizo lolote labda, akajibu Hakuna. Nikamuuliza na Mr T Kama anampenda jwa dhati yule manzi, akajibu Sanaa.
Nikamwambia manzi awe na amani ila Mimi nitakaa Kama miezi sita hivi ndio nitaangalia uwezekano wa kuwa na mahusiano mengine. Ikawa tumeishia hivyo.
Walivokuwa wanaingia kwenye ndinga ya jamaa ili wasepe nikafanya ukauzu kidogo, nikawauliza Sasa mnaniachaje achaje hapa maana ndio kwanza kunaanza kuchangamka.
Basi Mr T kwa mbwembwe akanifata na kunishikisha lakimoja na akaniambia, I have never meet such a nigga in my entire life. Nikamwambia be blessed coz u are lucky to meet me today.
Wakasepa. Ile laki nikaichana yote pale pale na wahuhudumu wa bar. Nikawa Mimi ndio doni.
Nikaja kuonana nae after couple of years akiwa tayari ameshaolewa lkn na mwanaume nwingine sio Mr T, na mm nikiwa kwenye pilika pilika za kuoa. Sikutaka hata kuuliza waliishia wapi kwenye mahusiano yao. Akanichangia elfu70. Maisha yakasonga.