holy holm
JF-Expert Member
- May 6, 2017
- 4,793
- 9,101
Habari za wakati huu wakubwa.
Jamani nimenasa kwenye penzi na Mmama mmoja mtu mzima.Japo siyo mara yangu ya kwanza ku date na hawa viumbe wakubwa , lakini kwa huyu daah.
Jinsi nilivyokutana naye
Mimi ni Fundi Rangi, gypsum board na skiming. Kama mnavyojua hizi kazi zetu siyo za kila siku, kuna wakati tenda ni nyingi na kuna wakati tunapigika mtaani siyo poa.
Mwaka jana mweza wa kumi na 11 ilikua ni miezi migumu kwangu, kazi hamna yaani ni kupewa tu ahadi na maboss lakin kazi hamna , labda siku moja moja upewe day na mafundi wenzako.
Tuachane na hayo , kuna siku moja nimekaa home mfukoni nimebaki na tsh 6000 tu na sijui nitaishi vipi kwa wiki nzima na hiyo hela. Basi kama utani hivi nilipigiwa simu na fundi mwenzangu mmoja, akanambia kuwa kuna kazi ya kupiga msasa nyumba ya tajiri balaah..
Basi nilikubali pale haraka, akaniunganisha na msimamizi wa hyo nyumba, tukaelewana bei. Baada ya kubageini bei tukakubaliana anilipe 250k, nyumba ilikua ina vyumba 6.
Nilitafuta vijana wangu wa kazi watatu ili ni wape day, basi bwana kesho yake siku ya ijumaa hao tukawahi kazini, sehem moja hivi panaitwa Bukanga (watu wa Musoma wanapajua ). Ile tunafika sehem waliyo tuelekeza niliishiwa pozi kabisa. yaani yule msimamizi alikua fala sana , eti tunafika anatuomba samahani eti boss wake kashapata wapiga msasa kutoka SIDO , fikiria kama ndiyo wewe upate huo usumbufu na ukizingatia kwenye ile buku sita yangu nilitoa buku tatu kwa ajili ya nauli yangu na vijana wangu.
Sikuona hata haja ya kubishana naye ingawa wale vijana wangu walitaka kumletea noma nikawazuia.
Tukiwa bado eneo la tukio bado tunashauriana tufanyeje , tuliamua kupumzika nje ya hiyo nyumba na hasira zetu. Hapo hapo jirani kulikua kuna msiba tulikua tunasubiria muda wa msosi twende tukamlie marehemu ubwabwa halafu tusepe zetu.
Kuna mzee mmoja alikuja pale tulipokua akatusalimia akatuuliza kama sisi ni mafundi, nikasema ndiyo basi akaniomba twende chemba tuongee.
Mungu siyo Asumani, mzee alinambia kuwa kuna kazi. Kulikua kuna nyumba ya mchungaji wa kanisa la kilokole ilitakiwa ipigwe brandaling, iwekwe body na iskimiwe pamoja na rangi kabisa tukabadilishana namba basi tukawa tumeachana akiahidi kunipa majibu.
Tuliondoka na vijana wangu kurudi kila mtu sehemu yake , na tulitembea siku hyo asee kilomita za kutosha 😂😂.
Basi jumatatu asubuhi saa moja moja hivi yule mzee alinipigia simu akanielekeza niende kanisani kwao kuona hiyo nyumba pia nipige na hesabu kabisa. Nilifika eneo la kazi nikapiga hesabu ya material na ufundi kabisa , ikumbukwe kwenye simu yule Mzee alinipanga kuwa pesa ya ufundi nimpe % kadhaa, maana yeye ndiyo kanipa tenda, siku mbishia maana aliniokoa sana na njaa.
Baada ya yote hayo kuisha niliambiwa kazi nianze siku inayofata kwani material tulienda kununua mimi pamoja na yule mzee akiwepo na muhazini wa kanisa. Yote kwa yote yule mzee ni noma , alipiga gaa za kutosha, uzuri waligawana wote yeye na muhazini.
Kwa vile kazi ilikua kubwa nilitafuta mafundi wengine pamoja na wale vijana wangu kazi ikaanza. Nili plan ndani ya wiki moja na nusu nikabidhi Kazi.
Sasa siku moja wakati tunafunga body sebuleni, kuna wamama wawili ni washiriki wa hilo kanisa , wakuja kuona jinsii kazi inavyoenda, walivutiwa sana na kazi wakawa wanatoa sifa kwetu kwa kazi nzuri. Mmoja wa wale kina Mama aliulizia fundi mkuu ni nani, basi nikaenda kumsikiliza. Tulitoka naye njee maana ndani kelele. Alinambia ana nyumba yake na yeye inatakiwa ifungwe body ila kwa awamu, nilisema sawa akanipa no yake basi wakawa wamesepa.
Niliona hiyo ni fursa imekuja kwahyo lazima nicheze nayo mapema, siku hiyo hiyo usiku nikiwa home mida ya saa tatu , nilimpigia yule Mama , ilipo pokea simu alinambia atanitafuta baadae maana alikuwa kwenye ibada.
Kwenye saa nne alinipigia nikajitambulisha kwake kuwa me ni fundi wa nyumba ya mchungaji, basi tukaongea kuhusu kazi akanambia siku ya kesho yake atanielekeza kwake nikaone hiyo kazi.
Kesho yake niliwapa maelekezo mafundi wenzangu halafu mimi nikaenda nyumbani kwa yule Mama kuona hiyo kazi, nilifika nikapiga hesabu za mbao na body na hela ya ufundi basi akanipa ahadi ya kuanza kazi next week.
Kwa wakati huo hata nilikua simtafuti kwenye simu hata yeye pia maana hatukuwa na mazoea kihivyo.
Zilipita kama wiki mbili yaani hata ile kazi ya kanisa tulikuwa tushamaliza, ndo akanichek kwenye simu , alitaka kesho yake niende kwake nianze kazi.
Nitarudi baade kumaliza sehemu ya mwisho.