Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,455
- 73,145
Hakuna aliyetegemea hali iliyopo Nairobi ingekuwa hivi ilivyo sasa. Nairobi imechafuka na askari wameanza kuonyesha kuchoka mapema kabisa na maandamano yanazidi kushika kasi.
Rais Ruto atashuhudia kama utani akiondoka madarakani maana nguvu ya umma haiwezi kuzuiwa na polisi hata kidogo.
Kama ilivyokuwa mataifa ya kiarabu miaka michache iliyopita ambako vurugu na maandamano yaliambukizana kutoka nchi moja kwenda nyingine, jee hali hiyo yaweza kuambukizwa hapa Afrika mashariki?
Kwamba twaweza kuja sikia Uganda yakotokea au Tanzania (Tanganyika) nako yakifumka? Maana sababu kubwa ni hali ngumu ya maisha na tuhuma za uchaguzi usio haki ambao kwa EAC ni kama gonjwa sugu.
Viongozi wayaangalie matatizo kwa jicho la tatu badala ya kuwaambia watu waende Burundi au wabunge wao wakajadili uganga wa kienyeji maana uchumi sio professional yao.
Mungu ibariki EAC isiingie kwenye machafuko na viongozi walio shindwa kutekeleza majukumu wajitambue na kung'atuka.