Kama viongozi wa CCM na Mwenyekiti wao hawawezi kuisikiliza sauti ya Demokrasia ya WanaCCM wenzao unadhani watamsikiliza nani?

JET SALLI

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2014
Posts
2,392
Reaction score
1,578
Mtu anayeamini kuwa CCM bado ni chama halisi anajidanganya. Kwa sasa, ni genge la watu wanaoendekeza udhalimu, kusifia na kutetea uovu. Chama kimeshikiliwa na watu wanaotenda uovu bila kujali mateso ya wengine; hawataki kusikia sauti za watu wema waliopo ndani ya CCM.

Leo hii, Mr. Nchimbi anadai kuwa wamekaa na mwenyekiti na kukubaliana kuwa walioenguliwa kwa makosa madogo madogo warejeshwe. Hii ni hoja isiyo na mantiki, kana kwamba watu wengine wote hawajui kusoma na kuandika isipokuwa wao pekee. Hii ni dharau kubwa, kana kwamba wamewapeleka darasani ghafla kujifunza kusoma na kuandika.

Aidha, mnaagiza wakurugenzi nchi nzima wajaze majina ya wapiga kura, ikiwemo ya marehemu, na kuondoa wagombea wa upinzani kwa mbinu zilezile za enzi za Magufuli. Kisha mnajitokeza hadharani na kusema mnawarudisha, mkitarajia kuonekana wa maana sana. Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu ambaye hajabaini ujinga mnaoufanya.

Uchaguzi huu umejaa uchafu wa kutisha na unahitaji kuanzishwa upya kwa kuwa mchakato mzima umejaa dosari. MUNGU ameyaona yote haya, na CCM inapaswa kukumbuka kuwa watu wakimlilia MUNGU, atajibu. Bado kuna muda wa kurekebisha na kuondoa usanii wote uliokithiri katika maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
 
CCM wametengeneza tatizo halafu wanajifanya kulitatua, wanatuona Watanzania ni wajinga.

Vv

..exactly!

..Wizara ya Tamisemi iko ndani ya Ofisi ya Raisi.

..Kikatiba Raisi ndiye Waziri Kamili wa Tamisemi.
 
CCM kwa sasa inafanya mambo ya kutisha hata shetani mwenyewe hakuwahi kufanya!
 
Kwa yanayoendelea nakubaliana nawale wanaosema miafrika ata kujiongoza wenyewe hatuwezi.Mambo yakijinga kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…