G Jonathan Kamenge
Member
- Apr 8, 2023
- 30
- 23
Mzee Butiku anasema IGP, Mkuu wa Usalama wa Taifa, na hata CDF "wasitwambie hawajui". Lakini huenda hawajui! Ingawa kama ni kweli kwamba hawajui, maana yake ni kwamba hali ya Usalama wa taifa letu ni mbaya kuliko wakati wowote ule katika historia yetu walau kwa kipindi cha miaka ishirini iliyopita!
Ndiyo, kwa sababu Watanzania kwa sehemu kubwa sisi ni waheshimu sheria (ingawa wahalifu hawakosekani kwenye jamii yoyote), na hili limechangiwa kwa miaka mingi na mambo matatu makubwa walau kwa maoni yangu. Kwanza "nidhamu" na uzalendo wa watu kwa taifa letu. Baby boomers na Millennials (tulioimba Alama za Chama cha Mapinduzi, na Iddy Amin akifa), tulijengwa kuweka mipaka tunapokosoa mambo na hata tulikuwa na msemo "Mkubwa hakosei" ingawa kusema kweli wakubwa wengi hukosa na kosa la mkubwa ni kubwa na madhara yake ni makubwa na ya muda mrefu kwa watu wengi.
Ni msingi huu wa uheshimu sheria uliofanya mpaka kukaanza kuwako kwa Polisi bandia wakikamatwa mitaani, ama maafisa wa Trafiki bandia wakisimamisha magari barabarani. Hatukujua wakati huo kwamba hiyo ilikuwa dalili ya kansa mbaya sana kwamba kwa wananchi kutojua haki zao za kisheria, na uoga wa kuzidai na hata Polisi wenyewe kuzivunja (mara nyingine kwa vipigo na fujo ukimhoji Polisi anapokiuka sheria kwenye kutekeleza majukumu yake), tulikuwa tunatoa fursa ya watu kuamini kwamba ikiwa mtu yeyote atakuja kwenye jamii akijitambulisha na taasisi yoyote ya dola, basi anaweza kufanya lolote bila kuhojiwa chochote na yeyote, na matokeo yake ndiyo haya!!!
Kama Polisi na vyombo vingine vya dola vingekuwa vinazingatia sheria na kanuni katika ukamataji na usimamizi mzima wa mfumo wa haki jinai, kungekuwa na tofauti kati ya wahuni na watendaji wa vyombo, na hilo lingefanya tuweze kuhoji inapotokea tofauti; lakini sasa ni holela, mradi kila mtu anafahamu "codes" kadha tu za wanausalama, basi anafanya lolote, vyovyote na wananchi hawawezi kuhoji chochote. Najiuliza, watu zaidi ya sabini, walishindwa vipi kumtaka dereva kupeleka gari hadi kituo cha Polisi, ndipo hao "watu" wamshushe mtuhumiwa wao?
Au nao waliogopa kubambikiwa kesi ya "kuingilia utendaji wa mamlaka" na kurundikwa ndani bila due process kwa vile sasa hiyo ni kawaida ya vyombo vyetu!!? Wakati mtu anapopigwa akiwa kafungwa pingu na hata mara nyingine kuuawa kama mnyama tu tena akiwa kwenye gari ya Polisi (kama ilivyotokea kwa kijana Heche) na bado hakuna hatua za wazi zinazochukuliwa dhidi ya msimamizi wa Operesheni ile na askari wake na bado tunawataka raia kushirikiana na wanausalama, ni dalili mbaya siyo tu kwa afya ya mahusiano ya pande mbili hizi, bali ya uwapo wa kansa mbaya inayotafuna jamii na 'organs' zake.
Wakati tulipoanza kuona na kusikia watu wakijitambulisha kama "Usalama wa taifa" mitaani na kuwatapeli, tukaona ni kawaida na miaka kadha hapo nyuma tukianzisha hizi "task forces" zisizofungwa na sheria yoyote, na mwisho hivi karibuni tukafanya marekebisho ya sheria kuruhusu "Usalama wa Taifa" kufanya ukamataji (jukumu ambalo lilikuwa la Polisi pekee kisheria) na hata kuondoa kanuni kadhaa za ukamataji, sasa mtu anashushwa kwenye gari, na kesho anakutwa amekufa na kutupwa kama mzoga wa Mbwa, na hivyo tunazipa uhalali taarifa kwamba watu wamekuwa wakichukuliwa majumbani mwao, makazini mwao, barabarani na kupotea jumla; hakuna aliye salama!!
Kama baada ya matendo ya namna hivi bado tunasubiri "taarifa za uchunguzi" ambao nao unafanywa na watu kutoka kwenye taasisi ambazo nazo hazina namna ya kujitofautisha na wahuni wanaoteka watu na kuwaua ama kuwapoteza, maana yake ni kwamba tuna watendaji wa vyombo wasiozingatia sheria kwenye kutumia mamlaka yao, na tuna magenge ya kigaidi yanayoweza kubeba silaha na kuteka watu mitaani na wote wana mfumo mmoja tu (mabavu bila kuzingatia sheria na kuheshimu utu wa watu) na bado Wakuu wa vyombo hawajui, nao wanasubiri taarifa za uchunguzi ili wampelekee Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ndipo naye ajue namna ya kulinda usalama wetu na maisha yetu. In the meantime, we are all animals to be porched by predators wakati wowote wakijisikia. Ndipo hapo ninapojiuliza, kwani wasiojulikana watajulikanaje kama wote hatujui wanaojulikana wanapaswa kutenda kwa jinsi gani!!?
Nasema tena, sijui lolote Nanga miye, nawaza tu kibanangabananga wala msinijali, na please msiniteke ama "kunichukua" maana hata mimi sijui nasema nini! Simo!
- Hali ya Mifumo ya Haki Jinai na Haki za Binamu nchini; Je, Mamlaka zinatekeleza Mapendekezo ya Tume ya Rais ya Haki Jinai?