Kama Wachezaji wa Simba wataendelea kucheza 'Show Game', kwenye Makundi nje na kwenye ligi hawapati kitu

Tatizo ni kocha timu ipo slow na wanasubiri tukose ligu kuu ndio watimuane
 
Teh teh teh teh teh ila Simba bhana sijui maneno ya Manara yanawalevya? Ukiangalia usajili wao.......
.
Mkuu ni kama vile maneno ya Obama kwa putin, simba ni kama vile mtoto alienda shuleni alafu akaingia darasani, kisha akakaa nyuma ya ubao, hajui kilichompeleka!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Timu ata haieleweki inacheza mfumo gani.wachezaji nikuruka ruka tu uwanjani kama wanacheza mdumange.Kocha naye uwezo umekwisha kabakia kushika tu mzuzu.Soka letu bado sana,kelele za mdomo nyingi kuliko vitendo.
 
Hata kwa as vita walijkfanya kucheza kupasiana pasiana pasi zisizo na tija. Kilichotokea kila mtu anajua. Natabiri mabaya zaidi ya ya kongo kutokea huko misri.
 
Hata angepewa timu mwaka juzi ubingwa tungekosa hajiwezi na hajui mbinu mbadala hususani soka la africa hela za mo zinateketea
Cha kusikitisha Mo hilo halijui au wapambe waliomleta wanaendelea kumdanganya kuwa awe na subira.

Tungekuwa tupo kwenye mashindano ya FA, au tumechukua kombe la Mapinduzi angalau ningemwelewa kidogo lakini huko kote amefeli, hili la Sport Pesa amefeli halafu ana matumaini na ubingwa wa Africa, he must be insane.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasema hii michuano ya ndani ikiwemo sport pesa sio kipaumbele chao wao wanataka ubingwa wa Africa
 
Kocha wa Nkana na Vita walishamfundisha kocha wa Simba cha Kufanya.
Lakini nadhani hazingatii ushauri wa makocha wenzake.
-Kasi Zero
-Bidii Zero
-Umakini golini Zero
- Pasipasi 100%
Kamati ya Uwekezaji ni lazima mkae chini mtathmini hali ya timu.
Haina maana ya kuwekeza wakati hata kikombe cha Mbuzi timu inashindwa kupata.
Ona hao washambuliaji waliofanya Majaribiao, hata kuzima mpira hawawezi.
Ni nani kawaleta ?
Muwasajiri basi tuone vituko.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…