Kama Wachezaji wa Simba wataendelea kucheza 'Show Game', kwenye Makundi nje na kwenye ligi hawapati kitu

Kama Wachezaji wa Simba wataendelea kucheza 'Show Game', kwenye Makundi nje na kwenye ligi hawapati kitu

tatizo sio Kocha haya mashindano yameingiliana na mashindano mengine makubwa kocha lazima achezeshe timu kwa tahadhari ya kutopata majeruhi, kuwafanya wasichoke sana na pia kuangalia viwango vya wachezaji anaotaka kuwasajili ila kuna wachezaji wengine hata wapewe nafasi kiasi gani bado mazoba
Dhana ya kuwa na kikosi kìpana ni nini? Sì mlituaminïsha kuwa simba ina kiķosí kipana imekuwaje tena?
 
Dhana ya kuwa na kikosi kìpana ni nini? Sì mlituaminïsha kuwa simba ina kiķosí kipana imekuwaje tena?
Wanasema eti mashindano yameingiliana wakati hata huko ulaya timu zinacheza vikombe vingi na bado wanafanya vizuri hapa ni kwamba timu ina mapungufu mengi hawataki kukiri hili.
 
Simba ni mbovu.
Na haitapata hata kikombe cha Mbuzi msimu huu.
Tatizo ni kocha.
Hataki hata msaidizi
Hana mbinu ya ushindi
Huu ukweli wengine hawautaki.


Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu kipaumbele chake kwenye ubingwa wa Afrika kwa gharama ya kupoteza vikombe vingine vyote huwa nashindwa kunwelewa, hata ligi kuu kwake sio muhimu kama klabu bingwa Afrika, huyu kocha kuna watu wamepiga hela za Mo bila huruma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni kocha timu ipo slow na wanasubiri tukose ligu kuu ndio watimuane
Tatizo siyo kocha. Tatizo siyo wachezaji. Tatizo ni anayetafuta kocha, na anayesajili wachezaji. Ungetarajia timu kuingia kwenye mfumo mpya ingebadili aina ya uendeshaji. Lakini wapi! Wapiga dili walewale ndio wamebaki kuongoza klabu. Kilichoongezeka ni pesa na mwenye pesa. Utegemee nini paka anapofungwa na kitoweo, kama si kukitowea mpaka akavimbiwa? Huwezi kushinda Kombe la Afrika kwa wachezaji/timu inayopata taabu kuifunga Yanga yenye matatizo lukuki, au Mbao yenye usajili wa kuungaunga, au timu ambazo ubora wake ni vinywa vya wasemaji wao.
Mpaka hapo wababaishaji watakapokuwa bidhaa adimu ndani ya Simba, tusitarajie mabadiliko ya maana. Na ndivyo ilivyo kwa soka lote la Tanzania.
 
tatizo sio Kocha haya mashindano yameingiliana na mashindano mengine makubwa kocha lazima achezeshe timu kwa tahadhari ya kutopata majeruhi, kuwafanya wasichoke sana na pia kuangalia viwango vya wachezaji anaotaka kuwasajili ila kuna wachezaji wengine hata wapewe nafasi kiasi gani bado mazoba
Hapo ndipo unapoona ubabaishaji wa soka letu. Emirates wanadhamini timu kubwa kubwa kadhaa barani Ulaya. Umewaona wakiziingiza kwenye mashindano ya wao kwa wao ndani ya msimu wa Ligi? Sportspesa ndio nani kuvuruga Ligi yetu kwa sababu tu ndio wadhamini wa timu zetu? Mbona hawaiingilii Everton ili icheze na huyo mshindi wa hili Bonanza katikati ya msimu wa EPL? Simba, yenye uwezo wa kifedha, imeshindiwa nini kuwaambia Sportspesa kwamba hawako tayari kuchezeshwa bonanza wakati huu wakiwa kwenye hatua muhimu ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hata kama ni kwa kuvunja mkataba na hao Sportspesa? TFF inashindwaje kukataa kupangua ratiba ya Ligi Kuu kwa ajili ya bonanza hilo? Wote ni kwa sababu ya tamaa ya vijisenti, iwe ni mapato ya milangoni au ujanja wa kwenye viingilio. Lakini na Kocha naye kama ameona Mashindano ya Sportspesa ni kikwazo kwa malengo yake mapana, alishindiwa nini kuweka msimamo wake mapema mpaka alalamike baada ya kipigo cha Bandari, kama si ubabaishaji? Kombe peke la kimataifa tunaloweza kujiamini kuwa tutalichukua ni la ubabaishaji!
 
Hivi mnategemea mtu kama Zimbwe au Kichuya anyumbulike kiufundi aamue matokeo hahaha mnachekesha sana,
Mimi toka zamani huwa naona Tanzania ina wachezaji wavivu wavivu wasiojitambua.
 
Wachezaji wanao cheza Tanzania wavivu
Ndio hili linachangiwa sana na aina ya mazoezi wanayopewa na Makocha wao.
Kocha Zahera ameonesha utofauti kidogo kwa kufundisha mpira wa kasi.
Na hata tuzo zake za kocha bora zinatokana na uwezo wake wa kuibadilisha timu na kucheza mpira wa kuleta matokeo chanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom