Kama Wachezaji wa Simba wataendelea kucheza 'Show Game', kwenye Makundi nje na kwenye ligi hawapati kitu

Hapo ndipo unapoona ubabaishaji wa soka letu. Emirates wanadhamini timu kubwa kubwa kadhaa barani Ulaya. Umewaona wakiziingiza kwenye mashindano ya wao kwa wao ndani ya msimu wa Ligi? Sportspesa ndio nani kuvuruga Ligi yetu kwa sababu tu ndio wadhamini wa timu zetu? Mbona hawaiingilii Everton ili icheze na huyo mshindi wa hili Bonanza katikati ya msimu wa EPL? Simba, yenye uwezo wa kifedha, imeshindiwa nini kuwaambia Sportspesa kwamba hawako tayari kuchezeshwa bonanza wakati huu wakiwa kwenye hatua muhimu ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hata kama ni kwa kuvunja mkataba na hao Sportspesa? TFF inashindwaje kukataa kupangua ratiba ya Ligi Kuu kwa ajili ya bonanza hilo? Wote ni kwa sababu ya tamaa ya vijisenti, iwe ni mapato ya milangoni au ujanja wa kwenye viingilio. Lakini na Kocha naye kama ameona Mashindano ya Sportspesa ni kikwazo kwa malengo yake mapana, alishindiwa nini kuweka msimamo wake mapema mpaka alalamike baada ya kipigo cha Bandari, kama si ubabaishaji? Kombe peke la kimataifa tunaloweza kujiamini kuwa tutalichukua ni la ubabaishaji!
kama kuna mashindano ya Emirates lakini wao wanayafanya kabla kipindi cha ligi hakijaanza sisi ndio tunashindwa kupanga ratiba mapinduzi cup hayana umuhimu zaidi ya siasa hii sportpesa walitakiwa waandae kabla msimu wa ligi haujaanza
 
Tofauti ya Mapinduzi Cup na Sportpesa ni kuwa Mapinduzi Cup TFF inajipangia yenyewe wakati Sportpesa wanashinikizwa na mdhamini - siyo wa Ligi - bali wa baadhi ya timu za Ligi.
 
Hapo ndipo unapoona ubabaishaji wa soka letu. Emirates wanadhamini timu kubwa kubwa kadhaa barani Ulaya. Umewaona wakiziingiza kwenye mashindano ya wao kwa wao ndani ya msimu wa Ligi? Sportspesa ndio nani kuvuruga Ligi yetu kwa sababu tu ndio wadhamini wa timu zetu? Mbona hawaiingilii Everton ili icheze na huyo mshindi wa hili Bonanza katikati ya msimu wa EPL? Simba, yenye uwezo wa kifedha, imeshindiwa nini kuwaambia Sportspesa kwamba hawako tayari kuchezeshwa bonanza wakati huu wakiwa kwenye hatua muhimu ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hata kama ni kwa kuvunja mkataba na hao Sportspesa? TFF inashindwaje kukataa kupangua ratiba ya Ligi Kuu kwa ajili ya bonanza hilo? Wote ni kwa sababu ya tamaa ya vijisenti, iwe ni mapato ya milangoni au ujanja wa kwenye viingilio. Lakini na Kocha naye kama ameona Mashindano ya Sportspesa ni kikwazo kwa malengo yake mapana, alishindiwa nini kuweka msimamo wake mapema mpaka alalamike baada ya kipigo cha Bandari, kama si ubabaishaji? Kombe peke la kimataifa tunaloweza kujiamini kuwa tutalichukua ni la ubabaishaji!
we mwenyewe ni bingwa wa hoja za kubabaisha!!

unauliza Sportpesa ni nani zama hizi,kwamba hujui mpira wahitaji pesa???
 
Hakuna jambo gumu kama kumfahamisha asiyeifahamu lugha yake mwenyewe. Kwa Kiswahili unaposema ‘fulani ni nani hadi a.......’ si kwamba humfahamu. Ila unahoji uzito wa anachokifanya au nafasi/fursa anayopewa ukilinganishwa na mchango wake katika muktadha mzima wa jambo husika. Hebu basi soma tena maoni yangu kwa kutumia tafsiri hiyo.
 
Umerudi palepale tu,,unahoji 'uzito' wa anachokifanya:kwamba hujui mpira wahitaji pesa??

swali langu limebaki palepale!
 
Wise people speak because they have something to say, fools speak because they have to say something.
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂

kumbe 'kidhungu' unakijua,

sasa mbona umejiita jina la kienyeji??

😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Ukweli ni kwamba wachezaji wa simba wanatudhalilisha sana sisi mashabiki wao.

Wanafungwa na vitimu vya vichochoroni ambavyo bajeti yake kwa mwaka haifiki hata mshahara wa Niyonzima wa mwaka mmoja hii ni dharau kama siyo kutokujitambua kwa wachezaji.

Wanacheza bila malengo na kujipigia pigia vichenga uchwara badala ya kucheza kutafuta matokeo au nani kawambia sisi tunakuja kuangalia vyenga vyao tu ?

Wao ndiyo wanalipwa vizuri kuliko team nyingine hapa bongo na east afrika badala ya kuhamasika na kucheza mpira kwa kiwango kikubwa wao wanaota vitambi !!!!

Kila siku tunajitoa uwanjani kuja kushangilia tunakuja kuvuna aibu tena kwa vitimu vya machakani tu kama bandari, green warriors na mashujaa are you serious ?
Nimekata tamaa ni wachezaji wa klabu ya Simba kutoka na aina ya uchezaji wao wa kutaka kushangiliwa "Show game".

Wachezaji hawajui kuwa kila dakika timu inataka goli wanatumia muda mwingi kupiga chenga zisizo na tija kwa timu.Wachezaji hawapigi mashuti wanapiga chenga na kupoteza mipira.

Kwa walioona mechi ya leo kati ya Simba na Bandari , Wachezaji wa Bandari walikuwa nyuma lakini wamecheza kwa malengo na kusawazisha goli na kuongeza bao la ushindi.

Naamini ingekuwa Bandari ndio imeanza kufunga kwa wachezaji wa Simba wasingeweza kusawazisha lile goli kwa wanapenda kucheza "Show game".Hitimisho kwa uchezaji huu Simba itatolewa Mechi za Makundi na Ligi kuu ya Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom