Kama wasanii wetu wote wakipimwa HIV

Mwanapropaganda

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Posts
4,235
Reaction score
2,508
Habari nyingi kuhusu wasanii(nawaita wasanii japo sio wasanii) wetu wa filamu na muziki ni kuhusu ngono tu! hakuna misuguano ya kikazi au uboreshaji wa kazi zao bali ni tuhuma tu za kunyang'anyana wanaume/wanawake huku wakijiona ni wajanja kubadili wapenzi kama nguo.

Kuna wengine imefikia hatua ya kukiri kuwa na mahusiano na waume za watu na kuzaa nao huku wakiwa na familia zao.

Ukitazama vizuri utaona kuwa msanii mmoja wa kike anakuwa na wanaume zaidi ya watano na huku kila mwanaume naye anakuwa na wanawake kama hao au zaidi na kila mmoja akiwa na wapenzi kama hao au zaidi na kutengeneza mzunguko ambao unaweza kuleta maambukizi ya VVU/UKIMWI na kupoteza nguvu kazi ya taifa.

Kwa upande wangu naona kwamba wasanii maarufu karibu wote wana maambukizi ya VVU ila kwa kuwa ni ugonjwa usiopimwa kwa macho wanaonekana wako vizuri. Hii inafanya sekta ya sanaa nchini hususani ya filamu na musiki kuonekana ni moja ya shughuli hatari sana kwq vijana wanaotegemea kujishughulisha nayo.

Pengine unawafahamu wasanii wenye mahusiano mengi kwa wakati mmoja, unaonaje kama wakipimwa kwa pamoja majibu yatatoka vipi?
 
Usizoee kusema wasanii wetu. Ni aibu. Wengine hatuna wasanii wala sio mdau kabisaaaa wa hao watu. Sipendi tabia zao, siwapendi, na hata kazi zao sijui kazi. Wanachofanya sikipendi. Wakaa uchi
 
Hatari, unaonaje wasanii wote kuwa huenda wana HIV!
Wewe unaamini kila unalosoma kwenye gazeti au kilanunachoona mtandaoni?
Wasanii nao ni kama binadamu wengine.
Tena inawezekana kabisa sisi tusio wasanii ni wazinzi tuliotukuka kupita hao wasanii.
 
Hatari, unaonaje wasanii wote kuwa huenda wana HIV!
Wewe unaamini kila unalosoma kwenye gazeti au kilanunachoona mtandaoni?
Wasanii nao ni kama binadamu wengine.
Tena inawezekana kabisa sisi tusio wasanii ni wazinzi tuliotukuka kupita hao wasanii.

Kwahiyo tuseme habari zao tunazozisoma humu ni uongo?
 
Sio kila habari ina ukweli asilimia zote.
Nyingine ukweli, nyingine tetesi, nyingine uongo, nyingine uzushi .Akili kumkichwa!.
So ukisikia Wema Sepetu katembea na Ridhwani nawewe unalichukua kama lilivyo?

Kwanini nisiamini?
 
Wasanii kitu gani.... Huku mitaani fanya utafiti. Ukimaliza endelea na sekta nyingine, jeshini, walimu, madaktari, wavuvi nk nk, eti wasanii... Hao cha mtoto.
 
Mimi sikubali kuwa kuna mtu unaweza kuliingiza dudu lako kwa mdada ambaye hujapima naye tena bila ya condom naona haiwezekani na hii si kwa wasanii tu bali ni kwa watu wote
 
Mimi sikubali kuwa kuna mtu unaweza kuliingiza dudu lako kwa mdada ambaye hujapima naye tena bila ya condom naona haiwezekani na hii si kwa wasanii tu bali ni kwa watu wote

Wewe jiulize wale makahaba wa sinza wanapima saa ngapi wakiwa kwenye shughuli zao? au wanaume wanaoenda kuwanunua wanahakikisha vipi afya zao? mwisho jiulize kwanini maambukizi ya VVU hayaishi kama huamini watu wanaweza kufanya mapenzi bila kujua afya zao na za wenzao?
 
wengine humu wanafanya huko uchochoroni hata zaidi ya hao wasanii ila kwakuwa wanatoka na watu wasiojulikana ndo maana.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…