Kama watoto wadogo wanaweza piga mbizi na kwenda na kasia mpaka kwenye ndege ilozama wakati wana maji wakiogopa kusogelea Je tubadili mfumo wa Elimu?

Kama watoto wadogo wanaweza piga mbizi na kwenda na kasia mpaka kwenye ndege ilozama wakati wana maji wakiogopa kusogelea Je tubadili mfumo wa Elimu?

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Nimejiuliza sana juu ya hivi Kwanini lisiwepo somo la self defense Kama Ulaya mtu ajue kuogelea na kujikinga na baadhi ya majanga?

Simaanishi waliopata ajali ndo waogelee namaanisha mfumo wetu wa elimu wa ku kalili mambo ya kinjekitile kichwani bila msaada wowote bora Liwepo somo la uokoaji uogeleaji na maisha halisi kuliko kila siku tunajifunza ambayo hayasaidii!

Jiulize swali kwakuwa tunaingia tu kazini kula pesa wakati hatujui hata Majukumu yetu ! Waokoaji wa ndege ilozama walizidiwa Mpaka na watoto wadogo wavuvi ambao waliweza zama ndani wakati waokoaji wakitegeana!


Tuna haja ya kubadili mfumo wa Elimu yetu uendane na Maisha halisi
Mtu anaitwa Mwanamaji kikosi cha uokoaji Uko angalia vema hawajui hata kuogelea

Britanicca
 
Vijana wengi sasa hivi wanapenda wawe kama wakina mondi konde jux ndy role model zao namba moja
Bush ndy kuna wajasiri, we huoni mandonga, pierre sjui spider mkata mauno wanaonekana Shuja kwa watu
Wakati mashuja wenyewe wapo

Ova
 
Nimejiuliza sana juu ya Hivi Kwanini lisiwepo somo la self defense Kama Ulaya mtu ajue kuogelea na kujikinga na baadhi ya majanga? ..
Kujifunza kuogelea muhimu, ikibidi ata tunavyokuza watoto unawapeleka training ya kuogelea na kung fu sio kukaa kaa kizembe, kuhusu kinjikitile iyo ni history ya tz na ni muhimu, bora ungesema ifutwe ya waliogundua vitu vyetu mito, maziwa na milima wakati ancestors wetu walikuwepo
 
Nimejiuliza sana juu ya Hivi Kwanini lisiwepo somo la self defense Kama Ulaya mtu ajue kuogelea na kujikinga na baadhi ya majanga?...
Kwa kuwa wanamaji hawakuwepo sio kigezo cha kuwadharau na kuwachukulia poa tu. Kutokuwepo katika eneo la tukio hakumaanishi wameshindwa kazi au hawaiwezi zipo sababu nyingi tu.
 
Haya masomo ya kuogelea zaidi huwa naona yanatolewa shule za michepuo ya kiingereza, english medium, kuna vipindi kabisa kwa ajili hiyo, na watoto wanatakiwa kuwa na nguo za kuogelea.

Tatizo lipo kwenye shule zetu za kayumba, huko hakuna hilo somo, au kama lipo litakuwepo kwa shule chache sana, tena kwa theory; na sidhani kama linawezekana kufanywa kwa practicals sababu ya uchache wa maeneo ya kujifunzia kuogelea, na wingi wa wanafunzi waliopo mashuleni.

Lakini kuhusu watoto wadogo kuwa wa kwanza kukimbilia majini kuokoa watu sishangai, hao wanayajua maji toka kuzaliwa, maji ni sehemu ya maisha yao, wameyazoea.

Hawa wakiamua kutumbukia majini huwa hawajiulizi mara mbili, ni tofauti na mwenzangu nami ambaye katoka bara huko hakuna ziwa wala mto akaamua kujifunza kuogelea, huyu kuingia majini lazima kwanza ajiulize mara mbili.
 
Nimejiuliza sana juu ya Hivi Kwanini lisiwepo somo la self defense Kama Ulaya mtu ajue kuogelea na kujikinga na baadhi ya majanga?...
Wakati mwingine ujinga unasaidia.

Huenda wasomi Walikuwa wanaogopa ndege kulipuka kutokana na uzoefu wao.

Lakini, asiyepata elimu ya masuala ya ndege huwa hajui kuwa ndege inalipuka na hivyo hushiriki kikamilifu kutoa msaada wa uokozi.

Nionavyo Mimi: wakati mwingine ujinga unaweza kuwa msaada mkubwa na elimu ikawa si msaada kutokana na Tahadhari anayokuwa nayo msomi katika kutenda jambo fulani.
 
Indigenous knowledge + experience kwenye local area ....hii ndo kilichofanyika kutokana na shughuli za jamii husika katika maeneo yao. Ukienda maeneo ya misitu wenyeji wahuko huwana ujuzi wa asili kuishi na misitu inayo wazunguuka sambaba na maene ya mito na maziwa hata milima

Wajanja wenye upeo hujakujifunza elimu na ujizi wa asili then huuchakata katika mifumo ya Kitaalam ...huku ku underrate communities zisizo enda shule bila ku scope ujuzi wa asili ya ikolojia ya eneo husika

Rethink.....
 
Nimejiuliza sana juu ya Hivi Kwanini lisiwepo somo la self defense Kama Ulaya mtu ajue kuogelea na kujikinga na baadhi ya majanga?...
Yule kijana "Maja Mnyama" aliyesaidia uokozi kwa ujasiri na ushupavu mkubwa bila hayo mafunzo rasmi, sasa anaenda kutiwa uoga na kupewa protokali za kijinga za kauli za "tuna upungufu wa vifaa", au tunasubiri vifaa kutoka Afrika ya Kusini.

Kiufupi tuna elimu ya kijinga na haifit kabisa mazingira ya Tz na Africa.
 
Nimejiuliza sana juu ya Hivi Kwanini lisiwepo somo la self defense Kama Ulaya mtu ajue kuogelea na kujikinga na baadhi ya majanga? ...
Hivi wale flight attendants wote walienda kujifungia kwenye cockpit? Kama wanakaaga kale ka siti ka nyuma kwanini hawakufungua mlango kwa ndani🤔🤔🤔🤔.

Marubani mikanda ili-jam? Kwanini hawakufungua mlango wao watokee kwa abiria?
 
Tunawasiliana na pilot walisikika wakisema.....wakati pilot anamuomba kijana Majaliwa avunje kioo....najiuliza maswali.

Hivi sasa hayo mawasiliano yalikuwa ya aina gani tofauti na aliyokuwa akiwasiliana na kijana Majaliwa kuwa avunje dirisha....
 
Wakati mwingine ujinga unasaidia.
Huenda wasomi Walikuwa wanaogopa ndege kulipuka kutokana na uzoefu wao....

Tahadhari ama uoga tu...they are simply cowards and lazy.

Ajali ikitokea ni kupambana na kuokoa ndio maana wanalipwa risk allowance...ukishakuwa jeshini kuna kufa au kupona..tahadhari tena?!...
 
Siongei kwa kukashifu.

Ila vikosi vingi hawafanyi mazoezi kwenye maji.

Nakuhakikishia vikosi vya uokoaji kwa hapa Bongo wanaogopa maji.. Siyo ya swimming pool... Bali maji ya mawimbi kama bahari au deep ziwani..

Wavuvi kwakuwa muda mwingi wapo majini hawaogopi waves za maji.. Lakini vikosi vyetu havina mazoezi... Muda mwingi wapo bar wanaagiza bia tu.

Mimi hii ajali imenisikitisha sana
 
Siongei kwa kukashifu.

Ila vikosi vingi hawafanyi mazoezi kwenye maji.

Nakuhakikishia vikosi vya uokoaji kwa hapa Bongo wanaogopa maji.. Siyo ya swimming pool... Bali maji ya mawimbi kama bahari au deep ziwani..

Wavuvi kwakuwa muda mwingi wapo majini hawaogopi waves za maji.. Lakini vikosi vyetu havina mazoezi... Muda mwingi wapo bar wanaagiza bia tu.

Mimi hii ajali imenisikitisha sana
Upo sahihi. Tanzania tunajali nadharia na hotuba hotuba yani maneno matamu matamu kuliko vitendo
 
Back
Top Bottom