Kama wazo la kujinyonga linakujia mara kwa mara kwasababu ya ugumu wa maisha, pitia hapa

Kama wazo la kujinyonga linakujia mara kwa mara kwasababu ya ugumu wa maisha, pitia hapa

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
4,580
Reaction score
7,943
Habari!

Nimesikitika sana kusikia habari ya mwanaJF mwenzetu kujinyonga kisa ugumu wa maisha.

Tafsiri ya ugumu wa maisha hutofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine kulingana na background ya mtu.

Mwingine akisema ninapitia maisha magumu anamaanisha hata kula yake ni ya kimuujiza, mwingine akisema maisha magumu ujue anamaanisha kuwa hawezi kupata mahitaji au fedha ya kufanya surplus lakini anakula na analala bila wasiwasi.

Sasa kama unawaza kujinyonga kisa hujui pa kula au hata pa kulala ni shida kwako usisite kuja PM, nitakuhoji na nikijiridhisha kuwa una hali ngumu zaidi nitakusaidia bila masharti.

Note: Swali la kwanza nitakalokuuliza ni;
Unatumia smartphone ya nani na ina gharama gani, kwanini hujaigeuza (kuiuza) kuwa mtaji wa kununua na kuuza matunda?
 
Inategemea na wewe jinsi ulivyo wengine unaweza kusema Wana roho/miili mepesi
Hawawezi kukabiliana na changamoto
Na haswa Hao wanahitaji msaada
Ila Kuna watu humu wakisema watiririke kwa waliyoyapitia kwenye Maisha"unaeza kusema mbona hawajaamua kuchukua uamuzi wa kujitoa uhai" unakuta mtu una makesi, una matatizo ya kifamilia, una matatatizo ya kifedha, mambo hayaendi lkn unakomaa tu
Ila nachojua watu tumeumbwa tofauti na ulilelewa ktk malezi gani?

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sio mwanasaikolojia indeed.
Kama mkuu wa kitengo cha Psychology UDSM alijinyonga lazima jamii ijue kuwa watu wa zama hizi wanataka kutatuliwa shida zao na si ushauri
Lakini usifanye hitimisho kuwa kila anaejinyonga ana shida na pesa kuna watu wana hizo pesa. Sema kujinyonga sio jambo zuri Ila yawezekana ni njia ya kifo kama njia nyingine kama ugonjwa, ajali na nyinginezo sipingi unachofanya ni jambo zuri keep it up.
 
Wengine ni mapenzi, wengine tatizo la akili n.k
That's why nimesema kwa wale wanaotaka kujinyonga kwa ugumu wa maisha
Lakini usifanye hitimisho kuwa kila anaejinyonga ana shida na pesa kuna watu wana hizo pesa. Sema kujinyonga sio jambo zuri Ila yawezekana ni njia ya kifo kama njia nyingine kama ugonjwa, ajali na nyinginezo sipingi unachofanya ni jambo zuri keep it up.
 
NAPINGANA NA WEWE

Elewa mantiki husika, elewa level ya tatizo lililozungumziwa na ndio maana ajasema “kuwa na Smartphone” bali “una Smartphone ya shingapi” huwezi eti ukawa na shida kihasi cha kula yako ya leo huijui na kesho changamoto then ukawa na Smartphone ya thamani ya 200,000/= hapo hata mwenye ujaona umuhimu wa kujisaidia uza simu hiyo nunu Smartphone ya 60,000/= mbona hii nayotumia mie nimenunua 50,000/=

Hii nishafanya sana nikivyokuwa nasoma.
Pia sio kila anayetumia smartphone ana maisha mazuri. Inabidi arekebishe hapo

Portfolio | 2020
 
Mkuu kujiua sio matokeo ya ugumu wa maisha,ni matokeo ya mtazamo wetu kuhusu maisha na mambo yote tunayodeal nayo.Wengi wanaofikia kujiua huwa wanashindwa/wanakosa mtu wa kuzungumza nae na kumueleza yale yanayowasibu,Wengine wanahitaji msaada wa kitaaluamu kwa sababu ya Msongo wa mawazo.

Binafsi natambua kwamba kama mtu ameshafikia hatua ya kujinnyonga/kujiua basi anahitaji msaada tena msaada mkubwa sana na mara nyingi ni msaada wa kitaalam zaidi kuliko kutatuliwa shida yake kwani tatizo sio shida yake tatizo ni mtazamo wake kuhusu shida yake.

Ndio maana kuna wanaojiua kwa sababu ya mapenzi,kukosa cheo,kunyimwa kile wanachokitaka,kuulizwa kuhusu mienendo yao.etc.Ni tatizo la jinsi tunavyo yashughulikia mambao yetu hasa kimtazamo.
 
NAPINGANA NA WEWE

Elewa mantiki husika, elewa level ya tatizo lililozungumziwa na ndio maana ajasema “kuwa na Smartphone” bali “una Smartphone ya shingapi” huwezi eti ukawa na shida kihasi cha kula yako ya leo huijui na kesho changamoto then ukawa na Smartphone ya thamani ya 200,000/= hapo hata mwenye ujaona umuhimu wa kujisaidia uza simu hiyo nunu Smartphone ya 60,000/= mbona hii nayotumia mie nimenunua 50,000/=

Hii nishafanya sana nikivyokuwa nasoma.

Portfolio | 2020
Ukifikia stage ya kujiua,hata kama una smartphone hutaweza kuiuza,na ukiiuza haitauzika kwa sababu unakuwa na VIBE MBAYA sana.ni suala la mtazamo zaidi kuliko uwezo.
 
Pamoja na kuzaliwa familia masikini wenye uwezo mdogo lakini nakula vizuri, namiliki smartphone ya 200k na nilinunua mwenyewe pia namudu kuweka vocha za bundle ili kusukuma siku lakini maisha yangu bado siyo mazuri, furaha ni ya kulazimisha kwa sababu ya ugonjwa ulionipa ulemavu. Ulemavu ukaleta changamoto nyingine nyingi maumivu ya kila siku na zingine ni za aibu kuelezea hapa. Upweke kwangu ni 24/7 hivyo mawazo ya kufa huwa yanakuja mara kwa mara tena akili inaniambia kabisa "KUFA NI KUPUMZIKA" mara zingine natamani ningekuwa jela kuliko kuumwa ndani, au ningekuwa masikini wa mwisho lakini niwe na Afya njema. Wanaojiua wanasiri nyingi ambazo hazisemeki wakati mwingine. Imagine mtu ambaye ana Impotence anawezaje kusema

NB: kuna watu watadhani mimi ndo nina impotence
Mkuu nakubaliana na wewe kabisa.Suicide huanza na mtazamo,Jinsi unavyochukulia jambo.Ndio maana huwa wenye tatizo kama hilo hukutanishwa na watu wenye matatizo kama haya ili wabadilishane uzoefu na kutiana moyo jinsi ya kucope
 
Back
Top Bottom