Kama wazo la kujinyonga linakujia mara kwa mara kwasababu ya ugumu wa maisha, pitia hapa

Kuna uzi humu unasema KAZI GANI ULIFANFA ULIPOPITIA MSOTO humo ndio utajua watu majasiri na wamepitia magumu ila wanapambana hadi kieleweke

Watu wangepitia Uzi ule wangejifunza mengi na kuacha hayo mawazo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukifikia stage ya kujiua,hata kama una smartphone hutaweza kuiuza,na ukiiuza haitauzika kwa sababu unakuwa na VIBE MBAYA sana.ni suala la mtazamo zaidi kuliko uwezo.
Sijazungumzia kujinyonga elewa nilichojibu.

Portfolio | 2020
 
Ni Sawa na una shida kwahio uuze kitendea kazi chako, no sio sahihi! Hata hivyo "smartphone ya shilingi ngapi" does guarantee kiwango cha shida au kiwango cha kuhitaji msaada. Very soon itakua kama basic need tu kuwa na smartphone. Sasa Mpwa nikiuza smartphone nitawezaje kutafuta kazi, kuperuzi taarifa za kazi na kutuma maombi???

Kwa mtazamo wangu, ingekua Mimi ningekusaidia kwa kadiri Mungu atakavyosaidia bila kuwa judgemental. Maana kama unaanza kuniuliza "simu ya shilingi ngapi", then possibly utaniuliza umevaa nguo za shilingi ngapi, viatu vya bei gani, umekula msosi wa bei gani, unaishi nyumba ya bei gani etc.

Kuwa na shida, stress, depression and the like hadi kufikia hatua ya kajinyonga au kuomba msaada doesn't mean niwe na simu ya being ndogo, niwe rough, nisiwe na makazi mazuri, No, TUNATOFAUTIANA KIWANGO CHA UHITAJI kwahio ukishindwa kunisaidia kwa sababu ya "bei ya simu" nitakushangaa Mpwa.

Miaka kadhaa hapa jukwaani alijitokeza binti mmoja akaanzisha Uzi kuwa "Anauza Uchi ili aweze kuishi mjini na apate ada". Nilimfuata inbox tukaongea kwa kirefu sana na niliweza kumpa nilichompa, nimefurahi siku moja kumuona amekua AGENT anatangaza bidhaa sake kwenye makundi ya WhatsApp.

Sasa tukisema uza simu au lugha yoyote yenye uelekeo wa kuwa judgemental hatutakua tunawasaidia, wengine tunahitaji maneno ya faraja tu.

Hapo vipi Mpwa, nikutakie Siku njema.
 
Sijazungumzia kujinyonga elewa nilichojibu.

Portfolio | 2020
Nimekuelewa,nimeweka msisitizo kwamba,unapokuwa na anxiety hata njia ya nyumbani unasahau,hata mambo madogo utashindwa kuyaamua au kuyafanya.
 
Pokea like yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nahisi hatutaelewana mpaka duniaa inaisha kwa lugha nyingine ni unajua kuandika vizuri ila hujui kusoma hoja vizuri.

Kwakuongeza jifunze kusoma kilichoandikwa.

Period, naomba upigwe na njaa ya week moja ndio utajua ni tofauti ya ‘Smartphone’ na ‘Smartphone ya shingapi’

Portfolio | 2020
 
Pole sana daviie, Usichoke kuomba huruma ya Mwenyezi Mungu ipo siku atakupatia ahueni na kwa maombezi ya Mt. Yuda Tadei usifikiri hata siku moja kwamba bwana amekuacha!!

Magumu ni sehemu ya maisha ya mwanadamu huku duniani, usikate tamaa!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asee...
 
Elli.
Ankali umeongea mengi mazuri sana, heshima nyingi kwako... ila pale ulipogusia “tunatofautiana uhitaji” ndipo kwenye msingi wa mada mezani.

Umeeleza hayo kwa kadri ya mdau uliyekuwa unamjibu, ila hoja ya Bonde la Baraka ni kwa wale ambao hata ‘kula’ yao ni muujiza.... ni kweli kuwa tunatofautiana uhitaji na hata mitazamo juu ya ‘mapitio’ maishani.
 
Barikiwa sana na asante kwa kujazia pale ambapo sikupataja, ndio afya ya mjadala. Blessed
 
Akishauza halafu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…