PreGE2025 Kama wenyewe wanakiri kabisaa "Oktoba tuna-tik Tu", kuna haja gani ya uchaguzi?

PreGE2025 Kama wenyewe wanakiri kabisaa "Oktoba tuna-tik Tu", kuna haja gani ya uchaguzi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Huko lumumba hakuna watu wenye Akili? Hadi wanakuja na msemo huu wa hovyo?
Yaani unasema kabisaa kuwa ikifika kipindi cha uchaguzi tutakuwa tunatick Tu Kwa upande wa CCM hii imekaaje?

Kuna haja ya kupiga kura ilhali wenyewe mnakiri hadharani kuwa hatupigi Kura zaidi ya kutick kwenye makaratasi? Watanzania tumeshuhidia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa jinsi wasimamizi wa uchaguzi walivyokuwa wanatick wagombea wao wa CCM.

Kura yangu nitailinda mwenyewe Kwa kutopiga Kura kwasababu ni Kura yangu Nina uwezo wa kuitumia au kukataa
Kule, watu wenye busara na nia njema ni wachache. Taifa letu limejaa wezi, wauaji, wabakaji, na wahalifu wa kila aina. Kwa bahati mbaya, wengi wao hujificha ndani ya chama tawala ili kulinda maovu yao. Hatimaye, hupewa nafasi nyeti za maamuzi serikalini na ndani ya chama, wakifurahia keki ya taifa. Hawa watu ndio wanaamua hatma ya taifa. Usitarajie jambo jema kutoka kwa mtu mwovu, hata kama yupo kwenye jukwaa sahihi. Ni lazima tuwe waangalifu sana.
 
Msije mkashangaa hata jina la Pm liko tayali kwenye bahasha ili lipelekwe bungeni na yule mama sijua wanamwita adc sijui ads sikumbuki vizuri kwa ajili ya kuidhinishwa
 
Back
Top Bottom