MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Kwanza kabisa nakubaliana kuwa maisha hayana kanuni kwenye kuyaishi. Kila mmoja ana njia zake za kujipatia kipato ili mradi ni halali. Pia kila mmoja ana tafsiri yake ya utajiri na umaskini. Kwa upande wangu kama una kipato cha chini ya $10000 (Approximately Tsh 28m) kwa mwaka basi wewe ni fukara unayepaswa kupambana haswa.
Nina ushauri ingawa sio lazima wewe kuufanyia kazi. Kwa muda huu unaopambana kujitoa hapo ulipo usijiingize kabisa kwenye jambo lolote linalotafuna pesa bila kurejesha chochote. Jikite kwenye kuongeza vyanzo vya mapato na sio kujibana kutumia hicho kidogo kuwekeza kwenye mambo yasiyotengeneza pesa kama vile kujenga nyumba na kununua gari ya kutembelea. Pia tafuta mpenzi anayependa miwa na mahindi ya kuchoma kuliko Pizza na Shawarma.
Hata kama unataka sana ardhi fanya ujanja wa kwenda vijijini ununue kwa bei ndogo uliendeleza ili baadae likuletee manufaa. Binafsi kipindi nikiwa fukara wa kukosa milioni 28 kwa mwaka nilitumia kiasi kidogo sana cha pesa kisichozidi hata milioni moja kununua ekari kadhaa huko Karatu karibu kabisa na Ngorongoro. Ninavyoandika hapa hayo maeneo kumeanza kujengwa camps na hotel za kitalii. Ina maana thamani ya eneo langu imeshapanda.