Kama wewe bado ni fukara wa kipato cha chini ya Tsh 28m kwa mwaka soma hapa

Matajiri mtuache na maisha yetu, kwani tushawagongea milango kutaka msaada.

Hapa nasikiliza kibao cha OTTU JAZZ BAND, wazee wa msondo ngoma, kibao kinaitwa MAPENZI YA RABANA.

kuna kipande mzee gurumo anasema
"wala si ujinga kwa wale mafukara na si ujanja kwa wale matajiri, tuache kudharauliana,"
Kisha waitikiaji wanajibu
" haya yote ni mapenzi yake rabana"

Kisha hapo linaburuzwa gitaa la hatari na saidi mabela..
Kibao safi kabisa hiki.
Hii imenikosha hahahahaha
 
Hakika kibao hiki kilitamba sana Mia law ya 80’s maisha ya utajiri ni kazi yake rabana 🙏
 
Kwanza kabisa nakubaliana kuwa maisha hayana kanuni kwenye kuyaishi. Kila mmoja ana njia zake za kujipatia kipato ili mradi ni halali. Pia kila mmoja ana tafsiri yake ya utajiri na umaskini. Kwa upande wangu kama una kipato cha chini ya $10000 (Approximately Tsh 28m) basi wewe ni fukara unayepaswa kupambana haswa.

Nina ushauri ingawa sio lazima wewe kuufanyia kazi. Kwa muda huu unaopambana kujitoa hapo ulipo usijiingize kabisa kwenye jambo lolote linalotafuna pesa bila kurejesha chochote. Jikite kwenye kuongeza vyanzo vya mapato na sio kujibana kutumia hicho kidogo kuwekeza kwenye mambo yasiyotengeneza pesa kama vile kujenga nyumba na kununua gari ya kutembelea. Pia tafuta mpenzi anayependa miwa na mahindi ya kuchoma kuliko Pizza na Shawarma.

Hata kama unataka sana ardhi fanya ujanja wa kwenda vijijini ununue kwa bei ndogo uliendeleza ili baadae likuletee manufaa. Binafsi kipindi nikiwa fukara wa kukosa milioni 28 kwa mwaka nilitumia kiasi kidogo sana cha pesa kisichozidi hata milioni moja kununua ekari kadhaa huko Karatu karibu kabisa na Ngorongoro. Ninavyoandika hapa hayo maeneo kumeanza kujengwa camps na hotel za kitalii. Ina maana thamani ya eneo langu imeshapanda.
Utashangaa huyu ndio kinara wa kubeba zile vocha za bure
 
Mkuu umeongea jambo la msingisana , weng wanakupuuza ila nmekuelewa, ni kama ulikua unaongea na mimi
Kuna uzi wang naomba msaada wa ushaur wako boss

Ukweli mtupu, bro
 
Mkuu umeongea jambo la msingisana , weng wanakupuuza ila nmekuelewa, ni kama ulikua unaongea na mimi
Kuna uzi wang naomba msaada wa ushaur wako boss

Mkuu usije ukauza nyumba yako. Mimi ni mjasiriamali nisiyeogopa hatari ila kwa uzoefu wangu naona kujenga nyumba ni kama suala la kiimani sana... yaani mtu usipokuwa makini unaweza kugonga 50yrs huna hata kibanda cha nyasi. Wewe nakupongeza sana kujenga ukiwa mdogo. USIJILAUMU KWA CHOCHOTE. Ushauri zaidi nimepost kwenye uzi wako.
 
Back
Top Bottom