Kama wewe bado ni fukara wa kipato cha chini ya Tsh 28m kwa mwaka soma hapa

Kama wewe bado ni fukara wa kipato cha chini ya Tsh 28m kwa mwaka soma hapa

Acha kuwapa watu wasiwasi maisha ni njia tu ,kila mtu anaridhika na hali yake ...Anza na ndugu zako kwanza wanaokunya vichakati huko Arusha .
Jomba kwani ukikusanya hela zako zote kwa mwaka hazifiki 28m?
 
Kwanza kabisa nakubaliana kuwa maisha hayana kanuni kwenye kuyaishi. Kila mmoja ana njia zake za kujipatia kipato ili mradi ni halali. Pia kila mmoja ana tafsiri yake ya utajiri na umaskini. Kwa upande wangu kama una kipato cha chini ya $10000 (Approximately Tsh 28m) basi wewe ni fukara unayepaswa kupambana haswa.

Nina ushauri ingawa sio lazima wewe kuufanyia kazi. Kwa muda huu unaopambana kujitoa hapo ulipo usijiingize kabisa kwenye jambo lolote linalotafuna pesa bila kurejesha chochote. Jikite kwenye kuongeza vyanzo vya mapato na sio kujibana kutumia hicho kidogo kuwekeza kwenye mambo yasiyotengeneza pesa kama vile kujenga nyumba na kununua gari ya kutembelea. Pia tafuta mpenzi anayependa miwa na mahindi ya kuchoma kuliko Pizza na Shawarma.

Hata kama unataka sana ardhi fanya ujanja wa kwenda vijijini ununue kwa bei ndogo uliendeleza ili baadae likuletee manufaa. Binafsi kipindi nikiwa fukara wa kukosa milioni 28 kwa mwaka nilitumia kiasi kidogo sana cha pesa kisichozidi hata milioni moja kununua ekari kadhaa huko Karatu karibu kabisa na Ngorongoro. Ninavyoandika hapa hayo maeneo kumeanza kujengwa camps na hotel za kitalii. Ina maana thamani ya eneo langu imeshapanda.
uvccm mkishiba huwa mnaandika ushuzzy tu.
 
Watu wenye kipato cha 2m kila mwezi hapa Tanzania hawafiki 5% ya watanzania wote, kwahiyo unamanisha nchi zima ni masikini......huo utafiti wako sio sahihi kabisa
Sure Tanzania ni miongoni mwa nchi masikini hata hivyo
 
Matajiri mtuache na maisha yetu, kwani tushawagongea milango kutaka msaada.

Hapa nasikiliza kibao cha OTTU JAZZ BAND, wazee wa msondo ngoma, kibao kinaitwa MAPENZI YA RABANA.

kuna kipande mzee gurumo anasema
"wala si ujinga kwa wale mafukara na si ujanja kwa wale matajiri, tuache kudharauliana,"
Kisha waitikiaji wanajibu
" haya yote ni mapenzi yake rabana"

Kisha hapo linaburuzwa gitaa la hatari na saidi mabela..
Kibao safi kabisa hiki.
Ah huku ukishushia na mvinyo laini kwenye koo unahisi rahaa afu mbele toto mbili tatu zinakatika katika
 
Ah huku ukishushia na mvinyo laini kwenye koo unahisi rahaa afu mbele toto mbili tatu zinakatika katika
Unasahau shida zote za dunia, hukumbuki deni la baba mwenye nyumba, hukumbuki hela yenyewe uliipata kwa ugumu kiasi gani.
 
Acha niache mitoko ya kwenda pub na maeneo ya katikati ya mji na nijikite kufanya mitoko ya kula mshindi na miwa huenda "my wangu" mpenda mahindi na miwa nitampata huko.
 

Attachments

  • Screenshot_20240831_093109_Chrome.jpg
    Screenshot_20240831_093109_Chrome.jpg
    553.7 KB · Views: 8
Back
Top Bottom