chumachakavu
Member
- Oct 1, 2017
- 55
- 103
Jiepushe na mikopo ya muda mrefu. Binafsi nashauri usikope zaidi ya mwaka mmoja.
Kama lengo lako ni kujenga nyumba, fanya hatua kwa hatua mpaka nyumba itakapoisha. Utatumia gharama na riba ndogo kuliko kukopa kwa muda mrefu, na pia unepunguza hatari ya nyumba kutokamilika.
Kama unataka kufanya biashara, fanya vivyo hivyo. Kwanza chunguza mwenendo wa biashara; pili, hata kama itashindikana, utaweza kujifunza mapungufu na kurudi kwa haraka.
Biashara yenye mafanikio inaweza kukua kidogo kidogo kila mwaka, usiharakishe kufungua biashara kubwa kwa muda mfupi kwani utafail.
Mfano halisi: unaweza kukopa kila mwaka kipindi cha mavuno kununua mazao; faida yake mara tatu ya kile ulichokopa.
Kwa ufugaji, nunua mifugo kila mwaka. Fanya hivyo kwa miaka mitano kisha acha mtaji ujiendeshe wenyewe. Kwa mfano, ukikopa milioni 4 kwa mwaka, unaweza kununua ndama 10.
Baada ya miaka 5, utakuwa na ng’ombe zaidi ya 70 kwa sababu ndama wa mwanzoni watakuwa wameshazaa. Hii ni njia ya kujiandaa pensheni kwa miaka 5.
Mungu awabariki.