Kama wewe ni mtumishi wa umma au mfanyakazi anayetegemea mshahara, fuata ushauri huu

Kama wewe ni mtumishi wa umma au mfanyakazi anayetegemea mshahara, fuata ushauri huu

Nitafata ushauri huu masna nimekuwa muoga kukopa kwa hofu ya riba kubwa
 
Napenda kuuliza mwalimu wa degree mpya anaweza kopa shilingi ngapi akitaka mkopo wa mwaka mmoja tu
 
Hao ndama hawataugua? Hawatahitaji Mchungaji?? Gharama za Mchungaji zinatoka wapi??? Gharama za madawa wakiugua zinatoka wapi???

Kuibiwa je???


Unapo-analyse kitu onyesha pande zote yaani upande hasi na upande chanya pia.

Maisha yangekuwa rahisi hivyo nadhani kila nyumba kungelikuwa na Ng😱mbe 70+.
Most people are so afraid of losing money that they lose. They go broke over a duplex. Financially, they play life too safe and too small. They buy big houses and big cars, but not big investments.-Robert kayosaki ameandika haya
Je, unapokopa ununue gari au simu mbona hatuwazi gari kuungua, kuibiwa,extra cost za mafuta na service?!!
 
Neno la kuponya, atakaye kuelewa atapona, nyongeza...sheria na riba za taasisi za kukopesha kwa hapa Tanzania, siyo rafiki kwa wateja. Ukilijua hilo utajikuta unaangukia kwenye ushauri wa mtoa mada
 
Jiepushe na mikopo ya muda mrefu,binafsi nashauri usikope zaidi ya mwaka mmoja.Kama lengo lako ni kujenga nyumba fanya hivyo mpaka nyumba itakapo Isha utakuwa umetumia gharama kidogo/riba ndogo kuliko kukopa kwa muda mrefu na huwenda nyumba isikamilike.
Kama unataka kufanya biashara fanya hivyo hivyo,kwanza utaona trend ya biashara inavyokwenda pili hata kama biashara itafail utaweza kurudi tena kwa kusoma mapungufu yaliyo kukwamisha baada ya muda mfupi.Kama biashara inakwenda vizuri unao uwezo wa kufungua biashara mpya kila mwaka( usitake kufungua biashara kubwa kwa muda mfupi utafail).
Niwape mifano halisi,unaweza kukopa kila mwaka kipindi cha mavuno,kwa kununua mazao,faida yake huwa mara tatu ya kile ulichokopa
Kama upo katika mazingira ya ufugaji,nunua mifugo kila mwaka,fanya hivyo kwa miaka mitano kisha acha mtaji ujiendeshe wenyewe,utakuja kuona umeandaa pensheni yako kwa miaka 5.Mfano kama unaweza kukopa mil 4 kwa mwaka,kiasi hicho unaweza kununua ndana 10, kwa miaka 5 utakuwa na mtaji wa ng'ombe zaidi ya 70 kwa kuwa wale ndama wa mwanzoni watakuwa wameshazaa mara moja moja na wengine mara mbili mbili.Mungu awabariki
Hakuna anayependa kuwa na mkopo wa muda mrefu, tatizo ni marejesho. Mfano ukikopa million 100;

1. Kwa mwaka mmoja utarejesha benki jumla ya million 110 . Hizo Million 110 ukigawa kwa mwaka mmoja yaani miezi 12, kila mwaka utarejesha Million 9,166,667. Hiyo ni hela ndefu.
2. Ukirejesha kwa miaka miwili, jumla utalipa million 120. Million 120 ukizigawa kwa miezi 24 (Miaka miwili) utalipa kila mwezi Million 5.
3. Ukirejesha miaka 3 itakuwa Million 130 na utarejesha kwa muda wa miaka 3 kila mwezi Million 3.61
4. Ukirejesha miaka 4 itakuwa Mill 140 na utarejesha Mill 2.92 kwa mwezi
5. Ukirejesha miaka 5 Itakuwa Million 150 na marejesho kwa mwezi ni Mill 2.5
6. Miaka 10 itakuwa million 200 na marejesho ni Million 1.7 kwa mwezi kwa muda wa miaka 10 kila mwezi

Kwa mahesabu hayo hapo juu, utaona kuwa kwa mfanyakazi wa kawaida kukopa akarejesha kwa muda mfupi hakuwezekani kwani ukikopa sheria inakutaka ubakize 2/3 ya mshahara wako.

Hiyo ndiyo sababu wengi wanakopa na kurejesha kwa muda mrefu. Hapo hapo na Benki zinapata faida kubwa.

Angalizo: Ili uendelee lazima ukope. Mkopo maana yake ni nini, ni kuwa ukitaka kufanya development, narudia development; huitaji kutumia cash yako. Tumia hela za watu ili ujiletee maendeleo. Jambo la msingi ni kuhakikisha una uwezo wa kurejesha.
 
Kwa mara ya kwanza nimeona mtu alietoa ushauri mzuri kuhusu kukopa, safi.

Unakopa million 6 unalipa 10M huo ni uduanzi kama huna familia na majukumu makubwa bora usikope save pesa yako mwenyewe ,

Hasa kwa wale wanaokopa kwaajili ya kununua gari na kujenga utajikuta unaishi maisha magumu sana
Nimejaribu kujenga hoja hapo juu
 
Back
Top Bottom