Kama wewe ni mtumishi wa umma au mfanyakazi anayetegemea mshahara, fuata ushauri huu

chumachakavu

Member
Joined
Oct 1, 2017
Posts
55
Reaction score
103
Jiepushe na mikopo ya muda mrefu. Binafsi nashauri usikope zaidi ya mwaka mmoja.

Kama lengo lako ni kujenga nyumba, fanya hatua kwa hatua mpaka nyumba itakapoisha. Utatumia gharama na riba ndogo kuliko kukopa kwa muda mrefu, na pia unepunguza hatari ya nyumba kutokamilika.

Kama unataka kufanya biashara, fanya vivyo hivyo. Kwanza chunguza mwenendo wa biashara; pili, hata kama itashindikana, utaweza kujifunza mapungufu na kurudi kwa haraka.

Biashara yenye mafanikio inaweza kukua kidogo kidogo kila mwaka, usiharakishe kufungua biashara kubwa kwa muda mfupi kwani utafail.

Mfano halisi: unaweza kukopa kila mwaka kipindi cha mavuno kununua mazao; faida yake mara tatu ya kile ulichokopa.

Kwa ufugaji, nunua mifugo kila mwaka. Fanya hivyo kwa miaka mitano kisha acha mtaji ujiendeshe wenyewe. Kwa mfano, ukikopa milioni 4 kwa mwaka, unaweza kununua ndama 10.

Baada ya miaka 5, utakuwa na ng’ombe zaidi ya 70 kwa sababu ndama wa mwanzoni watakuwa wameshazaa. Hii ni njia ya kujiandaa pensheni kwa miaka 5.

Mungu awabariki.
 
Hao ndama hawataugua? Hawatahitaji Mchungaji?? Gharama za Mchungaji zinatoka wapi??? Gharama za madawa wakiugua zinatoka wapi???

Kuibiwa je???


Unapo-analyse kitu onyesha pande zote yaani upande hasi na upande chanya pia.

Maisha yangekuwa rahisi hivyo nadhani kila nyumba kungelikuwa na Ng😱mbe 70+.
 
Ila richa ya hayo mapungufu mleta mada ana point kubwa sana ya kuachana na mikopo ya muda mrefu
 
Kwa mara ya kwanza nimeona mtu alietoa ushauri mzuri kuhusu kukopa, safi.

Unakopa million 6 unalipa 10M huo ni uduanzi kama huna familia na majukumu makubwa bora usikope save pesa yako mwenyewe ,

Hasa kwa wale wanaokopa kwaajili ya kununua gari na kujenga utajikuta unaishi maisha magumu sana
 
hao ndama ametolea mfano tu unaweza kufanya biashara nyingine ambayo wewe unaona utaweza kuimudu.
 
Ubarikiwe sana kwa maarifa haya
 
watumishi mchukue huu ushauri mkopo usizidi miaka miwili unakua nyonya damu, mtu anachukua milioni kumi kwa miaka kumi seriously? halafu hela unaenda kujengea hapo katikati utaishije? ndani ya miaka miwili unapata shida nyingine unaenda ku top up deni lina shoot mpaka mil 30 kasoro halafu unaondoka na mil 3 hapo ndio taabu zinaanza sasa, watu wanaanza kuacha kadi ya benki ili apewe laki moja.Hizi elimu za mikopo inatakiwa watu wapewe huko makazini hasa ajira mpya just because unakopesheka haimaanishi ukope, tuliza kichwa kwanza na uangalie malengo yako ikiwezekana tafuta hata financial advisors wakushauri hata namna ya kuwekeza hela zako kama huwezi kufanya biashara.
 
Asante, nimeipenda.
 
Ushauri mzuri sana huu. Asante sana
 
Mikopo inatesa sana watumishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…