Kama wewe ni mtumishi wa umma au mfanyakazi anayetegemea mshahara, fuata ushauri huu

Vipi kuhusu kulipa processing fee ya mkopo kila mwaka hauoni kuna kiasi cha fedha unakipoteza? Mkopo wa kijenga kwa mwaka mmoja utapata pesa kidogo ambayo haitatosha chochote kwenye ujenzi kulingana na vipato vya watanzania wengi. Mimi naamini ukisha kopa kwa ajili ya ujenzi lazima utoke kwenye nyumba za kupanga. Ili kile kiasi cha riba kitoke kwenye kodi uliyokuwa unalipa
 
Ufugaji wa wosapu
 
Mikopo ina laana hasa hii ya riba ,ataendelea hivyo mwisho wa siku anaingia mtaani kukopa na halipi .

Mikopo inadhalilisha sana.
 
Ni kweli,mfano Mimi niktaka kukopa million 15 Kwa Muda wa miaka mitano nitarejesha 22 million ,Kwa ongezeko la 7M kama riba,ila hiyo 15M nikisemaa nikope Kwa Kila mwaka Kwa miaka 5 ,Kwa kiasi Cha 3M Kwa riba ya 400K Kwa Kila 3M Kwa miaka mitano nitakuwa na marejesho ya 17M tu
 
Ushauri mzuri kwa watu waoga ,ukikopa milion 2 kwa zama hizi huna kikubwa utakachofanya ,neno ni moja tu kopa kwa malengo ya kuzalisha na hasa uwe tayari umeanzisha kitu na kinalipa kiasi kwamba ukiongezea mtaji zaid kinakuwa better zaidi bila hivyo top up huikwepi
Sioni ubaya wa top ups kwa mtu makini maana hata biashara nyingi unazoona zinashine town wananuka mikopo tu seuze mtumishi kukopa? Watumishi sharti wawe wabunifu wa kufanya biashara hiyo ndiyo njia ya kutoboa tu no way out
Mimi nilikuwa natengeneza pesa mara tatu ya mshahara wangu baada ya mwaka mmoja kazini na nakumbuka nilikopa bank kwa muda wa miaka mitatu.By now nipo busy kuwekeza kwenye kilimo zaidi na biashara zimekuwa vizuri zaidi nipo free kuhusu pesa japo nilikopa kwenye kazi yangu nyakati hizo.
Biashara haidanganyi kadri unavyovuta soksi zako ndivyo inakwenda juu zaidi muhimu uwe mkali ,mtulivu na very calculative kwa kila hatua.Kwa sasa nakopesheka kibiashara tena hela nyingi kuliko ningetegemea mshahara tu nilivyokuwa mtumishi
 
Swali ni je hiyo milion 4 utaizalisha kwa kipi? Frem za biashara tu zilizo location nzuri miji ya kati kwa mwezi ni Tsh 250000-300000 na unalipia at once means ukope milion 4 ulipe mil 3600000ubaki na laki 4 haya uje ukarabati wa sehemu husika hapo utarudi kukopa tu taka usitake 🤣
 
Huyo wa kufanya biashara ya location ya fremu ya 2M-3M hawezi kuwa mfanyakazi mwenye kuwa na makato ya mkopo ya 400K,maana hata angekopa 15 for five years hatamfaa kiutu Kwa mazingira ya biashara ya namba hiyo
 
Kwa ndugu zangu wa halmashauri kopeni mikopoyenu ile isiyo na riba
 
Nitafata ushauri huu masna nimekuwa muoga kukopa kwa hofu ya riba kubwa
Ishu sio riba kubwa kwani wewe unaweza kumpa mtu milion 10 kwa miaka 10 afu uweke riba ya milion 1 ? Jibu ni hapana lazima utarget faida kumbuka hiyo ni pesa nyingi ambayo akifa huyo mtumishi huenda ukawa umeipoteza so the higher the risk the higher the profit.
Mimi nakopesha ila huwa nikimpa mfanyakazi laki 5 tu nabaki nawaza mno naomba Mungu meza isipinduke nikapoteza pesa yangu.

Unakopa miaka 10 umechukua riba ya mil 9 , mil 9 kwenye biashara makini nipesa ambayo naiigiza within one year means unapaswa kufanya uchambuzi wa namna pesa yako itakwenda kujizalisha kufidia riba ili yale makato yasikuumize akili ,kumbuka huku upande wa wafanyabiashara unakopa milion 30 na unatakiwa kuzilipa ndani ya mwaka mmoja hadi miwili tu na watu wanatoboa.Usikope kujenga nyumba wala kusomesha utakuja kulia asiwepo wa kukufuta machozi 😀
 
Huyo wa kufanya biashara ya location ya fremu ya 2M-3M hawezi kuwa mfanyakazi mwenye kuwa na makato ya mkopo ya 400K,maana hata angekopa 15 for five years hatamfaa kiutu Kwa mazingira ya biashara ya namba hiyo
Sasa biashara ni location kaka huwezi kwenda kuweka pesa uchochoroni ambako kuirejesha ni mbinde ndiyo maana simshauri mtu kukopa visenti japo nashauri asikope hadi kufunga mlango wa kukopesheka once more hata na bank nyingine
Mfano miaka mitano ni moderate kabisa na pesa mtu anachukua nyingi ,hii kufikiri eti riba ni kubwa niuvivu wa kufanya kazi maana mtu akipata 3k kwa mwezi tu kama faida hiyo milion 9 ataipata ndani ya miaka miwil na nusu tu then ile milion 12 aliyokopa itabaki ni yake.

Kumbuka wanao hawatarithi mshshara bali mali ulizoziacha wewe mzazi wao.Ukiuonea mshahara huruma basi ukiondoka ghafla tambua kabisa una uhakika wa kuacha matatizo mengi ya kifedha nyumbani kwako
 
Akili kubwa sana
 
Hizo ni risk ambazo ameshauri Kwa kukopa mwaka mmoja utakufanya ujue wapi umekwama
 
Wakat wa kufanya biashara nyie wenye degree hamjawahi kufaulu wengi wenu, hiyu ku-analyse mapungufu ndo ujinga. Fanya kwamba itakupa biashara mengine utayakuta ndani Ya game.
 
Moja ya komenti bora, ahsante kwa ushauri kaka.
 
Hizo ni risk ambazo ameshauri Kwa kukopa mwaka mmoja utakufanya ujue wapi umekwama
Kwa mshahara wa laki 5 nipe calculation ya mkopo wa mwaka mmoja ukope sh ngapi kisha nikuoneshe kwamba huwezi kutoboa kwa njia hiyo
Kumbuka mshahara wako unapaswa kubaki 1/3 means kopa milion 3.2 hivi kwa makato ya Tsh 333333 ubaki na 166666 mshahara
Hivi unaijua laki na sitini na sita kweli? Na biashara au kitu gani uweke milion 3.2 kikulipe parefu kufidia hiyo laki 3 nzima unayokatwa? Kumbuka 166666 kodi imo humohumo ,msosi na gharama nyingine za maisha ukikumbuka kuwa anything can happen kwenye hako ka pesa na maisha yako so ukichukua ndogo ujue na mambo ni madogo ndiyo maana bank wanakwambia kopa milion nyingi uzungushe zaidi sio ukope pesa ndogo inayokunyima uhuru wa kuizungusha
Kama upo vijijini mil 3.5 inaweza tenda kitu ila kwa kubahatisha sana
 
ACha kujipa umuhimu kwenye maisha ya watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…