Kama Wewe ni Mwana Simba Sports Club 'Mwenzangu' na 'unajiuliza' nini 'Kimeitokea' Timu yetu na sasa 'inafungwa' mfululizo haya ndiyo majibu

Kama Wewe ni Mwana Simba Sports Club 'Mwenzangu' na 'unajiuliza' nini 'Kimeitokea' Timu yetu na sasa 'inafungwa' mfululizo haya ndiyo majibu

1. Posho ya Wachezaji imekuwa ikipunguzwa na kuna muda hawakupewa kabisa isivyo kawaida na Mo Dewji anafichwa
2. Kuna Mgawanyiko mkubwa baina ya Wachezaji hali ambayo imesababisha Chuki na Majungu baina yao
3. Kocha Sven Vandebroek amechokwa kutokana na Misimamo yake ya Kutopangiwa Timu na sasa anachomeshwa afukuzwe
4. Kocha Msaidizi Matola na Kocha wa Makipa Mwarami kuongoza kwa Majungu kwa Kipa Kakolanya kwa Kumpendelea Manula
5. Kuna Wataalam (Waganga) Wawili Mmoja kutoka Kisiwani na mwingine Morogoro wamedhulimiwa Pesa yao japo ilitolewa
6. Hali ya Uchumi sasa Klabuni si nzuri kutokana na 'Mwekezaji' Hela yake nyingi kuitoa Kukisaidia Chama fulani katika Kampeni
7. Usaliti mkubwa baina ya Viongozi 'Waandamizi' wa Klabu kutoka pande zote mbili za Mwekezaji na ule wa Wanachama

Mo Dewji na 'Poti' wangu Magori ambaye ni Mshauri Mkuu wa Mwekezaji ambao wote kwa ujumla najua huwa mnanisoma mno tu GENTAMYCINE hapa Jamvini (JamiiForums) tafadhalini upesi sana 'okoeni' hii hali kwa kuanzia huko 'Uongozini' Kwenu mlipo ila 'ikiwapendeza' upesi sana Vunjeni Benchi lote la Ufundi kwani Kocha Mkuu 'hasikilizwi' na Msaidizi Matola ana 'Majungu' kupitiliza.
Sehemu kubwa hayana mashiko Zaid ya nadharia ya kufikirika na huenda very tactical thinker wanaweza iona ni habari swali inatoka kwa maslahi ya Nani?
 
Kuna mchezaji alikua akizozana na Matola baada ya mechi ya Ruvu kuisha. Hiki hakikukua kiashiria kizuri kwa watani wetu.
 
All Simba has to do is to sweep all Dar es salaam 18 points and the trophy will be their's.
 
Hakuna lolote credict ziende kwa Ruvu na Prisons. Simba imepata ushindi wa tabu Sana na Ihefu Sokoine, ikadroo na mtibwa jamhuri morogoro, ikafungwa na Prisons na Jkt. Simba huwa inapata tabu Sana ikicheza na timu zinatumia mtindo wa "low block" na kukaba kwa nguvu hasa kwenye hivi viwanja vya zamani ambavyo pichi ni vidogo. Kwenye hizi mechi mbili za mwisho kukosekana kwa striker mwenye nguvu kumeiathiri Sana timu kwani ili uweze kuipenya defense ya timu inayocheza mtindo huu lazima striker aweze kuhold Mpira na awe na uwezo wa kugombea mipira ya juu. Vyote hivyo Simba hawakua navyo. Pichi ya Uwanja wa Mkapa ni mkubwa hata timu zikitumia mfumo huu Bado kunakuwa na nafasi kubwa Kati ya wachezaji. Watanzania tujifunze sayansi ya Mpira inatangulia kabla ya siasa ya Mpira. Huwezi kulaumu uongozi katika Jambo linaloonekana wazi kiufundi.
 
Rwemamu na kocha wa makipa wametupiwa virago kisa wapo karibu na Masingisa daaah kuna kitu kinaemdelea pale simba kwa kweli
 
Rwemamu na kocha wa makipa wametupiwa virago kisa wapo karibu na Masingisa daaah kuna kitu kinaemdelea pale simba kwa kweli
Wapo sawa huyo Rweymamu ana majungu sana ndio alikuwa anamuingilia uchebe eti ampangie kikosi, kipa wa makipa hakuwa na vyeti anafundishia uzoefu safi sana
 
Hakuna lolote credict ziende kwa Ruvu na Prisons. Simba imepata ushindi wa tabu Sana na Ihefu Sokoine, ikadroo na mtibwa jamhuri morogoro, ikafungwa na Prisons na Jkt. Simba huwa inapata tabu Sana ikicheza na timu zinatumia mtindo wa "low block" na kukaba kwa nguvu hasa kwenye hivi viwanja vya zamani ambavyo pichi ni vidogo. Kwenye hizi mechi mbili za mwisho kukosekana kwa striker mwenye nguvu kumeiathiri Sana timu kwani ili uweze kuipenya defense ya timu inayocheza mtindo huu lazima striker aweze kuhold Mpira na awe na uwezo wa kugombea mipira ya juu. Vyote hivyo Simba hawakua navyo. Pichi ya Uwanja wa Mkapa ni mkubwa hata timu zikitumia mfumo huu Bado kunakuwa na nafasi kubwa Kati ya wachezaji. Watanzania tujifunze sayansi ya Mpira inatangulia kabla ya siasa ya Mpira. Huwezi kulaumu uongozi katika Jambo linaloonekana wazi kiufundi.
Fafanua hapo ktk pichi ndogo

Vipimo viko sawa sasa iweje?
 
Back
Top Bottom