Kama wewe ni smart na una akili, kwanini hujafanikiwa kuwa Tajiri? Inageukia kwamba wewe ni mjinga

Kama wewe ni smart na una akili, kwanini hujafanikiwa kuwa Tajiri? Inageukia kwamba wewe ni mjinga

Ninakubaliana kwa kiasi kwamba juhudi na mipango ni msingi wa mafanikio yoyote, lakini haimaanishi bahati haina nafasi kabisa.

Bahati inaweza kuwa ni mchanganyiko wa fursa ambazo hazikuundwa moja kwa moja na mtu binafsi lakini zilitokea kwa sababu ya mazingira, wakati, au hali zilizokuwepo.

Mfano wa Bill Gates, pamoja na juhudi zake binafsi, alinufaika na mazingira fulani, kama upatikanaji wa kompyuta katika umri mdogo (ambalo lilikuwa jambo nadra wakati huo), malezi katika familia yenye uwezo wa kumsaidia kufanikisha ndoto zake, na nafasi ya kuwa katika mji wenye sekta ya teknolojia inayokua haraka.

Hii inaonyesha kwamba juhudi peke yake si sababu pekee ya mafanikio—mchanganyiko wa juhudi na mazingira (tunachokiita bahati) mara nyingi huwa na nafasi.

Kwa hiyo, ingawa ni kweli kwamba mali haziji kwa bahati mbaya, nafasi fulani ambazo mtu hakuunda mwenyewe zinaweza kuchangia safari ya mafanikio.

unaona kwamba mazingira yanaweza kuwa na mchango wa kimkakati kwa mtu yeyote.
Uko sahihi kabisa na nakubaliana na wewe.
Chukulia Bill gates angekuwa amezaliwa Mkuranga au Kisemvule unadhani angepata yale mawazo ya kufanya projects kama zile jibu ni hapana,angeishia tu kuwa mchoma mkaa.
 
Kubadikisha akili kuwa mali ni kazi kubwa mno chief - na ndiyo maana unashangaa kukuta Prof ni chawa.
Maana yake pia kuwa Prof inawezekana pia ukawa huna akili! But akili ni nini? Ni sawa na maarifa?
 
Na hakuna Siri kwa tajiri yaan tajiri hana Siri, pigia mstari msipumbazwe na maneno ya kuokoteza matajiri hawana siri wana Wasiri na hao wasiri ndio wanaowatunzia Siri, tajiri hana Siri bali anao watu wanaomtunzia Siri
Tumia akili wewe hamna Siri ya watu wawili duniani
 
Na wewe umeamini hayo? Bahati ni imani tu.

bahati siyo imani, bali ni sehemu ya fursa tulizozikuta na zinazojitokeza mbele yetu bila ya mpango wa moja kwa moja.

"Mafanikio yako maishani hayatategemea tu uwezo na mafunzo, bali pia inategemea uamuzi wako wa kushika bahati zinazokuja na kuzigeuza kuwa fursa." -Yogananda
 
Hii inamaanisha kuwa mafanikio hayategemei tu akili au maarifa, bali pia ni matokeo ya jinsi tunavyoweza kuchangia au kuhusika katika mazingira yanayotoa fursa.

Hivyo, iko wazi kuwa mafanikio ya kifedha mara nyingi ni matokeo ya mchanganyiko wa talanta, juhudi, lakini pia ni matokeo ya fursa, wakati, na hata mazingira ya kijamii.

Kama unajiuliza kwanini haujafanikiwa kuwa tajiri licha ya kuwa na akili, inaweza kuwa kwamba hujapata nafasi nzuri au umekosa sehemu muhimu ya bahati inayohitajika kufanikiwa.

Je, unakubaliana kuwa bahati na mazingira vina nafasi kubwa kwenye mafanikio?
Wenye akili hawajali pesa bali pesa huwajali wao
 
Ni ujinga huwezi Lima kwa kutegemea mvua.
Na endapo utapata Basi itakuwa kwa bahati.
Nchi hii inalishwa kwa kilimo cha mvua.Unaweza kuniambia wapi kuna hekta za mahindi walau 500 zinamwagiliwa ?
Hivi huko Arusha, Shinyanga, Dom nk kuna mito na maziwa ya kumwagilia mashamba ? Nahisi umri wako ni wale 2anwopevuka au kubalehe. Kama una age walau 35+ huwezi toa comment ya hivyo. Siwezi endelea jadiliana na mtu asie na experience ya maisha halisi bali ya kijifurahisha.
Umwagiliaji ni hadithi inayosimuliwa TZ, haina uhalisia wowote.
 
Tukio la kwanza halina maana kwamba mahindi umelima na ukafanikiwa kuuza pekeyako soko nzima, japo wengi wamekosa lakini lipo kundi lililopata. Je hao wote waliopata wana bahati inayo fanana?
Hayo ni matokeo ya hali ya hewa tu.

Misimu ya mvua pia haiji kwa bahati mbaya, wapo wanaoweza kufanya climate forecasting na wakajua kama mvua kubwa zinafata hivyo wakapunguza kipimo cha uzalishaji

HAPO HAKUNA BAHATI, NI MATOKEO YA MABADILIKO YA HALI YA HEWA NA ASILI KWA UJUMLA.
Kalime basi kwa kufuata hizo forecast Unakuwaje unatabiri wakati hali ya hewa yenyewe inabafirika .Labda nikwambie tu kuna mikoa ina mvua miaka yote na mingine hali ya mvua inatabirika.
Hio hio mvua ikizidi ni janga na wengine hawapati tena mnaweza kuwa zone moja.
Wazungu wenyewe na elimu zao bado wameweka "FIDIA YA HASARA ZISIZOTABIRIKA"
Kwa hio nyie ndio mnajua kucheza na weather forecast eti.
Mie sie mtoto wa kunidanganya, ukubwa dawa. Kuishi kwingi kuona mengi. Elimu zamajira nazo ni utabiri mda mwingi e ni tofauti na wanavyotabiri.Hivyo hakuna assurance bali mna fantasize your opinions.
 
Nchi hii inalishwa kwa kilimo cha mvua.Unaweza kuniambia wapi kuna hekta za mahindi walau 500 zinamwagiliwa ?
Hivi huko Arusha, Shinyanga, Dom nk kuna mito na maziwa ya kumwagilia mashamba ? Nahisi umri wako ni wale 2anwopevuka au kubalehe. Kama una age walau 35+ huwezi toa comment ya hivyo. Siwezi endelea jadiliana na mtu asie na experience ya maisha halisi bali ya kijifurahisha.
Umwagiliaji ni hadithi inayosimuliwa TZ, haina uhalisia wowote.
Tanganyika, tunaeleweshana ndugu. Ni Mimi kwa upande wangu ambaye siwezi fanya kilimo kwa kutegemea mvua huwa sipendi coz inakuwa Ni Kama bahati kupata mazao niliyoyakusudia lkn pia hata kwa watu wengine wangeweza niwazavyo nadhani wangefaidika na kupunguza vilio vya ukame.

Shida kubwa Ni umasikini tu unamsumbua lkn maji yapo tu yakutosha. Hata chini ya ardhi Kuna maji mengi. Vile vile usiseme kwamba umwagiliaji hauna mantiki nchini hasha unasaidia vibaya mno. We fikiria kiangazi watu tunakula mchicha, nyanya, vitunguu makabeji nk. Kwa umwagiliaji tu. Hata mahindi pia.

Kilimo Cha kutegemea mvua kinaweza kuwa na tija tu pale ambapo uwezo wa kiuchumi kwa mkulima bado Ni duni.
 
We fikiria kiangazi watu tunakula mchicha, nyanya, vitunguu makabeji nk. Kwa umwagiliaji tu. Hata mahindi pia
Sawa .
Ila Maheka ya Mahindi na mounga yanategemea mvua au mixer. ndio maana tukaweka neno bahati ktk uasili sio ktk utaalamu. Kuna ndugu yangu alimwgiilia shamba lake mwaka juzi mazao yalipokomaa masai wakalisha usiku. Sasa hapo utasemaje ? Ukizingatia jamaa ndio alikuwa anajitafuta hata hhawzi kuweka walinzi masaa yote.
Tujadili ktk hali halisi ya mtanzania na mwafrika. Tunakumbana na changamoto nyu gi sana hata kama una akoli kama mchwa bado bahati ina bafasi yake.
Unakumbika stoti ta Sumri ba mshindi yake yalioyoda soko ?
 
Bahati sikatai ipo. Lakini wanapotupiga gep matajiri Ni pale tunapodharau Yale ya msingi yanayotuvuta kwenye umasikini.

Bado hujapambana na changamoto ya kilimo Cha kutegemea mvua na Wala haikufanyi kuwaza! Wakati mwenzio kwake kuvuna Ni lazima apate labda changamoto iwe masoko hata hivyo ikitokea Bei imeshuka anahifadhi nakuuza kipindi Bei inapopanda maradufu, hapohapo anapata na bahati mafuriko yanatokea anapata tenda yakuuzia serikali mazao yake kwa Bei ya kuringa hahaha!
Kuna jamaa mmoja alikuwa fundi pikipiki maeneo ya katikati ya soko Sasa sijui pango lilimshinda, ikambidi kuhamia karibu na kituo Cha polisi akiendelea na ufundi wake. Lakini wateja wakawa wakutafuta kweli. Tukawa tunamkuta usiku saa sita anaoga dawa kila siku. Jamaa yangu mmoja akaniambia huyu fundi ujinga unamsumbua, wateja wanashindwa kuja wakihofia polisi watawakamata kwa kutovaa helmet na makosa mengine lkn yeye ndo kwanza anaoga dawa. Hahahaha. Basi alifanya ufundi matokeo yake alishindwa.
 
Hii inamaanisha kuwa mafanikio hayategemei tu akili au maarifa, bali pia ni matokeo ya jinsi tunavyoweza kuchangia au kuhusika katika mazingira yanayotoa fursa.

Hivyo, iko wazi kuwa mafanikio ya kifedha mara nyingi ni matokeo ya mchanganyiko wa talanta, juhudi, lakini pia ni matokeo ya fursa, wakati, na hata mazingira ya kijamii.

Kama unajiuliza kwanini haujafanikiwa kuwa tajiri licha ya kuwa na akili, inaweza kuwa kwamba hujapata nafasi nzuri au umekosa sehemu muhimu ya bahati inayohitajika kufanikiwa.

Je, unakubaliana kuwa bahati na mazingira vina nafasi kubwa kwenye mafanikio?
mafanikio ya kifedha hayatafutwi yanakuaga kama bonus kwa unachofanya
 
Yes.
Mtu aliyefanikiwa rohoni huyo ndiye kafanikiwa.
Huwezi kufanikiwa rohoni, alafu mwilini uwe kapuku, acheni kutafsiri mambo ndivyo sivyo, hii dhana ya kuaminisha watu kuwa utajiri unaanzia rohoni, ililetwa na wakoloni ili kuwaaminisha waafrika kuwa umasikini ni mzuri na walidhike na hali zao uku wakifarijiwa na mafundisho ya dini yanayotafsiriwa isivyotakiwa.

Utajiri ni ukamilisho wa mafanikio ya Rohoni, nafsini, akilini na mwili kiujumla, huwezi kufanikiwa sehemu Moja tu.

Huwezi kusema umefanikiwa kwa kumiliki wazo la utajiri ambalo lipo akilini mwako na hujalitendea kazi mwilini na likaleta matokeo chanya, hayo sio mafanikio huo ni umiliki tu wa mawazo ya mafanikio.

Iyo dhana ya kufanikiwa rohoni pekee Ingekuwa hivyo mnavyotafsiri basi Africa kiujumla ingekuwa tajiri kuliko mahala popote maana ndiyo sehemu pekee hapa dunian watu wanakufa wakiwa na lundo la ndoto/maono yao ambayo hawajayatimiza na kweli kama yangefanyiwa kazi yangeleta matokeo chanya, Sasa kwa mifano hii utaweza kusema Watu hao wa afrika wamefanikiwa Kisa kumiliki mawazo ya mafanikio?

Mafanikio ni jumla ya mawazo, uthubutu na matokeo chanya, kikipungua hata kitu kimoja hapo, hayo sio mafanikio Bali ni mawazo ya mafanikio ambayo si mafanikio Bali njia ya kubashiri mafanikio.
 
Labda nijaribu kujibu, una akili ila sio tajiri! Hakika utajiri mara nyingi ni kuthubutu, "mwenye akili anaogopa kuthubutu " anatumia akili yake katika kuamua mambo yake, mwenye akili anatambua roho ya mtu ni kitu chenye thamani ila asiye na akili hatambui hilo, kwake yeye "find money by any means "
 
Bado hujapambana na changamoto ya kilimo Cha kutegemea mvua na Wala haikufanyi kuwaza!
Chukulia mazingira ambayo wote mnategemea mvua lakini mmoja anatajrika meingine hatajiriki. Halafu kaa ujue sio kila mahala hapa Tanzania hakuna mvua. Njombe, Mbeya, Songea nk hakunaga ukame. Naona unawaza sana mwelekeo wa kumwagiliia.
Kilimo cha kumwagilia asilimia kubwa ni bustani au mazao ya kudumu kama miwa, chai.
Hao matajiri wengi wa kilimo unao waona hawajatajirika na kilimo chakumwagilia. Kule unangu umwagiiliaji ni ziada ila wanategemea mvua.
Bro usijikite sana kwenye kilimo makaratasi, kilmo kinachoendesha nchi hii ni kilimo mvua.
Vilevile watu wengi breaking point ya poverty wanaanza na kilimo cha asili na wanategemea mvua ambayo ni bahati. Mtu nwenye mipango ya umwagiliaji ashavuka kutegemea bahati, ashatoboa usimjadili sana. Muangalie yule mtu anatafuta pa kutokea nadhani ndio lengo la uzi.
 
Ingekuwa yangu nchi hii ningeweka system ya mabomba ya maji nchi nzima then nikafuta bili ya maji ili kila anayepigwa na maisha kimbilio liwe kilimo. Alafu tuone Ni mpuuzi gani analia njaa.

Asilimia kubwa nchi yetu Ni asili ya joto mbali na maeneo yenye athari za tabia ya nchi Kama mikoa uliotaja, so ukame upo tu usibishe alafu wajanja hata mihogo inamwagiliwa brother.
Sasa tukichukulia mtu ambaye anaanza kujitafuta Ni lazima awe na mipango thabit yakufikia zana za kisasa. Kwa upande wangu Mimi nikizungumzia bahati huwa naiweka upande wakiimani kabisa, Mungu mwenyewe anahusika Sasa kawaida ya Mungu huwa anahusika kwa wajinga na sio kwa wapumbavu ndo sababu Babu zetu wametukuza kwa kilimo hichohicho chakupiga ramli. Lkn unapofikia hatua ya kujitambua halafu umekaza fuvu utabaki na fuvu lako.
 
Hii inamaanisha kuwa mafanikio hayategemei tu akili au maarifa, bali pia ni matokeo ya jinsi tunavyoweza kuchangia au kuhusika katika mazingira yanayotoa fursa.

Hivyo, iko wazi kuwa mafanikio ya kifedha mara nyingi ni matokeo ya mchanganyiko wa talanta, juhudi, lakini pia ni matokeo ya fursa, wakati, na hata mazingira ya kijamii.

Kama unajiuliza kwanini haujafanikiwa kuwa tajiri licha ya kuwa na akili, inaweza kuwa kwamba hujapata nafasi nzuri au umekosa sehemu muhimu ya bahati inayohitajika kufanikiwa.

Je, unakubaliana kuwa bahati na mazingira vina nafasi kubwa kwenye mafanikio?
In society we have normal and smart people

Ufafanuzi mtu smart ni mtu mwenye akili, normal wa kawaida kama mimi
 
Back
Top Bottom