Unaweza kusemaaliyekwenda kurusha mabomu Syria si Mungu, kwa sababu Mungu hayupo.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye utakatifu wote, uwezo wote, upendo wote, angekuwepo, palemwanzo kabisa alipokuwa anaamua kuuumba ulimwengu (kabla shetani, watu, ulimwenguhavijakuwapo) asingejiruhusu kuumba ulimwengu ambao watu wanawezakurushiana mabomu,watoto wachanga wanakufa kwa kufukiwa na kifusi kinachotokana na tetemekokubwa laardhi etc etc.
Ulimwengu huu tunaouona ambao maovu mengi yanaweza kutokea unapingana moja kwa moja na sifa za huyo Mungu mnayemsema yupo.
Kuwepo kwa Mungu huyo, halafu akaumba ulimwengu huu tunaouona ni sawasawa na kuwapo kwa "pembe tatu yenye pembe sita", pembe tatu hiyo yenye pembe sita haiwezi kuwepo kiuhalisia kwa sababu ileile ambayo Mungu huyo hawezi kuwepokiuhalisia.
Logical consistency. Contradiction.
Pembe tatu hiyo yenye pembe sita haina logical consistency.Dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe.Ina contradiction.
Vivyo hivyo.
Mungu huyo dhana ya kuwepo kwake haina logical consistency. Dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe.Ina contradiction.
Mungu huyu ni hadithi za kuliwaza moyo na kuwarudisha watu kwenye mstari na kuwa control watu tu, lakini kiuhalisia hawezi kuwepo.