Kama wewe upo kwenye makundi haya halafu unakidharau na kukikashifu CCM tarajia laana kukuandama katika maisha yako

Usisahau mikopo inarudishwa. Kila siku watu wankabwa makazini.
Inarudishwa ndiyo ila tushukuru!wangapi tungeweza kumudu hizo gharama!!tumefika point ya kukatwa hiyo mikopo makazini kwa sababu serikali ya ccm ilichukua jukumu la wazazi wetu kutusomesha hivyo tukishukuru chama cha mapinduzi
 
Kodi ndiyo hizo zinarudi kuwapa wajasiamali mikopo isiyo na riba hivyo inabidi wawe na heshima kwa ccm

Serikali inawatumikia wananchi. Ndio maana kila baada ya miaka mitano wanakuja kuomba kura kwa wananchi
 
Mzazi ni mdhamini Kama hujui. Kwa hivyo mwanafunzi asipolipa mzazi wake atadaiwa.
Mzazi gani kashawahi kudaiwa kisa mtoto wake kashindwa kulipa mkopo?wanafaika wangap wanafariki kila siku wakati wanadaiwa umeshawahi kusikia ndugu zao wanadaiwa?tuwe na shukrani jamani
 
Inarudishwa ndiyo ila tushukuru!wangapi tungeweza kumudu hizo gharama!!tumefika point ya kukatwa hiyo mikopo makazini kwa sababu serikali ya ccm ilichukua jukumu la wazazi wetu kutusomesha hivyo tukishukuru chama cha mapinduzi

Wengi hawapati hiyo mikopo. Ni wachache wanapata kwa Asilimia mia. Ila ujue hiyo ndio kazi ya Serikali Sio hisani. Serikali ipo kuwatumikia wananchi na Sio wananchi kuitumikia.
 
Serikali inawatumikia wananchi. Ndio maana kila baada ya miaka mitano wanakuja kuomba kura kwa wananchi
Ndiyo kweli kabisa basi tuipongeze kwa jinsi inavyotumikia wananchi vizuri siyo kila siku matusi tu
 
Mzazi gani kashawahi kudaiwa kisa mtoto wake kashindwa kulipa mkopo?wanafaika wangap wanafariki kila siku wakati wanadaiwa umeshawahi kusikia ndugu zao wanadaiwa?tuwe na shukrani jamani

Shukrani kwenye mkopo?. Basi tushukuru na mabenki au kausha damu wanaokopeshwa. Wapinzani walikuja na slogan ya elimu Bure kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu. Ndipo CCM wakaiga.
 
Ndiyo kweli kabisa basi tuipongeze kwa jinsi inavyotumikia wananchi vizuri siyo kila siku matusi tu

Tofautisha matusi na maoni kinzani. Pia Saa zingine boss akikasirika anaweza kukutukana.
 
Wengi hawapati hiyo mikopo. Ni wachache wanapata kwa Asilimia mia. Ila ujue hiyo ndio kazi ya Serikali Sio hisani. Serikali ipo kuwatumikia wananchi na Sio wananchi kuitumikia.
Utaki kukubali ukweli tu tatizo serikali ya ccm ina upendo mpaka tunaipa majukumu ya wazazi wetu,na yenyewe inakubali,kazi ya serikali ni kuweka miundombinu wezeshi ya wewe kusoma,kazi ya kukusomesha ni ya wazazi wako,serikali ya ccm ina upendo mno tuishukuru
 
Shukrani kwenye mkopo?. Basi tushukuru na mabenki au kausha damu wanaokopeshwa. Wapinzani walikuja na slogan ya elimu Bure kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu. Ndipo CCM wakaiga.
Kuiga jambo jema siyo kitu kibaya
 
Ccm wakubali tu kuwa zama zao zimekwisha, wanapolazimisha kutawala bila ridhaa ya wananchi wanajitakia matusi yasiyo ya lazima. Na kwa jinsi ccm inavyoshurutisha kukaa madarakani, siku ikitoka madarakani ndio kwaheri.
 
Dua la kuku,karibu chama cha mapinduzi, chama la ushindi
 
Kama kuna siku nimeona uzi wenye pumba nyingi ni huu,
Nasisitiza hakuna akili iliyotumika kuandika bandiko hili,
Zaidi umetumia hisia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…