Kama wewe upo kwenye makundi haya halafu unakidharau na kukikashifu CCM tarajia laana kukuandama katika maisha yako

Kama wewe upo kwenye makundi haya halafu unakidharau na kukikashifu CCM tarajia laana kukuandama katika maisha yako

Usisahau mikopo inarudishwa. Kila siku watu wankabwa makazini.
Inarudishwa ndiyo ila tushukuru!wangapi tungeweza kumudu hizo gharama!!tumefika point ya kukatwa hiyo mikopo makazini kwa sababu serikali ya ccm ilichukua jukumu la wazazi wetu kutusomesha hivyo tukishukuru chama cha mapinduzi
 
Kodi ndiyo hizo zinarudi kuwapa wajasiamali mikopo isiyo na riba hivyo inabidi wawe na heshima kwa ccm

Serikali inawatumikia wananchi. Ndio maana kila baada ya miaka mitano wanakuja kuomba kura kwa wananchi
 
Mzazi ni mdhamini Kama hujui. Kwa hivyo mwanafunzi asipolipa mzazi wake atadaiwa.
Mzazi gani kashawahi kudaiwa kisa mtoto wake kashindwa kulipa mkopo?wanafaika wangap wanafariki kila siku wakati wanadaiwa umeshawahi kusikia ndugu zao wanadaiwa?tuwe na shukrani jamani
 
Inarudishwa ndiyo ila tushukuru!wangapi tungeweza kumudu hizo gharama!!tumefika point ya kukatwa hiyo mikopo makazini kwa sababu serikali ya ccm ilichukua jukumu la wazazi wetu kutusomesha hivyo tukishukuru chama cha mapinduzi

Wengi hawapati hiyo mikopo. Ni wachache wanapata kwa Asilimia mia. Ila ujue hiyo ndio kazi ya Serikali Sio hisani. Serikali ipo kuwatumikia wananchi na Sio wananchi kuitumikia.
 
Serikali inawatumikia wananchi. Ndio maana kila baada ya miaka mitano wanakuja kuomba kura kwa wananchi
Ndiyo kweli kabisa basi tuipongeze kwa jinsi inavyotumikia wananchi vizuri siyo kila siku matusi tu
 
Mzazi gani kashawahi kudaiwa kisa mtoto wake kashindwa kulipa mkopo?wanafaika wangap wanafariki kila siku wakati wanadaiwa umeshawahi kusikia ndugu zao wanadaiwa?tuwe na shukrani jamani

Shukrani kwenye mkopo?. Basi tushukuru na mabenki au kausha damu wanaokopeshwa. Wapinzani walikuja na slogan ya elimu Bure kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu. Ndipo CCM wakaiga.
 
Ndiyo kweli kabisa basi tuipongeze kwa jinsi inavyotumikia wananchi vizuri siyo kila siku matusi tu

Tofautisha matusi na maoni kinzani. Pia Saa zingine boss akikasirika anaweza kukutukana.
 
Wengi hawapati hiyo mikopo. Ni wachache wanapata kwa Asilimia mia. Ila ujue hiyo ndio kazi ya Serikali Sio hisani. Serikali ipo kuwatumikia wananchi na Sio wananchi kuitumikia.
Utaki kukubali ukweli tu tatizo serikali ya ccm ina upendo mpaka tunaipa majukumu ya wazazi wetu,na yenyewe inakubali,kazi ya serikali ni kuweka miundombinu wezeshi ya wewe kusoma,kazi ya kukusomesha ni ya wazazi wako,serikali ya ccm ina upendo mno tuishukuru
 
Shukrani kwenye mkopo?. Basi tushukuru na mabenki au kausha damu wanaokopeshwa. Wapinzani walikuja na slogan ya elimu Bure kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu. Ndipo CCM wakaiga.
Kuiga jambo jema siyo kitu kibaya
 
1. Kundi la watu wote ambao hawakuweza kumudu gharama za masomo ya elimu juu,serikali ya chama cha mapinduzi ikachukua jukumu la kuwasomesha tena kwa kutumia gharama kubwa,leo mnatumia usomi wenu kukitukana chama cha mapinduzi, nawaambia laana ipo malangoni mwenu,tubuni Mungu hapendi watu wasiokuwa na shukrani.

2. Kundi la watu wote ambao wamekuta babu zao,wazazi wao wakiwa na itikadi ya chama cha mapinduzi wakalelewa katika maadili mema ya chama cha mapinduzi ,walivyokuwa wakakengeuka na kuanza kuleta itikadi ngeni kwenye ukoo,kundi hili nalionea huruma sana,hakuna laana mbaya kama laana ya kutowatii wazazi,hamjachelewa tubuni.

3. Kundi la wazazi ambao watoto wao wanasoma bure katika shule za serikali hawalipii chochote zaidi ya madaftari ,viatu,na hela ya mtoto ya kula miogo na bado wanapata kiburi cha kukitukana chama cha mapinduzi,nawaambia hawa watoto ni malaika na chama cha mapinduzi kimeamua kuwekeza kwa malaika,uwekezaji huu kwa malaika hautawaacha salama wazazi hawa wasiokuwa na shukrani,tubuni.

4.Kundi la wajasiriamali waliokopeshwa mikopo isiyo na riba na serikali ya chama cha mapinduzi halafu kila kukicha wanashinda mitandaoni kukitukana na chama cha mapinduzi hakika Mungu ataiona sadaka ya chama cha mapinduzi na hatonyamaza,muda bado mnao tubuni kabla laana ijawapata.

5. Kundi la watu ambao mnashinda mitandaoni,kumtukana na kumkashifu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ambae pia ni kiongozi wenu tena mnamtukana kwa mambo ambayo hamna huakika wa uthibitisho,nyie pia hamjachelewa tubuni,kumtukana kiongozi aliyewekwa na Mungu ni kumdharau Mungu.
KATAA LAANA
Ccm wakubali tu kuwa zama zao zimekwisha, wanapolazimisha kutawala bila ridhaa ya wananchi wanajitakia matusi yasiyo ya lazima. Na kwa jinsi ccm inavyoshurutisha kukaa madarakani, siku ikitoka madarakani ndio kwaheri.
 
Dua la kuku,karibu chama cha mapinduzi, chama la ushindi
 
Kama kuna siku nimeona uzi wenye pumba nyingi ni huu,
Nasisitiza hakuna akili iliyotumika kuandika bandiko hili,
Zaidi umetumia hisia
 
Back
Top Bottom