Kama Yanga watajenga Uwanja hapo Jangwani basi Mo Dewji hastahili kuendelea kuwepo Simba



Hastahili kuwepo kwenye mali aliyonunua?
 
Tukuamini wewe au Engineer aliyeaminiwa na Engineer???
kwani Engineer ni Nani mzee Ata kituo cha mwendokasi wakati kinajegwa pale ao ao Ma Engineer Ndio walitoa izini kwamba wajenge tu hapana shida ila umeona balaa ambalo lilikua linawakuta hadi wakaamua kuamia Ubungo
 
Hastaili kuendelea vipi wakati timu ni Mali yake na familia yake? Wewe vipi hujui kitu gani? Au unamiliki asilimia ngapi ya hisa za clabu . Mwache afanye awezavyo na timu yake
 
Hizo ni porojo na siasa tu kwa timu za Simba na Yanga haziwezi kuwa na Viwanja kama Azam kwa sababu zile ni timu za Serikali, Sasa vikije ga Viwanja pale kwa Mkapa unataka pageuke kama ule Uwanja wa ndege kule CHATO ?
Utajuaje labda serikali imeamua kuijengea uwanja Yanga
 
Simba tumheshimu MO Dewji sana sana.

Alijitolea pesa yake kuiboresha Simba peke yake, hadi imekuwa Club ya 5 Bora Afrika.

Yanga wana Matajiri wengi sana kama GSM, Rostam, Riz-wan, Manji, na Matajiri wengine wanao jisogeza CCM kwa maslahi Yao.

Ndio maana Wana wachezi wazuri kutokana na kuweka pesa nyingi.

Waacheni Yanga waende sisi tusubiri muda na wakati wetu.

Ni vema sasa huyo CEO wa Simba atumie muda wake kuwatafuta Matajiri wengine wenye nia ya kuwekeza Simba.
Badala ya kuzurula zurula tu OFISINI.
 
watu kama nyie ndio mnasababisha simba imegota sehemu na haisongi mbele tena
 
Hastaili kuendelea vipi wakati timu ni Mali yake na familia yake? Wewe vipi hujui kitu gani? Au unamiliki asilimia ngapi ya hisa za clabu . Mwache afanye awezavyo na timu yake
Simba ni mali ya wanachama, huyo Mo Dewji anapaswa apimwe kama alikuwa ametumia kilevi wakati anatoa ile kauli ya kununua simba
 
watu kama nyie ndio mnasababisha simba imegota sehemu na haisongi mbele tena
Kwanini hebu fafanua.
Wapi nimesema sivyo?
Hujaeleweka.
Simba imegota wapi ilhali kila mwaka inaingia robo fainali Club-Bingwa Afrika.
Yanga ndio inaingia baada ya miaka 25.
Sema imegota wapi?
 
Tutaona Mkuu, hilo halitatokea hapa Tanzania na kuelekea Afcon 2027 Viwanja vyenye hadhi ya CAF vitakavyokuwa vinamilikiwa na CAF vitakuwa vingi tu.
Weka akiba ya maneno.
 
Kwanini hebu fafanua.
Wapi nimesema sivyo?
Hujaeleweka.
Mo Dewji ndiye anayekwamisha hao matajiri wengine wasije kuwekeza Simba, amehodhi madaraka yote kiasi hata mwenyekiti wa wanachama ndugu Mangungu anafata matakwa yake.
Kabla ya kuja Simba unadhani Mo Dewj alikuwa na utajiri kiasi gani? Baada ya kuja Simba amekuwa tajili no moja Tanzania na miongoni mwa Matajili wakubwa Afrika kwa sasa.
Simba ndio imemtangaza na kumkuza kibiashara na amekuwa akitangaza bidhaa zake kupitia Simba kwa gharama karibu na bure.
Mo Dewji hana nia ya dhati Simba isonge mbele ndio maana huoni akiwekeza kwny project zitakazoacha alama kwa klabu.
 
Acha uongo,Mo ni tajiri hata kabla ya kuwekeza Simba,kwa mujibu wa Forbes mwaka 2015 Mo alikuwa tajiri no moja,hiyo ni kabla ya kuwekeza Simba.Mo ana madhaifu yake lakini kuhusu utajiri amewazidi mbali sana wale jamaa wa magodoro.
 

Attachments

  • Screenshot_20240317-021614.png
    357.6 KB · Views: 4
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…