Kama Yanga watajenga Uwanja hapo Jangwani basi Mo Dewji hastahili kuendelea kuwepo Simba

Hao Matajiri walikuwa wapi wakati Simba ikitembeza Bakuli na Yanga ikipepea na tajiri Manji ?

Hata baada ya Manji tajiri gani mwingine alijitokeza kuwekeza Simba ?

Au hata Leo tajiri gani amekatazwa kuwekeza Simba ?
Ameonyesha hiyo nia lini wakati Simba ilitangaza anaye taka kuwekeza hadharani na hakuna aliyejitokeza zaidi ya MO Dewji.
 
Yanga inamatajiri wengi kama nilivyosema hapo juu ndio maana inachukua wachezaji wazuri kuzidi Simba.

Simba walianza kimtaka KI AZIZI Yanga wakamchukua.
Simba alianza kimtaka Aucho Yanga wakamchukua.

Naskia hata Pakome na Nzengeli Simba ilionesha nia ya kuwachukua Yanga ikawabeba.

Hiyo yote inatokana na kuwepo Matajiri wengi hapo Yanga hivyo wanawachukua wachezaji wazuri bila kujiuliuliza.

Simba kwa sasa haiwezi kugombea mchezaji na Yanga. Yanga wanamchukua mapema tu.
Kwakuwa kuna Matajiri wengi wanashirikiana.

MO yupo yeye tu, hivyo hata skauti ya wachezaji muhimu inafeli. Wanachukuliwa akina Freddy wa kucheza miezi sita tu.
 
Kuna kama wana simba hatutakiwi laumu kama mentor wetu ni Mangungu..
Na huku mtandaoni vila.za kama genta
 
Tatizo la Simba janja janja zimekuwa nyingi sana kuanzia mwekezaj mpaka viongozi wa chini yake,mara Mo arena mara bunju hata hawaelewiki mwisho wa siku Wanatuletea akina jobe na fredy na Sasa hvi wanaona mechi yao ya robo finali itakuwa rahis sna kupita Ile ya wapinzani wao Mpaka mtu unajiuliza ni timu ipi hapa ya kuitoa Al ahly
 
Kwa hiyo mnaamini mtajengewa uwanja 3 years ago mlionyeshwa hadi eneo la kujenga uwanja Kigamboni.

"Tuliweka wazi ili makampuniyanayoona yanaweza kufanya kazihiyo yajitokeze lakini mpaka sasa nimakampuni 10 yaliyoonyesha niahiyo.

“Tutamtangaza wazi ambayeatakuwa amepata hiyo tenda tayarikwa kuanza majukumuhayo,'alisema Mfikirwa.
 
Kwani huyo Mo wenu si ameshajenga uwanja kule Bunju na kuuita Bunju Mo Arena!! Mumshawishi auzungushie uzio na pia kuujengea majukwaa. Siyo anaendeleza tu ile tabia yake ya ujanja ujanja.
 
Viongozi wa Yanga wasipoitimiza hii ahadi yao ya kujenga uwanja (Iwe Kigamboni au Jangwani), hakika nitakuwa mstari wa mbele kuwakosoa waziwazi humu jukwaani kutokana na kushindwa kuitimiza hii ahadi yao.

Maana ni upuuzi na pia ni uwendawazimu! Yaani timu za juzi tu kama Azam Namungo, Gwambina, JKT Tanzania, Mtibwa sugar, nk zina viwanja vyao binafsi kwa ajili ya mechi na mazoezi! Halafu Yanga yenye miaka zaidi ya 80 tangu ilipoanzishwa; mpaka leo haina uwanja wake binafsi! Na badala yake uwanja wa Taifa ukifungwa kwa matengenezo, wanaenda kukodi uwanja wa Azam Complex!
 
kwa mtu anayepafamu jangwani vizuri hawezi kujenga uwanja sehemu ya ovyo kama ile Njia tu za kuingila na kutoka jangwani mara nyingi huwa zinafunga had mwendokasi za kimara kuna kipind zinazunguka ilala boma
Kwa hiyo Kwa akili yako unaamini Jangwani hapawezekani kujengwa chochote? Wewe ni Injinia wa fani gani Mkuu?
 
Tutaona Mkuu, hilo halitatokea hapa Tanzania na kuelekea Afcon 2027 Viwanja vyenye hadhi ya CAF vitakavyokuwa vinamilikiwa na CAF vitakuwa vingi tu.
CAF haijengi viwanja na kuvimiliki kwenye nchi zinazo fanyika AFCON.
Vinajengwa na nchi husika na hapa Tanzania ndiyo hivyo ulivyo sikia Raisi anajenga viwanja vipya kadhaa kimojawapo kilichotangazwa kujengwa Arusha.
 
Mimi nilichangia milioni 20 ya ujenzi wa uwanja alafu uongozi ukaja ukasema fedha zilizochangwq zimetumika kujengea ukuta!
 
kwa mtu anayepafamu jangwani vizuri hawezi kujenga uwanja sehemu ya ovyo kama ile Njia tu za kuingila na kutoka jangwani mara nyingi huwa zinafunga had mwendokasi za kimara kuna kipind zinazunguka ilala boma
Kuna mradi wa serikali unakuja unaenda kuibadili bonde lote la mto msimbazi
 
Sasa kama Mo ni tajiri number 1 anashindwa nini na hao wauza magodoro
 
Anataka zirudi kwanza pesa slizowekeza Simba, zikirudi hapa shaka ataanza kuujenga uwanja,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…