Kamanda kova afichua siri ya mabenki kuvamiwa asema,dharau za wamiliki wa benki ndio tatizo..

Kamanda kova afichua siri ya mabenki kuvamiwa asema,dharau za wamiliki wa benki ndio tatizo..

Mandla Jr.

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Posts
3,098
Reaction score
631
JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam limefichua Siri ya kuongezeka Vitendo vya ujambazi katika maBenki mbalimbali hapa nchini na kusema vitendo hivyo vinasababishwa na Wamiliki wa Mabenki hayo kulipuuza Jeshi la polisi,Kauli hiyo ya Jeshi la polisi Kanda ya Dar es Salaam imekuja SIKU moja kupita baada ya watu wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi kuvamia katika Benki ya Stanbic tawi la Kariakoo liloko mtaa wa Swahili na kukomba mamilioni ya pesa aliyokuwa nayo Mteja, Kauli hiyo imetolewa Mda huu na Kamishna wa Polisi kanda Maalum Dar Es Salaam,Suleiman Kova wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam,ambapo alisema watu wanaochangia Vitendo hivyo vya Ujambazi kuzidi kuongezeka katika Mabenki mbalimbali hapa nchini ni Wamiliki wa Mabenki kupuuza ushauri wa Jeshi la Polisi ,

Uliowataka waache kutumia walinzi wa Makampuni Binafsi peke yake,watumia na Walinzi kutoka Jeshi la polisi.
“Nataka niwambie waandishi hivi vitendo vya Uvamizi kwenye mabenki viemtokana na wamiliki wamabenki hayo kupuuza ushauri wetu uliowataka kwenyes shuhuri za Ulinzi kwenye mabenki watumike Polisi tu,lakini wao wakapuuza,ukitaka kuamini Nenda kwenye Mabenki yanayolindwa na Polisi kama utaona kama kunauvamini wowote uonotokea,kwasababu majambazi hao wanashindwa kuvamia kutokana na umakini wa Jeshi la Polisi”alisema Kova
Kamishna Kova,alisema kwa sasa Jeshi la polisi limejipanga kuongea na Benki kuu(BOT) ambaye ni kiongozi wa Benki zote hapa nchini na kutafuta ufumbuzi wa hili tatizo la Mabenki Mengine kupuuza ushauri huo wa Jeshi la polisi.
Vilevile jeshi hilo la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Limeeanza msako kali wa kuwatafuta Majambazi watano waliovamia Jana kwenye Beki ya Stabinc Tawi la Kariakoo lilioko mtaa wa Shwahili majira ya mchana.
Kwa Mujibu wa Kamishna Kova alisema watu wa tatu kati yao waliingia ndani ya Benki hiyo wakiwa na Mifuko Mikubwa wakijifanya ni wateja wanapeleka Fedha nyingi katika Benki hiyo,watu hao walipoingia ndani walianza kuwalazimisha kuvuka wigo wa wateja wa kwaida na kutaka kuingia kwa nguvu kupora Fedha.
Ambapo Benki hiyo ya Stabinc ina mitambo ya Aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na Vingora vya Tahadhari,ikasaidia kwa majambazi hao kushindwa kuingia ndani kuiba pesa za Benki hiyo kutokana na Vingora hivyo kupiga kelele na kuanza kuwapa uwoga majambazi hao ,ambapo walifanikiwa kuiba pesa za mteja mmoja ambae alikuwa anataka kuweka pesa kwenye benki hiyo,
Kova alisema Majambazi hao walipotoka nje ya Benki hiyo walipiga Risasi Juu ili kuwapa Hofu wananchi walikuwa Nje ya Benki hiyo,ambapo kwa Mujibu wa Kamishna Kova anasema bado wanaendelea kuwafuatilia majambazi hao.
 
a4cbe827c0fd405b84231ebb3b7b042b

Kwa hiyo ni nani aliyepora Sh65 milioni kwa kutumia silaha Benki ya Stanbic, tawi la Kariakoo, Julai 27 mwaka 2014?

Hili ni swali linalodai majibu baada ya Mahakama ya Rufani kumwachia huru Richard Otieno maarufu kama Gullo, raia wa Kenya katika kesi iliyoacha maswali mengi kuhusu umakini wa wapelelezi na uendeshaji mashitaka nchini.

Mahakama ya Rufani imemwachia huru Otieno ikisema upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kuwa fedha hizo ziliibwa huku ikionyesha makosa katika utambuzi wa mshitakiwa.
Watu wasiojulikana wakiwa na silaha walivamia Benki ya Stanbic tawi la Kariakoo na kupora fedha zilizodaiwa kuletwa na mteja mwenye asili ya Asia muda mfupi baada ya kufika tawini hapo. Mteja huyo alienda katika tawi hilo asubuhi akiwa amebeba mabegi mawili yaliyohisiwa kuwa na fedha.

Akiwa katika mlango wa benki, aliomba kusaidiwa kubeba mabegi hadi kaunta na alipofika kaunta mtu asiyejulikana alitokea nyuma yake na kumwekea bastola shingoni. Mteja huyo aliupiga mkono wa mhalifu na bastola ikaanguka hivyo kupiga kelele za kuomba msaada.
Ilidawa pia waporaji hao walimtishia ofisa masoko msaidizi wa benki hiyo, Paskas Marcel na ofisa wa kaunta, Godknows Alininkumbu kwa bastola na kuwaamuru walale chini.
https://www.24lottos.com/lottery/me...rwYTr5VOgp7H2Hw_IvCT-Zr0iDh90AotqTWqsaX54WeAQ

Wakiwa wamelala, wahalifu walipora fedha na kutoweka. Baadaye Otieno alikamatwa na kutambuliwa katika gwaride la utambulisho na wafanyakazi watatu wa benki hiyo kuwa ndiye aliyevamia.
Alikamatwa pamoja na mshitakiwa mwingine, Omary Mohamed ambaye aliachiwa pia kwa kukosekana ushahidi.

Licha ya matokeo ya gwaride la utambuzi, polisi waliofika eneo la tukio walikabidhiwa picha zilizopigwa na kamera za usalama (CCTV) zikionyesha jinsi uhalifu huo ulivyofanyika.
Mtaalamu wa Jeshi la Polisi aliyetafsiri picha zile alisema alimtambua Otieno kama mmoja wa majambazi waliovamia benki hiyo kwa mwonekano wa kichwa, nywele na utembeaji wake.

Katika utetezi wake, Otieno alisema siku ya tukio hakuwepo Dar es Salaam, kwani alikuwa Nairobi nchini Kenya na kupinga vikali utambuzi wa gwaride na picha za CCTV kwamba video hizo hazikuonekana vizuri na utambuzi haukufanywa kwa kufuata utaratibu.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikataa utetezi wake na kumhukumu kifungo cha miaka 30 jela, ikisema iliridhika na utambuzi wa gwaride na picha za CCTV.
Jaribio lake la kwanza kupinga kutiwa hatiani kisha kufungwa liligonga mwamba mwaka 2018 katika Mahakama Kuu iliyothibitisha uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aenda Mahakama ya Rufani Oktoba 2019, Otieno alikata rufaa Mahakama ya Rufani akidai upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitisha kosa dhidi yake.
Katika sababu zake za rufaa alisema ushahidi kuhusu utambuzi wake ulikuwa dhaifu na hapakuwa na ushahidi kutoka benki kuwa Sh65 milioni ziliibwa Hivi karibuni majaji wa Mahakama ya Rufani, Shaban Lila, Mwanaisha Kwariko na Ignus Kitusiwalikubaliana na hoja za rufaa ya Otieno katika hukumu iliyoonyesha udhaifu katika upelelezi wa kesi na uendeshaji mashitaka.

“Katika kesi iliyo mbele yetu, wakati maelezo ya kosa yanadai Sh65 milioni ziliibwa katika tukio la uporaji, ushahidi wa upande wa mashitaka hauonyeshi kama fedha hizo zilikuwepo,” walisema majaji.
Majaji hao walisema hapakuwa na ushahidi wowote wa nyaraka au wa kielektroniki kuthibitisha kuwa benki hiyo ilifanya hesabu na kugundua kiasi hicho cha fedha ndicho kilichoibwa kama ilivyodai.
“Tuna maoni kuwa ushahidi ulitakiwa kuonyesha benki ilikuwa na kiasi gani cha fedha kabla ya uporaji na kiasi gani kilibaki,” walisema. Majaji pia walisema ofisa wa kaunta ya benki aliyedai kuwa pesa zilichukuliwa kwake hakuitwa kutoa ushahidi kama alikuwa na kiasi hicho cha fedha au la.
Waliendelea kueleza kuwa licha ya shahidi wa upande wa mashitaka kudai kuwa pesa hizo ziliporwa kwa mtu mwenye asili ya Kihindi, mtu huyo hakuitwa mahakamani kutoa ushahidi. Majaji pia walikataa ushahidi wa wafanyakazi watatu wa benki waliodai kuwatambua waporaji hao.

“Ni maoni yetu kuwa mashahidi hawa wasingeweza kuwatambua waporaji kwa sababu ushahid wao wenyewe unaonyesha baada ya uvamizi ule waliamriwa kulala chini na walikuwa katika hali ya hofu,” walisema majaji. Walilikataa pia gwaride la utambulisho wakisema kama hawakuweza kumtambua katika tukio wasingeweza kumtambua katika gwaride hilo.
Pia mahakama ilikubaliana na Otieno kuwa picha za CCTV hazikuweza kuthibidisha sura yake kwa sababu askari aliyezitafsiri alisema wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo kuwa hazikuwa zikionekana vizuri. “Shahidi wa 11 wa upande wa mashitaka hakufafanua alimaanisha nini aliposema alimtambua mrufani (Otieno) kwa mwonekano wa kichwa na nywele.
Hakusema kichwa au nywele za mtu katika picha zilionekanaje ukilinganisha na mrufani. “Tunazingatia ukweli kuwa shahidi wa kwanza alisema jinsi alivyohangaika na mhalifu aliyekuwa na bastola, lakini shahidi wa 11 hakueleza ukweli huu katika picha za CCTV,” walisema majaji.
Katika rufaa yake, Otieno alikuwa akitetewa na wakili Nehemia Nkoko huku Jamhuri ikiwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Simon Wankyo.

Majaji wamshangaa hakimu Katika ukurasa wa mwisho wa hukumu yao, majaji wa Mahakama ya Rufani walionyesha kushangazwa na baadhi ya maneno yaliyotumiwa na hakimu aliyemhukumu Otieno, wakisema isingekuwa sawa kwao kumaliza hukumu yao bila kutoa neno kuhusu maneno hayo. Rekodi za mahakama zinaonyesha hakimu aliandika kwa Kiingereza maneno yafuatayo ambayo kwa tafsiri isiyo rasmi yalimaanisha ifuatavyo:
“Tanzania sio shamba la bibi ambalo raia kutoka nchi nyingine wanaweza kuja na kufanya uhalifu ili watunze familia zao.
“Ili kumpa fundisho, mshitakiwa Richard Otieno anahukumiwa kifungo cha miaka 12 jela pamoja na viboko 12, sita siku anaingia na sita siku anatoka jela ili aendapo nyumbani akamuonyeshe mkewe.”
Mahakama ya rufani haikuridhika na lugha iliyotumiwa na hakimu.

“Ni maoni yetu kuwa maneno kama hayo hayakuwa na ulazima na ni wazi yalikuwa nje ya kanuni za kuandika hukumu. Maneno hayo yanaonyesha kuwa hakimu hakuwa katika hali ya kutopendelea katika hukumu yake. Kwa hiyo, tunafikiri mwenendo huo unapaswa kukataliwa,” walisema.
Polisi waelezea tukio Siku moja baada ya tukio hilo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alikanusha kuwa Sh70 milioni ziliibwa Stanbic. “Hawakuiba chochote, lakini walipora kiasi kidogo tu cha pesa kisichojulikana kutoka kwa mteja aliyekuwa akihudumiwa benki,” alisema Kova.
Baada ya ving’ora vya usalama kupiga kelele, alisema waporaji hao walitoka nje na kuanza kupiga risasi huku wakiacha mabegi yao na kukuta yana mawe ndani
 
Back
Top Bottom