Kamanda Mambosasa: Saruji ipo ya kutosha jijini Dar, wanaopandisha bei ni wahujumu uchumi tutawashughulikia!

Kamanda Mambosasa: Saruji ipo ya kutosha jijini Dar, wanaopandisha bei ni wahujumu uchumi tutawashughulikia!

Huyu polisi ni nani kwani mpaka anaingia na kwenye mambo ya biashara kana kwamba ni waziri wa mambo hayo?

Huku ni kuchanganyikiwa sasa, siyo bure..

Pls, wewe polisi acha mamlaka zinazohusika na biashara zitoe matamko siyo wewe..

Mtu kama anauza mfuko mmoja wa simenti kwa Tshs 35,000 ina maana yeye kanunua kwa jumla kwa Tsh. 33,000..!

Na hivi vile viwanda 100 kila mkoa ina maana hakuna vya kutengeneza saruji??
 
Kwani unajuaje kama hajakabidhiwa jukumu tayari?
Jukumu la nini? Kwenye biashara siku zote kinacho affect bei ni demand and supply! Hii ni basic principle kwa watu ambao hata hawajaenda shule. Kamwe kinacho affect bei hakiwezi kuwa supply and police force! Huku tulishapitia tangu enzi za Mwalimu Nyerere na tunajua kuwa polisi hawawezi ku affect bei za bidhaa!
 
Kupandisha bei ni uhujumu uchumi, vipi kuhusu kushusha bei kama vile za "kolosho", pamba na "kaawa"?
 
Kwa hiyo nyumba ya msonge imefika thamani sawa na gorofa kutokana na kupanda bei ya material?
 
Haya mapolisi ya ccm nayo yameshakuwa irrelevant.

Siasa, maigizo na ujanja ujanja.
 
Hata mwezi bado cement bei juu, inauma sana.
 
Tokea nimsikie RPC fulani akisema ataanza kuwashughulikia watu wote atakaohisi wanataka kujinyonga nilishangaa sana
Nikajiuliza maswali mengi then nikakoncludi polisi wameanza kutoka katika mstari wao na ndio Kama huyu mambosasa kwenye hili
 
Je walionunua saruji kwa bei zaidi na iliyokuwa bei elekezi na risiti wanazo , serikali kwanini isiwachukulie hatua wasambazaji wa saruji maana ushahidi upo ...
 
MIMI tangu sukari ilipoadimika mkasema ipo nitakua wa mwisho kuamini haya mambo
 
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP), Lazaro Mambosasa amewataka wafanyabiashara kuuza cement kwa bei iliyowekwa na serikali vingiinevyo watashughulikiwa kisheria.

Mambosasa amesema jiji la Dar es Salaam lina cement ya kutosha hivyo yoyote anayeongeza bei ni muhujumu uchumi.

Chanzo: Channel ten

Maendeleo hayana vyama!
Polisi na masuala ya cement wapi na wapi??[emoji2955][emoji2955][emoji2955]
 
Back
Top Bottom