Ila ndugu zangu kuna mambo tunayohoji wakati mwingine yanashangaza sana!
Halafu hatuoneshi utayari wa kutaka kujifunza na kufahamu badala yake tunaonesha ujuaji na kama dharau fulani hivi.
Sasa Naomba kuwajibu wale wanaoshangaa polisi kujihusisha na tatizo la kupanda bei holela kwa bidhaa ya cement.
Ni hivi pale ambapo kunakuwa na viashiria vya biashara ya magendo, ulanguzi, utapeli kufanyika, n.k polisi huwa ni jukumu lao kuingilia kati ili kuiondoa hiyo hali sababu ni mojawapo ya aina za wizi zidi ya wananchi.
Ulanguzi, biashara ya magendo, utapeli, Ulaghai n.k hizo zote ni aina za wizi kwa wananchi !
Askari kazi yake ya msingi ni kulinda watu na mali zao.
Mtu akikuuzia cement kwa mfuko mmoja shilingi 16,000 badala ya 14,500 atakuwa amekuibia shilingi 1,500 ? Sasa piga hesabu kama unanunua mifuko mingi itakuwa amekuibia fedha nyingi kiasi gani?
Kutokujua siyo kosa kosa ni kujifanya unajua wakati hujui!
Tuungeni mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha !
Hata kama polisi wana mapungufu yao basi wasemeni kwa kosa au udhaifu mahsusi na siyo pale wanapofanya jambo sahihi mnataka kuwabeza itakuwa mnakosea!