Double Taxation (Makato Ya Kodi Mara Mbili) haina tofauti kisheria na Double Jeopardy (Hatari Mara Mbili - Kumtia Mtuhumiwa Hatarini) Na vyote viwili ni kosa/unyanyasaji kumfanyia mtu, hata kama ni mtuhumiwa.
Double Jeopardy, ni pale mtuhumiwa anaposhtakiwa mara mbili kwa kosa moja aliofanya. Mtu anasadikiwa kuua halafu Mwendesha Mashtaka anamfungulia kesi mbili kwa hilo kosa moja. Au mtu ameshahukumiwa kunyongwa kwa kosa la kuua halafu baada ya hukumu anafunguliwa kesi ya pili ya mauwaji ya yule mtu aliemuua tena. Na kama isingekua kosa basi watuhumiwa wangekua wanafunguliwa kesi 10 kwa kufanya kosa moja - Hii Ni Hatari.
Double Taxation, ni pale serikali/mtawala anapomtandika mtu kodi mara mbili kwa muamala mmoja wa kibiashara. Na kama isingekua kosa basi serikali zingekua zinawapiga kodi 10 wafanyabiashara kwa muamala mmoja wa kibiashara wanaofanya. Mfano unaagiza gari inapigwa kodi ya kwanza halafu inapigwa kodi ya pili kwa gari moja - Hii Ni Hatari.
Mwigulu Nchemba na kujitapa na elimu yake ya Phd ila ni kilaza asiejua taaluma yake. Angesomea VETA badala ya kusomea maswala ya Biashara & Uchumi. Maamuzi anayofanya katika Wizara Ya Fedha hata mtu ambae hajasomea Biashara & Uchumi hawezi kufanya (Hata umchukue mwanakijiji kutoka Kolomije ambae hajasoma shule ya msingi, hawezi akafanya upuuzi anaofanya Mwigulu).
Mwigulu ni Mzigo katika Serikali zote alizowahi kuteuliwa na kuzitumikia. Ila kwa taifa letu lilivyo la kipuuzi na upuuzi wa CCM msije kushangaa huko mbeleni akaja kuwa Rais au Waziri Mkuu.
Hii nchi ni kupambana kisawasawa kupata Katiba Mpya;
1) Mawaziri Wasiwe Wanatoka Bungeni (Wasiwe Wabunge).
2) DC & RC wapigiwe kura na wananchi ili kuchaguliwa, wasiwe wateule wa Rais.
3) Viongozi Wote Wasiwe Na Kinga Ya Kutokushtakiwa, atakaefanya ujinga aburuzwe Mahakamani (Hata Kama Makamo Wa Rais, Waziri Mkuu, Speaker).
4) Tume Ya Uchaguzi Huru.
5) Bunge Huru (Speaker Achaguliwe na Wabunge, sio Rais).
6) Mahakama Huru (Ma Judge Wasiwe Wateule Wa Rais, Wawe Wanapigiwa Kura Mbele Ya Jopo La Manasheria & Mahakimu & Judges). Hakuna kuteuliwa hovyo.