Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema sheria ya watoa taarifa kulindwa, haimaanishi watu kujikite kutoa za uongo, huku wakidai walindwe.
Kamanda Muliro ametoa kauli hiyo leo Aprili 28, 2024 alipotoa elimu kwa umma akijibu kilichoelezwa na Meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob maarufu Boni Yai na mwanaharakati Godlisen Malisa.
Baada ya wawili hao kuachiwa kutoka rumande jana Aprili 27, 2024, walitoa ujumbe kwa Jeshi la Polisi wakieleza watoa taarifa walipaswa kulindwa na si kupambana nao kwa kuwashikilia.
"Tuna sheria ya kuwalinda watoa taarifa. Watoa taarifa si wahalifu ila ni watu wenye nia njema kwenye nchi na kwa jamii na kulisaidia Jeshi la Polisi, wakitumiwa vizuri wanaweza kufanya kazi zao vizuri bila kuingia mgogoro au msuguano," alisema Malisa.
Jacob naye alisema: "Hatutaacha kupigania matukio ya watu kupotea na kutekwa hatutaki kumuonea mtu, tumehojiwa kwa hiyo sitegemei kama Jeshi la Polisi kutuona sisi maadui zao, watuone marafiki namna gani kuhakikisha watu hawapotei na wale wanaopotea wanapatikana."