Kamanda ambaye hakuna Mechi ya NBC Premier League iwe Kwa Mkapa au Chamazi anakosa sasa huo Utendaji wake hadi kufikia nae kupewa hiyo Nishani jana na IGP Wambura ni upi? Kama kuna Makamanda ambao nawakubali hasa Kiutendaji wao basi wale wa Tabora, Kigoma, Arusha, Rukwa, Morogoro, Lindi na Kwetu kwa Wanamume wa Shoka Mkoani Mara ( Musoma ) ila kwa RPC Muliro najua kapewa kwa janja janja tu ila hakustahili.
Unapenda sana kuandika magazeti ya upashkuna.
Unaandika as if wote tuliona tukio na tunafahamu unachokizungumzia.
Acha kuwashawashwa, kama unashindwa kuwasilisha jambo kwa muktadha wa kueleweka. Unaandika kama vile mikono ina funza, inawasha kiasi cha kushindwa kuandika vizuri.
Ungeandika tu vizuri, jana kulikuwa na tukio la kutunuku nishani kwa maafisa wa jeshi la polisi. Kisha useme RPC Muliro, alitunukiwa nishani fulani.
Ndipo useme kwa maoni yako, unadhani angepewa RPC fulani kwa sababu moja mbili tatu. Siyo upashkuna wa kijinga kweli.
Unamparamia Muliro kwa sababu tu anaenda viwanjani? Kwani viwanjani hapahitaji ulinzi na usalama? Kuna mechi ngapi ndani ya msimu mmoja? Zipi ambazo Kamanda Muliro kahudhuria?
Mkoa mgumu sana kiusalama ni Dar es Salaam. Ndipo kuna matapeli wengi, matumizi makubwa ya silaha, ukwepaji kodi, wizi, nk.
Bila shaka kuna kamati iliyofanya tathmini kwa undani na kupendekeza jina la anayestahili. Kumparamia yeye ni kukosa adabu.
Acha upumbavu.