Kamanda Muliro: Matukio ya kikatili kuna tatizo zaidi ya tunavyofikiria, kutegemea sheria haitoshi

Kamanda Muliro: Matukio ya kikatili kuna tatizo zaidi ya tunavyofikiria, kutegemea sheria haitoshi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Katika takwimu za matukio ya kikatili kwa baadhi ya watu mfano kubaka, ni tabia ambazo zimekuwa zikijirudiarudia, unakuta akihukumiwa maisha au miaka 30, akiwa jela anafanya tukio kama lilelile kwa mwanaume.

“Hapo unafikiri adhabu aliyopewa je, imemsaidia au la! Suala la maadili, kujitambua ni dawa kubwa kuliko adhabu zinazotolewa.

“Wapo watuhumiwa ambao ni watu wazima na wanaheshima yao lakini wanafanya matukio ya ajabu kama hayo, nadhani kuna tatizo zaidi ya watu wanavyofikiri," - Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Muliro Jumanne.


Chanzo: ITV
 
Tumejaza dispensary tukiamini mtu kichwa kikiuma Basi akapate Panadol kumbe msongo mawazo

Makanisa ya mchongo yamechukua nafasi kubwa ya ushauri nasaha

Serikali ilipo zahanati au kituo cha polisi fungueni ofisi za ushauri nasaha inashangaza hata kwenye mabaraza yakipolisi wachungaji ndo wamejaaa badala ya wataaluma wa ushauri
 
Dawa ya kansa ni kuondoa kile kiungo, sasa nyie munakipakaa dawa lazima itaenea maeneo mengine,
Mtu kaua au kabaka, badala ya kumkill
Munamfunga unafkiri atafanyeje?
Aliyeua naye auwawe,
Aliyebaka achinjwe
Hawatarudia tena
 
Back
Top Bottom