Kamanda Muliro, wewe na watu wote wanajua Polisi wawili uliowasimamisha kazi unawaonea, walichofanya ni utaratibu wa siku nyingi wa traffic polisi!

Wew ungetaka aamueje mkuu, yawezekan hayo anajua ila anapaswa kuwaajibsha au kuwajibika maan unachanganya mazoea na sheria
 
Mimi ndio nahalalisha, mimi ndio niliweka huo utaratibu, eboo!
Mbona unatetea rushwa na kudai ni Haki ya Polisi? Hakuna mahala Serikalini Wala Polisi Wameweka uhalali wa hicho unachotetea ndio maana wanaochukua wanajificha.

Pia nilisikia Serikali Ina Mpango wa kuondoa traffic barabarani na kuwa replaced na cameras
 
Kamanda Jumanne Muliro, tuache unafiki, tuache kuoneana. Unatutangazia kuwasimamisha hawa Polisi wawili walioonekana wakichukua fedha kwa makondakta wa dadadala kwa sababu wamefanya kosa au kwa sababu wameanikwa mitandaoni?
Amesema wamekosea kupokea rushwa hadharani
 
Mimi nawez kusema tuu uwajibikaji uanzie juu hadi chin utaleta maan san ndan ya governance
 

Sawa kwa hiyo ulitakaje yani?

Waachwe waendelee na kazi despite pure evidence kuwa wamekula rushwa?

Yaani ulitakaje mkuu?

Sio kila kitu mnakosoa.

Wamekula rushwa watakamatwa, mambo mengine yaendelee.

Again, ulitaka waachiwe waendelee na kazi au ulitakaje?
 
Kama vile ni lazima wale pesa

Sasa ndio hawa au wale wawili pekee?
Yaani hawa waliokamatwa ni za mwizi 40 zimetimia tu, wapo wengi sana huko. Hawa wachukua video ni kwamba wamechoshwa na tabia hii..!!
 
Sheria ambayo haijaandikwa inasema, we kula rushwa ili mradi usikamatwe kwa picha na video zitakazosambaa kwenye social media.
Kosa lao hapo si kula rushwa, ila ni kunaswa na video zikasambaa basi.
 
Ndio. Iwapo unajua trafiki wote wanafanya hivi, na imetokea tu hawa wamepigwa picha, kama kweli una nia njema kwa nini siku zote ukijua hilo umekaa kimya? Kuwafukuza hawa unafanya kosa lao ni kupigwa picha, sio kuchukua fedha, kwa sababu unajua kabisa kila trafiki anachukua fedha na na anapeleka mgao kituoni
 
Hebu warudishe kazini hawa askari wawili.
mbona unamfokea kwani amesha
wataja kuwa ni akina nani?
au ni wa kituo gani?
au wana vyeo gani?
au wamefanya nini zaidi ya kusema wamejihusisha na vitendo visivyo maadili?
 
Sheria ambayo haijaandikwa inasema, we kula rushwa ili mradi usikamatwe kwa picha na video zitakazosambaa kwenye social media.
Kosa lao hapo si kula rushwa, ila ni kunaswa na video zikasambaa basi.
Umenena vema sana Mkuu, kuna watu humu akili matope hawaelewi tunachoongelea hapa
 
mbona unamfokea kwani amesha
wataja kuwa ni akina nani?
au ni wa kituo gani?
au wana vyeo gani?
au wamefanya nini zaidi ya kusema wamejihusisha na vitendo visivyo maadili?
Uko wapi na wewe hufuatilii mambo? Ndio ameshasema wako mahabusu
 
Wew ungetaka aamueje mkuu, yawezekan hayo anajua ila anapaswa kuwaajibsha au kuwajibika maan unachanganya mazoea na sheria
Kama ana nia kweli aanze kula sahani moja na hao makamanda wanaowaambia askari wanaotumwa barabarani waache kudai mgao wao. Kisha kampeni ya kuwaambia madereva wa daladala, kenta, bajaji na gari za mchanga kutotoa rushwa. Pia akomeshe trafiki kulazimisha makosa kwa madereva.

Lakini sasa, kwa mishahara hii ya polisi sio rahisi kukomesha hili. Ndio maana nimesema jeshi la Polisi katika mazingira yao ya kazi halisafishiki
 
Kapokee rushwa na wewe tukunase uone
Mie natoa, sipokei, na imefikia mahali kwa hawa trafiki wala sioni ni rushwa tena, maana natoa bila hata wao kuniambia nina kosa lolote. Akifika tu nasema sema ofisa, hebu shika chai hii halafu nasepa. Sasa hapo nimetoa rushwa? Rushwa ni pale anakambia una kosa ndio unampa hela akuachie. Mie nawapa hela ya kubrashi viatu na kurefusha urefu wa kamba zao, kulingana na maagizo ya Amri jeshi Mkuu wa Tanzania
 
Inawezekana hatua ndio zimeanza kuchukuliwa labda.

Mi nadhani ili kuamini uungwana wa jeshi letu katika kukabiliana na rushwa kweli hasa za barabarani basi KILA MTU KWA MAHALA ALIPO AVIZIE MATUKIO KAMA HAYA NA KURUSHA HIVYO HIVYO MITANDAONI. Labda rushwa itakoma..
 
Ungemlaumu Magufuli basi, aliesema sio vibaya kuwapa askari elfu tano ya kubrashia viatu. Tena hawa askari wapole sana, wanakubali elfu mbili na sio elfu tano aliyoagiza Magufuli.

Unasema wanapokea rushwa, kunakuwaje rushwa wakati anaetoa hela ni konda sio dereva? Umeona hapo dereva akiambiwa amefanya kosa? Maana rushwa ni kutoa hela ili kukwepa kosa. Umeona dereva akitakiwa kulipa faini ndio akatoa rushwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…