Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Nilikuwa naangalia video hii (ina ubora wa chini sana) lakini ujumbe unafika.
Video inaonyesha matukio yaliyotokea siku ya kukaribisha askari wa Tanzania waliokuwa wakirudi kutoka vitani Uganda na matukio ya sherehe za siku ya mashujaa mwaka 1980 pale uwanja wa taifa wa zamani. Ndege moja ya kichina-Shenyang ilianguka pale pembeni mwa Chuo cha Chang'ombe na kumwua rubani wake ambaye alijitahidi kuhakikisha ndege haiangukii kwenye jukwaa kuu alipokuwa Nyerere. Kwenye dakika ya 1:17, kuna brigedia anatambulishwa kama Brigedia Ronald Mapunda. Kwa nini Kamanda huyu hajulikani sana katika historia zetu? Hata mimi niliyekuwa mfuatiliaji sana wa mambo ya kijeshi, sikuwa namfahamu. Je kuna mtu wa kuweza kutusaidia kumfahamu kamanda huyu na kuweza kurudisha jina lake katika kumbukumbu zetu kitaifa kwa mchango wake?